I made this widget at MyFlashFetish.com.

Friday, May 28, 2010

ZANZIBAR:

Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora Tanzania Jaji mstaafu Amir Ramadhani Manento ameonya masuala ya rusha katika uchaguzi mkuu ujao yanaweza yanaweza kulinagamiza taifa endapo halitadhibitiwa.
Akifungua mkutano wa baraza la tume hiyo mjini hapa amesema madhara ya rushwa katika uchaguzi yanaweza kuleta ubinafsi kwa viongozi watakaochaguliwa hivyo halina budi kupigwa vita kwa nguvu zote.
Jaji Mamento amehimiza kuelimishwa kwa wananchi haki yao ya kuchagua au kuomba kuchaguliwa bila kushwishiwa ili kuepusha vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo…
Mkutano huo wa tisa wa baraza la tume ya haki za binadamu unahusisha wawakilishi kutoka vyama vya wafanyakazi na baraza kuu la wafanyakazi serikalini.

ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwepo kwa vitendo vya uharamia kati ya visiwa vya Unguja na Pemba vinavyoripotiwa katika vyombo vya habari kunaweza kuathiri uchumi wa Zanzibar.
Akizungumza na zenji fm radio juu ya athari za vitendo hivyo kwa uchumi wa Zanzibar waziri anaeshughulikia masuala ya fedha na uchumi Dr. Mwinyihaji Makame amesema licha ya kutopata uthibitisho wa vitendo hivyo, lakini Zanzibar ni sawa na nchi nyingine ziliomo katika ukanda wa bahari ya Hindi inaweza kuathirika kiuchumi kutokana na uharamia huo.
Amesema iwapo meli za mizigo zinazotaka kuingia katika eneo la Afrika ya mashariki zinatishiwa na maharamia wa kisomali bila shaka hali ya uchumi wa Zanzibar itakuwa mbaya.
Hata hivyo Dr. Makame amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kufanya doria za kuwasaka maharamia hao walioripotiwa kuwepo katika kisiwa cha Pemba.
Kazi ya kuwasaka maharamia hao wa kisomali bado zinaendelea kwa ushirikiano wa jeshi la polisi, vikosi vya SMZ pamoja na jeshi la wananchi Tanzania JWTZ.
Akizungumza na Zenji Fm Radio juu ya msako huo kamanda wa kikosi cha kuzuia magendo KMKM kisiwani Pemba amesema kuwa kazi inaendelea vizuri na hadi sasa wananchi wanatoa ushirikiano mzuri…
Msako huo umekuja siku moja baada ya kuripotiwa watu wanaodaiwa maharamia waliotaka kuiteka nyara meli moja katika bahari ya Hindi upande wa Tanzania kukimbilia kisiwani Pemba.
Maharamia hao wamekimbilia Pemba baada ya kushambuliwa na majeshi ya jumuiya ya umoja wa ulaya wanaofanya doria katika pwani ya Afrika ya mashariki wakitaka kuiteka meli kati kati ya bahari ya visiwa vya Unguja na Pemba

Thursday, May 27, 2010

CHUO KIKUU CHA TUNGUU ZANZBAR

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Zanzibar, Tunguu mwaka wa pili, wameulalamikia uongozi wa chuo hicho kuwafukuza baada ya kukosa kusajiliwa kwa kile kilichoelezwa kushindwa kukamilisha malipo ya ada.
Akizungumza na Zenji Fm radio mmoja wa wanafunzi hao amedai chuo hicho kimeongeza ada ya masomo kinyume na mkataba wao wa zamani hivyo wameshindwa kulipa ada hiyo na kulazimika kufukuzwa.
Amedai kutokana na kufukuzwa chuo kinyume na sheria wanatarajia kufungua kesi mahakamani wiki ijayo kutokana na kufukuzwa kwa zaidi ya wanafunzi
Hata hivyo uongozi wa chuo hicho haukuweza kupatikana kuelezea juu ya madai hayo ya wanafunzi kufukuzwa chuoni hapo.

PEMBA

Watu tisa wanaodaiwa maharamia waliotaka kuishambulia meli ya Namtuna katika eneo la kati kati ya kisiwa cha Unguja na Pemba wamefukuzwa na halikopta ya askari wa umoa wa Ulaya na inadaiwa maharamia hao wamekimbilia Pemba.
Askari hao waliokuwa doria katika helikopta hiyo ya umoja wa Ulaya wamesema tukio hilo limekuja siku tatu tangu kutokea kwa tukio jingine katika kisiwa cha Sheli sheli.
Kiongozi wa opereseheni wa umoja huo unaofanya doria katika pwani ya Afrika ya Mashariki amesema wamepigiwa simu kuhusiana na kuwepo kwa tukio hilo kati kati ya visiwa vya Pemba na Unguja na hivyo kutuma helikopta hiyo na hatimae kuikoa meli hiyo na maharamia hao kukimbilia Pemba.
Amesema maharamia hao wameshindwa kuwafuatilia baada ya kuingia katika eneo la Pemba kutokana na sheria haziwapi mamlaka ya kuingi katika pwani ya Tanzania.

Akizungumzia tukio hilo mwana sheria mkuu wa serikali jaji Fred Tungelema amesema wakati umefika kwa serikali ya Tanzania kuweka mpango wa kuliwezesha jeshi kulinda maeneo yote ikiwemo bahari kuu
Kamanda wa polisi wa mkoa wa kusini Pemba Hassan Nassir amesema tukio hilo bado halijathibitishwa na kusema maharamia hao kukimbilia kisiwani humo ni uvumi.
Hivi karibuni mkurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar Mustafa Abudo Jumbe amesema tatizo la maharamia katika pwani ya Afrika ya Mashariki limesababisha wenye meli kupandisha gharama za usafirishaji wa mizigo.
Akizungumza katika mkutano uliojadili ushiriki wa Zanzibar katika soko la pamoja la Afrika Mashariki amesema hali hiyo inaweza kudhorotosha shughuli za bandarini na kuongezeka kwa bei za bidhaa.

DAR ES SALAAM:

Chama cha jamii C.C.J kimesema kiko tayari kutoa fedha ili kuharakisha mpango wa unaotakiwa kufanywa na afisi ya msajili ya vyama vya siasa nchini ili kukiwezesha chama hicho kupata usajili wa kudumu na kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa chama hicho Fedrick Mpendazoe mjini Dar es Salaam ambae amepinga kile inachodaiwa hujuma zinazofanywa na msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa dhidi ya chama hicho.
Hata hivyo Tendwa amesema hakuna utaratibu wa chama kuharakisha mpango unatakiwa kufanywa na afisi ya msajili wa vyama vya siasa ili kukiwezesha chama kupata usajili wa kudumu.

ZANZIBAR:

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeishukuru serikali ya watu wa China kwa juhudi inazochukua katika kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza umasikini kwa wananchi.
Waziri anaeshughulikia fedha na uchumi Dr. Mwinyihaji Makame ametoa pongezi hizo katika hafla fupi ya utiaji wa saini wa mradi wa kupunguza malaria uliotolewa na serikali ya China.
Amesema mbali na China kutoa misaada mbali mbali ya kiuchumi na kijamii lakini pia imekuwa ikisaidia sekta ya afya ikiwa ni miongoni mwa juhudi za serikali za kuimarisha sekta hiyo ili kupunguza umasikini.
Dr. Makame amesema msaada huo wa China wa kupambana na ugonjwa wa malaria utaisaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vinavyotoka na maradhi hayo yanayowasumbua wananchi.
Nae balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Le Jiang Pehn amesema mradi huo utagharimu zaidi ya dola za Marekani laki moja na elfu 46.
Serikali ya China imetoa misaada kadhaa kwa Zanzibar ikiwemo dawa, matrekta ya kulimia, matengenezo ya uwanja wa Amani pamoja na umarishaji wa vyombo vya habari.

Sunday, May 23, 2010

MASAUNI MASHAKANI

Jeshi la polisi nchini limesema linafanya uchunguzi wa nyaraka na vielelezo kuhusu umri wa mwenyekiti wa zamani wa jumuiya ya vijana ya chama cha mapinduzi UV-CCM, Hamad Masauni.
Hatua hiyo ya jeshi la polisi imekuja baada ya Masauni kudaiwa kuhushi umri wake wakati wa kugombea wadhifa huo mwaka 2008.
Naibu kamishna wa jeshi la polisi anekaimu ukurugenzi wa makosa ya jinai Piter Kibuyo amesema taarifa za vielelezo vya uchunguzi vitatolewa baada ya uchunguzi huo kukamilika.
Amesema katiba ya nchi inaeleza hakuna mtu alieko juu ya sheria hivyo iwapo Masauni ataonekana amehushi umri wake sheria itachukua mkondo wake
Masauni alitarajiwa kupokelewa leo kwa mapokezi ya aina yake, lakini umoja wa vijana wa UV-CCM, Zanzibar umesema hausiki na mapokezi hayo.
Uchunguzi uliofanywa na Zenji fm radio umegundua mapokezi hayo yaliandaliwa na baadhi ya vijana wa CCM kutoka jimbo la uchaguzi analoishi Masauni.

DAR ES SALAAM

Waziri wa fedha na uchumi Mustapha Nkulo amesema mkopo wa Tanzania kutoka benki ya Stanley ni sehemu ya fedha zinazohitajika kuziba pengo baada ya washirika wa maendeleao kupunguza kiasi kikubwa cha fedha.
Waziri mkulo amesema hayo alipokuwa akitoa ufafanuzi wa matumizi ya fedha za mkopo wa dola za Marekani milioni 250 kutoka benki hiyo baada ya nchi hizo kupunguza misaada ya bajeti ijayo ya serikali ya Tanzania.
Nchi wahisani zimepunguza zaidi ya shilingi bilioni 220 kutoka bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha na kuifanya serikali kutafuta mikopo kutoka taasisi nyingine za fedha zitakazosaidia kuziba pengo hilo.

ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume ameondoka nchini kuelekea China kwa ziara maalum ya wiki moja.
Akiwa nchini humo rasi Karume athudhuria maonyenyesho ya biashara ya Kimataifa yatakayofanyika mjini Shanghai China.
Katika ziara yake hiyo Rais Karume anafuatana na mkewe Mama Shadya Karume na viongozi na maafisa wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Miongoni mwa viongozi hao ni waziri wa Utalii, Biashara na uwekezaji Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Seif Ali Iddi na viongozi wengine wa serikali zote mbili.
Mara baada ya kumaliza ziara ya wiki moja ya nchini China, Rais Karume anatarajia kwenda nchini Qatar kwa ajili ya kuhudhuria mkutano Mkuu wa Kiuchumi Duniani utakaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha.

DAR ES SALAAM:

Wakaazi wa mkoa wa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ikiwa ni awamu ya pili ya kazi za uimarishaji wa daftari hilo.
Kazi za undikishaji hizo zimeanza leo na zinararajiwa kumalizika kesho katika vituo vyote vilivyotengwa kwa shughuli hiyo.
Jumla ya vituo elfu 24, 813 vimepangwa kutumika katika awamu ya pili ya undikishaji wa wapiga kura katika mkoa wa Dar es Salaam.
Awamu ya kwanza ya uandikishajiwa wapiga kura katika mkoa wa Dar es Salaam ilifanyika Marchi 22 kwa muda wa wiki moja na baadae kuongezewa siku mbili kutaokana na kazi hizo kukumbwa na kasoro kadhaa.

ZANZIBAR:

Jaji wa mahakama kuu ya Zanzibar Mshibe Ali Bakar ameonya juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria vinavyoendelea kutokea siku hadi siku hapa Zanzibar.
Akizundua ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2009 mjini hapa amesema ripoti hiyo inahitaji kufanyiwa kazi ili kuona yale yaliotokea katika mwaka huo ikiwemo uvunjaji wa haki za binadamu hayatokei tena.
Amesema vitendo vya uvunjaji wa sheria vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara katika maeneo yote nchini na kutishia amani ya nchi, hivyo ni vyema kwa taasisi husika kuifanyika kazi ripoti hiyo.
Mshibe amesema nchi kadhaa zimepata mafanikio katika kupunguza vitendo vya uvunjaji wa sheria na haki za binadamu kutokana na ripoti kama hizo, hivyo ni vyema kuwepo na ufuatiliaji wa ripoti hiyo.
Ripoti hiyo iliyoandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar pamoja na mambo mengine inazungumzia ukosefu wa ushahidi katika undelezwaji wa kesi.

ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wananchi wanaofuga chui kujitokeza hadharani na wanyama hao ili kusaidia ukuwaji wa sekta ya utalii nchini.
Mkuu wa hifadhi ya msitu wa Jozani mkoa wa kusini Unguja Ali Mwinyi amesema serikali haiwakatazi wananchi wake kufuga chui iwapo wanayama hao wanawatumia kwa nia njema.
Amefahamisha Zanzibar inaendelea kuimarisha sekta ya utalii hivyo wanyama aina ya chui ni moja wapo ya vivutio kwa watalii na kwamba kuwepo hadharani kwa wanyama hao ni sawa na kuwepo hoteli ya nyota tano…
Mwinyi amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika miaka ya 90 umeonyesha chuwi wengi waliopo katika kisiwa cha Unguja asilimia 60 wanafugwa na wananchi na waliosalia wanaishi msituni.
Wananchi wa Zanzibar wanaamini watu wanafuga chui kwa imani za kishirikina, hivyo kauli hiyo ya serikali iliyotolewa miaka kadhaa iliyopita haiwezi kuleta mafanikio iwapo elimu zaidi haitatolewa.

Friday, May 21, 2010

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM YUSSUF MAKAMBA AMESEMA


Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Yussuf Makamba amesema maandalizi ya mkutano mkuu wa chama hicho utakaomchagua mgombea urais wa Tanzania yanaendelea vizuri.
Akizungumza na Zenji Fm radio kuhusiana na kikao cha kamati kuu kilichofanyika jana mjini Dar es Salaam amesema mkutano huo utakaofanyika July 10 na 11 mjini Dodoma pia utapokea ratiba ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, kupitisha mwelekezo wa CCM 2010-2020 na kupokea taarifa ya uchaguzi ya 2010-2015.
Aidha Makamba amesema mkutano huo utateuwa majina ya wagombea kupitia chama hicho katika nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge kwa majimbo yote ya Tanzania bara na Zanzibar

MASAUNI KUPOKEWA KWA SHANGWE ZNZ?


Jumuiya ya vijana ya chama cha Mapinduzi UV-CCM imesema haiuhusiki na maandamano yanayotarajiwa kufanyika kesho kwa ajili ya mapokezi ya mwenyekiti wa zamani wa jumuiya hiyo Hamad Masauni.
Kauli hiyo ya jumuiya imekuja kufuatia kuwepo kwa taarifa zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa umoja huo kutaka kuandaa mapokezi ya mwenyekiti huyo wa zamani aliejiuzulu hivi karibuni akidaiwa amejipunguzia umri.
Akizungumza na wandishi wa habari katibu wa vijana wa CCM Zanzibar Shamhuna Mohammed Ibrahim amesema jumuiya hiyo haijaandaa mapokezi ya aina yoyote kwa mwenyekiti huyo wa zamani.
Hivyo amewataka vijana kuacha kutumiliwa na wanasiasa wachache kwa lengo la kuchafua hali ya kisiasa ndani ya umoja wa vijana wa CCM.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari katika jumuiya hiyo kimesema lengo la mapokezi hayo ni kumfariji na kuonesha mshikamano wao kuwa bado wanampenda na kilichotokea ni bahati mbaya.

Waandaaji wa maandamano hayo walidai yatawashirikisha vijana wa mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba kwa kuvaa sare maalum.
Kujiuzuli kwa Masauni kutawafanya vijana wa CCM Zanzibar kutokikalia kiti hicho kwa muda mrefu tokea kuandoka Mohammed Seif Khatib ambaye sasa ni mbunge wa jimbo la Uzini na waziri anaeshughulikia masuala ya muungano.
Hamad Masauni ambae amejiuzulu pamoja na naibu katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Mohammed Moyo wanatazamiwa kutaka kuwania nafasi ya ubunge katika majimbo ya Kikwajuni na Kwahani mjini Zanzibar.
Hatua ya kujiuzulu kwa Masauni imetokana na taarifa zilizotolewa katika vyombo vya habari za kujipunguzia umri wakati wa kuwania wadhifa huo na Moyo amesema amejiuzulu kwa sababu zake binafsi.
Masauni na Moyo walichaguliwa kushika nyadhifa hizo mwishoni mwa mwaka 2008.

DAR ES SALAAM

Waziri wa fedha na uchumi Mustapha Nkulo amekiri baadhi ya mataifa ya nchi wahisani wamepunguza kiasi cha dola za Marekani milioni 220 katika bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha.
Hata hivyo amesema tayari serikali imeshakopa dola za Marekani milioni 250 kutoka benki ya Stanlet kwa masharri nafuu ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kutokana na upungufu wa fedha hizo.
Nkulo amesema hayo mjini Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kutolea ufafanuzi taarifa ya mataifa ya wahisani kusitisha msaada wao katika bajeti ijayo ya serikali

Thursday, May 20, 2010

TCU IMEKIRI KUWEPO TATIZO LA USAJILI WA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA MASOMO KATIKA VYUO VIKUU NCHINI

Afisa habari kutoka tume ya vyuo vikuu nchini TCU Edward Mkaku amekiri kuwepo tatizo la usajili wa wanafunzi wanaojiunga na masomo katika vyuo vikuu nchini.
Bw Mkaku amesema moja ya matatizo katika usajili huo ni mtandao unaotumika katika utumaji maombi ya kujiunga na elimu hiyo kushindwa kumudu wimbi kubwa kutoka kwa wanafunzi wanaotumia huduma hiyo.
Akizungumza na shirika la utangazaji Tanzania Mkaku amesema Tume ya vyuo Vikuu inachukulia suala hilo kama changamoto ya maendeleo ya teknlojia na mawasiliano hususani katika kupunguza gharama kwa watumiaji.

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMETOA MSAADA WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 27

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 27 kusaidia watu waliopatwa na maafa ya kubomokewa na nyumba zao kufuatia upepo uliovuma miezi kadhaa katika shehia za Kilimahewa, Kwamtipura na Amani.
Akikabidhi hundi yenye tahamani ya fedha hizo kwa mkuu wa mkoa wa mjini magharibi waziri wanchi afisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma amesema serikali kwa kujali wananchi kutokana na hasara walioipata imeona ipo haja ya kuwafariji kwa msaada wa fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari waziri Hamza amesema fedha hizo zimetolewa baada ya kamati maaluma iliyounda kutahmini maafa hayo na kuitaka afisi ya mkuu wa mkoa kuhakikisha fedha hizo zinawafika walengwa.
Akipokea hundi hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa mjini Magharin afisa tawala wa Mkoa huo Amour Haji Nassor amewapongeza wnanchi walipata maafa hayo kwa ustahamilivu wao
Kiasi ya nyumba 74 ziliharika baada ya kuzuka upepe mkubwa katika maeneo ya Kilimahewa ,Kwamtipura na Amani

JAPAN KUSAIDIA TANZANIA

Serikali ya Japan imesaini mkataba wa kuipatia Tanzania msaada wa mchele wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 14 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la chakula nchini.
Utiaji saini wa msaada huo umefanywa mjini Dar es Salaam na Balozi wa nchi hiyo kwa niaba ya nchi yake na katibu mkuu wizara ya fedha nchini kwa niaba ya Tanzania.
Fedha zitakazopatikana baada ya kuuzwa mchele huo zinatarajiwa kutumika katika kuinua sekta ya kilimo.

LIPUMBA ASEMA ZANZIBAR HUENDA IKAKOSA NAFASI KUNUFAIKA KIUCHUMI KATIKA SOKO LA PAMOJA LA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI


Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF, Profisa Ibrahim Haruna Lipumba amesema Zanzibar huenda ikakosa nafasi kunufaika kiuchumi katika soko la pamoja la jumuiya ya Afrika ya mashariki kutokana na kukosa viwanda vya uzalishaji wa bidhaa.
Profisa Lipumba ambae ni mchumi ameiambia Zenji Fm radio kwamza ili kuondokana na hali hiyo Zanzibar inahitaji kuweka miundo mbinu ya kuanzisha viwanda vitakavyotoa bidhaa mbali mbali ili kuuza katika soko hilo…
Hata hivyo amesema Zanzibar bado inahitajika kuzisindikiza taasisi za fedha na benki zinazotoa mikopo kwa kuweka masharti na riba nafuu kwa wafanyabiashara.
Jumuiya ya Afrika ya mashariki iliyoanzisha mwaka 1999 tayari imeshatekeleza itifaki za ushuru wa forodha, soko la pamoja na baadae inatarajiwa kutumia sarafu ya pamoja na hatimae kuwa shirikisho la kisiasa.

COSOZA YAVAMIA MADUKA YA KASETI LEO

Afisi ya haki miliki imefanya msako maalum katika madula yanayokodisha na kuuza kanda za kazi za wasanii ambayo hayajafanya malipo ya kuuza kazi hizo za wasanii.
Akizungumza katika msako huo msimamizi na mtendaji mkuu wa afisi hiyo Mtumwa Khatib Khamis amesema lengo lao ni kuhakikisha haki za wasanii na wabunifu zinalindwa.
Amesema biashara ya sanaa imekuwa ikiwanufaisha wafanyabiashara pekee lakini wabunifu wanofanya kazi hiyo kama vile mziki, maigizo na sanaa za maumbo.
Msimamizi huyo amesema afisi yake imetoa elimu ya kutosha kwa wananchi na wanyabiashara wanaotumia kazi za sanaa kwa muda wa miaka mitatu sasa ili kujisajili na kufanya malipo lakini baadhi yao wameonekana kudharau juu ya hatua hiyo
Msako huo umefanyika katika maeneo ya Amani,Mpendae, Meli nne na tano barabara ya kuelekea Fuoni, Kwa Alinatuu na mali zilizokamatwa zinatarajiwa kuangamizwa na afisi hiyo.
Jumla ya wafanyabiashara wa maduka ya kanda 65 wamejisajili katika afisi hiyo kati ya hao wafanyabishara watano tuu ndio waliolipa kazi za sana hiyo.

MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR IMEFUNGA USHAHIDI WA KESI YA MAUWAJI YA AFISA WA UBALOZI MDOGO WA CHINA HWANG HONG XING YALIYOTOKEA SEPTEMBA 2006

Mahakama kuu ya Zanzibar imefunga ushahidi wa kesi ya mauwaji ya afisa wa ubalozi mdogo wa china Hwang Hong Xing yaliyotokea Septemba 2006 huko Mazizini baada ya kuwasikiliza mashahidi 12 wa upande mashitaka.
Akitoa kauli hiyo Jaji Abraham Mwampashi anaesikiliza kesi hiyo amesema Mahkama itatoa uwamuzi wake June 16 mwaka huu iwapo watuhumiwa wanakosa la kujibu au la.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mwendesha mashitaka wa Serikali Sleiman Masoud kusema afisi ya mkurugenzi wa mashtaka imekamilisha orodha ya mashahidi wa upande wa mashtaka.
Awali mahakama kuu ilikataa kupokea silaya aina ya SMG inayotadia kutumika katika mauwaji hayo kama kilelezo cha ushahidi kutokana kutokana na kuzuka utata wa kutofautiana kwa namba za silaha hiyo.
Watuhumiwa wanaohusishwa katika kesi hiyo ni Salum Abdalla mkaazi wa Baja, Hassan Abdalla wa Michenzani, Khamis Ali Abdalla wa Meli nne, Bimkubwa Saidi wa Fuoni Meli tano.
Wengine ni Faki Ali Hassan wa Dar es Salam, Miraji Mohammed wa Bububu na Abdulkadir Mohd wa Kiembesamaki wote kwa pamoja wanadaiwa kumuuwa afisa wa kibalozo Xing Septemba 11 mwaka 2006

MASAUNI AJIUZULU


Habari tulizozipata katika chumba chetu cha habari zinasema mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa chama cha Mapinduzi UV-CCM bwana Masauni amejiuzulu katika mkutano wa jumuiya hiyo unaofanyika mkoani Iringa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari katika mkutano ameiambia Zenji Fm radio naibu katibu mkuu wa UV-CCM upande wa Zanzibar bw. Mohamme Moyo nae pia amejiuzulu.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa UV-CCM wilaya ya Kinondoni mjini Dar es Salaam Emanuel Malema amesema mabishano kati ya viongozi hao na wajumbe wengine wa mkutano huo yalikuwa makali.
Amesema malumbano hayo yanatokana na wanasiasa wachache kuwatumia vijana wa Jumuiya hiyo kwa maslahi yao binafsi.

Aidha Malema alifahamisha shutuma anazotupiwa Masauni za kuhushi umri wake ni njama za wanasiasa wachache waliomo ndani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Viongozi hao waliojiuzulu Masauni na Moyo wanadaiwa kujipunguzia umri katika vikao vilivyohusika kupitisha majina yao wakati walipogombea nyadhifa hizo.
Hivi karibuni bw. Masauni alitanagaza nia yake ya kutaka kuteuliwa na chama chake cha CCM kuwa mgombea wa ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu

ZANZIBAR NA SOKO LA PAMOJA

Zanzibar imeelezewa huenda ikawa msindikizaji katika soko la pamoja la Afrika ya Mashariki linalotarajiwa kuanza hivi karibuni kutokana na kutegemea bidhaa kutoka nje ya nchi kwa asilimi 97.
Mwakilishi kutoka Jumuiya ya wafanyabiashara, wenyeviwanda na wakulima Msellem Khamis amesema Zanzibar inasafirisha bidhaa zake nje ya nchi kwa asilimia tatu hali ambayo inaweza kuiathari mara baada ya soko hilo kuanza Julai mwaka huu.
Aidha amesema wafanyabiashara wengi wa Zanzibar hawana uwezo wa kujiendeleza kibiashara kutokana na masharti magumu na riba kubwa zinatozwa na benki zinazotoa mikopo ikilinganishwa na nchi jirani.
Amefahamisha kuwa serikali ya Kenya ambayo inawasaidia wafanyabiashara wake kwa kuwapa mikopo yenye masharti na riba nafuu hadi kufikia mwaka 2007 zaidi ya wawekezaji 45 wamewekeza Tanzania.
Hivyo bw. Mselem ameiomba serikali ya mapinduzi Zanzibar kuwasaidia wafanyabishara wa ndani pamoja na kuzijengea uwezo wa kitaalamu sekta binafsi ili waweze kuleta ushindani katika soko hilo.

Nae mfanyabiashara wa Zanzibar Salum Turki amesema ipo haja kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuisiadia Zanzbiar kuimarisha sekta ya viwanda kutokana na hali yake ya kigeoraphia
Aidha baadhi ya wajumbe wengine wa mkutano huo wamelezea soko la pamoja la nchi za Afrika Mashariki linaweza kuisaidia Zanzibar kupanua sekta ya uwekezaji na nafasi za ajira kwa wananchi.
Jumuiya ya Afrika ya mashariki iliyoanzisha mwaka 1999 tayari imeshatekeleza itifaki za ushuru wa forodha, soko la pamoja na baadae inatarajiwa kutumia sarafu ya pamoja na hatimae kuwa shirikisho la kisiasa.

MAKONTENA 50 YA SARUJI YAINGIZWA Z`BAR BILA KODI


Makontena 50 ya saruji yenye thamani ya Sh. milioni 114.8 yameingizwa Zanzibar yakitokea nchini Pakistan bila kulipiwa kodi kupitia Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.

Uchunguzi umegundua kuwa makontena hayo yaliingizwa visiwani humu kufuatia msamaha wa kodi uliotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini.

Kibali cha msamaha wa kodi kimetolewa Mei 12, mwaka huu chenye kumbukumbu namba WF/EXEMPT/TA/2010/VOL.II/NO.2 akitakiwa Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Zanzibar kutotoza kodi ya ushuru wa forodha mzigo huo.

Shehena hiyo ya Saruji ililetwa Zanzibar na meli ya mizigo ya MV Concord ikitokea Karachi nchini Pakistan na kuwasili Zanzibar wiki iliyopita. Nyaraka za usafirishaji mzigo huo yenye kumbukumbu namba Karzan-091 ya Aprili 24, mwaka huu, inaonyesha makontena hayo yaliletwa na kampuni ya uwakala wa mizigo ya Abdul Enterprises C/F Company ya Darajani mjini Zanzibar.

Kampuni hiyo imepewa kazi ya kuingiza saruji hiyo na Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ.

Kwa mujibu wa msamaha wa kibali cha msamaha wa kodi cha waziri saruji hiyo haitakiwi kutozwa ushuru wa forodha pamoja na Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT)

Hata hivyo, saruji hiyo imeanza kuingia katika soko la ndani la Zanzibar na kuuzwa katika maduka ya rejareja. Mzigo huo wa saruji uliingizwa nchini kwa kutumia nyaraka za usafirishaji zenye namba 20100425CON703ZNZ ya Aprili 25, mwaka huu. Uchunguzi imebaini saruji inathamani ya dola za Marekani 84,000 Aprili 10, mwaka huu kutoka kampuni ya uwakala ya HMG International Agencies yenye makao makuu yake Karachi, Pakistan.

Naibu Kamishina wa TRA Kanda ya Zanzibar, Hassan Mcha, alithibitisha jana makontena hayo kutolewa bila ya kulipiwa kodi kutokana na msamaha wa kodi uotolewa na Waziri wa Fedha Zanzibar.

Akizungumza na Zenjfm Dk. Makame alithibitisha kutoa msamaha huo lakini alisema hana taarifa kama saruji hiyo imeanza kuingizwa katika soko la ndani la Zanzibar.

Sunday, May 16, 2010

MREMA ASEMA HAAMINI KUWA KAULI YA RAIS KIKWETE YA HIVI KARIBUNI JUU YA TAKRIMA ILIKUSUDIA KUHALALISHA TAKRIMA


Katika mbio za kuelekea uchaguzi mkuu Tanzania unaotegemewa kufanyika Oktoba mwaka huu, wanachama na wanasiasa wa vyoma tofauti nchini wamekuwa wakitangaza nia za kugombea nafasi tofauti katika vyama vyao.
Miongoni mwa wanachama hao ni pamoja na Bw Mtanegwa Mhinywa na Bw Maxmilian Lyimo wa TLP wametangaza nia ya kugombea kiti cha urais katika serikali ya jamhuri ya muungano wa Tananzia.
Akithibitisha hayo Mwenyekiti wa TLP Taifa B w Augustine Lyatonga Mrema amesema kuwa endapo mmoja kati yao atakuwa na sifa kwa mujibu wa taifa letu na wakapitishwa na mkutano mkuu wa chama chake wataruhusiwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.Bonyeza HAPA kumsikia Bw Augustine Mrema...Athibitisha baadhi ya wanachama kutangaza nia ya kugombea urais
Kwa upande wa tarifa iliyopewa nafasio kubwa mwishoni mwa wiki katika vyombo vya habari kuwa Rais Kikwete juzi mbele ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, muda mfupi kabla ya kufunga mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ambao ulijadili masuala ya uchaguzi na sheria zake amekiri kuwa kuikomesha takrima ni jambo gumu kwa sababu utamaduni wa Mtanzania umejengwa kwa misingi ya kumkirimu mgeni, kauli ambayo imechukuliwa kwa hisia tofauti na baadhi ya wnasiasa na wananchi.
Kufuatia hili Nyota Matukio ilitaka kufahamu kwa upande wake Bw Mrema ana maoni gani juu ya kauli hiyo..bonyeza HAPA kumsikia Bw Augustine Lyatonga Mrema...Maoni yake juu ya kauli ya Rais ya Takrima
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Nyota Matukio haikuishia hapo pia ilimtafuta mwanasiasa na mhadhiri katika chuo kikuu cha Dra es salaam Dr Sengondo Mvungi ambae ni mwalimu wa sheria na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha NCCR Mageuzi ambae amesema kuwa, kauli hiyo ni kupigwa vita vita na watanzania kwa nguvu zote kwa vile kufanya hivyo ni kuvunja katiba ya nchi.
Dr Mvungi amesema kuwa kama Rais Kikwete ameamua kutoa kauli hiyo, ina maana kuwa chama chake cha CCM kiko tayari kuvunja katiba na sheria na hatimaye kutoa takrima..Bonyeza HAPA kumsikia Dr Sengodo Mvungi....Maoni yake juu ya kauli ya Kikwete kuh takrima
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Baada ya kusikia kauli tofauti kutoka kwa wanasiasa mbali mbali Nyota matukio iligeukia upande wa chama tawala ambacho kinashutumiwa kuwa ni chama cha rushwa ambapo tulibahatika kuzungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Capt John Chiligati ambae amesema kuwa kauli ya Rais Kikwete imepotoshwa kwa makusudi na baadhi ya vyombo vya habari na amekanusha kuwa Rais amesema takrima ni kuksa.
Chiligati amefafanua kuwa Rais alikuwa anatoa maelezo kuwa baadhi ya maeneo utekelezaji wa sheria hiyo ni mgumu kutokana na mila na desturi za baadhi ya maeneo nchini na sio kuruhusu takrima kama ilivyoandikwa na baadhi ya magazeti.
Aidha Chiligati amesema kuwa sheria ya takrima iko pale pale na hivi karibuni bunge lilipigilia msumari wa moto sheria hiyo ambapo amedai kuwa hata wakati wa kura za maoni endapo watu watatoa takrima ni rushwa na atakaebainika sheria itachukua nafasi yake..Bonyeza HAPA kumsikia John Chiligati....Kauli ya Kikwete kuh takrima yapotoshwa

WAFANYA BIASHARA ZANZIBAR

Baraza la biashara Zanzibar limesema suala ya wafanyabiashara wa Zanziar kutozwa kodi mara mbili Tanzania bara linaweza kuathiri shughuli zao mara baada ya kuanza kwa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika mashariki Julai mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari katibu mtendaji wa baraza hilo Ali Vuai amesema licha baraza hilo kuyapatia ufumbuzi zaidi ya matatizo 60 yanayowakwamisha wafanyabiashara wa Zanzibar, lakini suala hilo haliko mikonini kwa Zanzibar.
Hata hivyo amesema suala hilo linaendelea kujadiliwa katika vikao vya kero za muungano vinavyohusisha mawaziri wa pande mbili za muungano chini ya mwenyekiti wake makamo wa rais wa Tanzania…
Aidha Vuai amesema katika kuwatayarisha wafanya biashara wa Zanziar kuingia katika soko la pamoja la jumuiya ya Afrika mashariki Jumanne ijayo litaendesha mkutano utakao wajumuisha zaidi ya wajumbe 300 kutoka ndani na nje ya Zanzibar.
Amesema lengo la mkutano huo ni kuwaemisha wafanyabiashara wa Zanzibar juu ya umuhimu wa kulitumia soko hilo pamoja na kuyapatia ufumbuzi matatizo yao watakayokabiliana nayo katika soko hilo….
Nae mkurugenzi wa Idara ya biashara Zanzibar Rashid Ali akizungumzia suala la misamaha katika soko hilo amesema misamaha ya bidhaa haitaombewa kwa mtu mmoa bali itaombewa kwa wafanyabiashara wote watakaoingiza bidha zinazoombewa msamaha…….

ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Seif Sharif Hamad wanatarajiwa kufanya uzinduzi wa utowaji wa elimu ya kura ya maoni itakayofanyika Julai 31 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema amewalika viongozi hao kutokana na mchango wao usiosahaulika katika historia ya Zanziar juu ya maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa amesema ingawa tarehe rasmi ya uzinduzi huo haijatolewa, lakini viongozi hao watatoa mchango mkubwa wa kuwaelimisha wananchi ili kushiriki katika kura ya maoni itakayotoa ridhaa ya mfumo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Hata hivyo Mwinyichande amesema katika kura hiyo hakutakuwa na kampeni kwa vile hakuna pande zinazopingana
Kura maoni itafanyika Zanziar Julai 31 kwa mara ya kwanza tokea mapinduzi ya 1964 inatokana na maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa Novemba 5 kati rais Karume na katibu mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad.
16

Tuesday, May 11, 2010

C U F

Chama Cha Wananchi CUF kimesema pamoja na kumalizika kwa daftari la kudumu la wapiga kura kiasi cha wananchi elfu 16 wenye haki na sifa za kuandikishwa hawakuandikishwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho Juma Said Sanani alipokuwa akizungumza na Zenji Fm Radio huko Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Amesema wananchi wengi ambao wamekosa kuandikishwa kutokana na sababu za kutokuwa na vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi na wengine kukosa vyeti vya kuzaliwa pamoja na barua za Masheha……CLIP(SANANI).
Tume ya uchaguzi Zanzibar imesema imefunga rasmi kazi za uwandikishaji wa wapiga kura na kuendelea na matayarisho ya uchaguzi baada ya kukamilika kwa kazi za uandikishaji, na ubadilishaji wa shahada za kupigia kura tume hiyo inaendelea na kazi za uhakiki wa majina ya wapiga kura waliosajiliwa katika awamu zote mbili.

JUMUIYA YA WANAO ISHI NA VIRUS VYA UKIMWI

Jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar Zapha plus imesema inakabiliwa na ongezeko la watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki na ukimwi pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao wazazi wao wanaishi na virusi vya ukimwi.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Jumuiya hiyo Salma Soud Nasibu wakati akizungumza na zenjiFm Radio huko afisini kwake Vuga mjini Zanzibar .
Amesema kutokana na ongezeko hilo Jumuiya hiyo imekuwa haina uwezo wa kuweza kuwapatia mahitaji mbali mbali ambayo wanahitaji watoto hao.
Aidha Mratibu huyo ameeleza kuwa Jumuiya hiyo pia imekuwa ikikosa uwezo wa kuweza kuwasaidia wanachama wao ambao wamepatiwa Rufaa ya Kimatibabu nje ya Zanzibar hivyo kupelekea kukosa msaada msaada kutokana na tatizo hilo.
Hivyo ameziomba Taasisi mbali mbali Jamii na Serikali kuitambua Jumuiya hiyo na kutoa misaada mbali mbali katika kuhakikisha watu wanaishi na virusi vya ukimwi wanaishi katika mazingira bora na salama

ZANZIBAR

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kuwachukulia hatua za kisheria askari polisi na madaktari wanaopoteza ushahidi wa kesi za makosa ya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto
Akizungumza katika mdahalo wa wazi wa siku ya Umoja wa Ulaya EU afisa wa wanawake na watoto wilaya ya Kaskazini ‘A” Mwajuma Kassim amesema licha ya watuhumiwa wa makosa hayo kukubali makosa yao, lakini baadhi ya watendaji wa taasisi hizo wanapoteza ushahidi kwa kile achodai maslahi yao binafsi.
Amesema hali hiyo imewafanya baadhi ya watuhumiwa kuendelea kufanya vitendo hivyo huku wakidhani wakipelekwa kwenye vyombo vya sharia huachiwa huru kwa kutokuwes na kesi ya kujibu.
Bi mwanajuma amefahamisha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hasa watoto vimeongezeka katika wilya ay Kaskazini ‘A’ hivyo ameiomba serikali kuwa makini na uposhaji wa ushahidi dhidi ya watuhumiwa.
Hata hivyo afisa huyo hakutoa takwimu halisi juu ya matukio ya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya watoto, lakini pio ameonya juu ya kushamiri kwa matukio ya kuwapa mimba wanafunzi.
Mdahalo huo wa siku moja uliofanyika katika chuo kikuu cha Zanzibar SUZA umeandaliwa kwa ushirikiano wa umoja wa Ulaya EU na chama cha wandishi wa habari wanawake TAMWA pia umehudhuriwa na balozi wa EU Tim Clark.

ARUSHA

Magavana wa benki kuu tano wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki wanakutana mjini Arusha ikiwa ni maandalizi ya nchi hizo kuwa na soko la pamoja na kuanza kutumia sarafu mpya.
Gavana wa benki kuu ya Tanzania Benerd Mbulu amesema wako katika majadiliano ya kuanisha aina ya fedha zitakazotumika katika jumuiya ya Afrika ya mashariki kuwa na sarafu moja itakayotumika kufanyia manunuzi na malipo ndani ya jumuiya hiyo.
Gavana Mbulu amesema benki kuu ya Ulaya imeombwa kufanya tathmini ambayo itaiwezasha jumuiya ya Afrika ya Mshariki kuwa na soko la pamoja.
Aidha ametaja baadhi ya hatua zilizofikiwa kuwa ni pamoja na kuoanisha baadhi ya sera za kifedha katika masuala ya riba, mfumko wa bei na masuala ya uchumi ambapo mafanikio yameshapatikana katika baadhi ya maeneo kama vile matumizi ya hundi

TUCTA

Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA Nicolas Mgaya amesema azma ya kufanyika mgomo wa wafanyakazi nchi nzima iko pale pale na kinachosubiriwa ni kutolewa kwa baraka za mgomo huo na baraza kuu la shirikisho hilo.
Amesema baada ya mazungumzo ya tarehe nane mwezi huu kati yao na serikali majibu yatapelekwa kwenye baraza kuu litalofanyika ndani ya mwezi huu ambalo litakalotoa uwamuzi wa kufanyika mgomo huo au la.
Kwa upande mwengine pamoja na tangazo la waziri wa kazi na maendeleo ya vijana Juma Kapuya alilotoa April 30 juu ya kupanda kwa kima cha chini cha mishahara katika sekta binafsi kwa asilimia 100 kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo amesema bado kuna kasoro kadhaa zinazohitaji marekebisho.

MICHEZO

Timu ya Majimaji ya Tumbe imefanikiwa kujinga na timu ya Falcon zote za Pemba kucheza ligi ya daraja la kwanza taifa msimu ujao baada ya kuichapa timu ya Azimio ya Mbuzini mabao 2-1 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kanda ya Pemba.
Mchezo huo mzuri na wa kuvutia ulifanyika katika kiwanja cha Gombani Pemba.
Shirikisho la soka duniani FIFA limethibitisha kuongezea Afrika ya kusini zaidi ya dola mia moja na 50 za Marekani katika kuiwezesha nchi hiyo kukamilisha martayarisho ya michuano ya kombe la dunia.
Pesa hizo zitasaidia kutumika kakamilisha kambi za mazoezi kwa timu 32 zitakazaoshiriki.
Ikiwa imebakia mwezi mmoja kabla ya mashindano hayo kuanza wandishi wa habari wamesema yataipatia faida nchi ya Afrika ya kusini zaidi ya dola bilioni tatu kupitia hati ya kutangaza mashindano hayo kwa mashirika ya televisheni na udhamini.
Faida hiyo imelezewa ni kubwa zaidi kuwahi ikilinganishwa na nchi za awali zilizoandaa mashindano hayo, huku ikiwa nusu ya tiketi za mashindano hayo zikiwa zimeshauzwa.

SEIF HATIB AJIBU SHUTUMA


Baadhi ya vyombo vya habari vimedai kuwa viongozi wa Jimbo la Uzini kwa kipindi cha maika mitano wamekuwa wakitoa ahadi hewa kwa wananchi wa jimbo hilo jambao ambalo limepelekea wananchama 50 wa CCM kurudisha kadi zao.
Vyombo hivyo vimeendelea kwa kudai kuwa wanachama hao wameamua kurudisha kadi hizo vikimtuhumu mbunge wa jimbo hilo Mh Mohd Seif Khatib kuwa hajatekeleza ahadi zake.
Kufuatia madai hayo Mwangaza wa Habari ulitaka kufahamu kiini cha tokeo hilo kwa kuzungumza na baadhi ya wahusika wa kadhia hiyo.
Miongoni mwa wananchi waliorudisha kadi zao ambae pia ni mkaazi wa Umbuji katika jimbo la Uzioni ni B w Hassana Abdalla umaarufu Kunguru ambae amekiri kurudisha kwa kadi yake ya uanachama ya CCM lakini amesema kuwa hawakurudisha kadi hizo kwa kumshinikizo mbunge wao na badala yake waliamua kuishinimiza Serikali kuu kwa vile ilitoa ahadi.
Aidha Bw Hassan amekanusha kuwa walijitoa moja kwa moja katika chama cha mapinduzi na kusema kuwa waliamua kupumzika hadi hapo ahadi itakapotekelezwa ambapo kwa sasa mambo yameshasawazishwa..bonyeza HAPA kumsikia Bw.. Hassan Abdalla ....Miongoni mwa wakaazi wa Umbuji waliorejesha kadi
Baada ya kumsikia mkaazi huyo tulimtafuta Mwenyekiti wakamati ya wazee wa Umbuji, Mzee Kassim Mohd Haji ambae nae alikanusha taarifa hizo na kusema yafuatayo...Clip.... Kassim Mohd Haji....Mwenyekit wa wazee wa Umbuji
Mwangaza hakuishia hapo bali pia ulizungumza na katibu wa CMM Jimbo la Uzini Bw Mzee Rajab Vuai ambae amekanusha vikali madai hayo ya vyombo vya habari kuwa jimbo hilo kwa muda mrefu halina maendeleo yoyote chini ya mbunge na mwakilishi wa sasa.
Bw Rajab amesema kuwa wanachama hao hawakujitoa kabisa ndani ya CCM na baadhi yao kazi zao zilirudishwa na watoto wao..Bonyeza HAPA kumsikia.. Katibu wa CCM jimbo la Uzini
Baada ya kumsikia katibu wa CCM jimbo la Uzini kuhuisiana na kadhia hiyo, tulimgeukia Mwenyekiti wa CCM wilaya ya kati Bw Hassan Shaaban atuthibitishie taarifa za wanachama hao kurudisha kazi zao ambapo alilithibitisha hilo na kusema kuwa sababu kubwa ya wananchi hao ni kushindwa kutekelezwa kwa ahadi ya rais ya kuwajengea barabara ya lami..Bonyeza HAPA kumsikia Mwenyekiti wa CCM wilaya ya kati
Tulikata mzizi wa fitina kwa yote tuliyasikia kwa kumtafuta Mbunge wa jimbo la Uzini ambae pia ni waziri wan chi ofisi ya makamo wa Rais Muungano Mh Mohd Seif Khatib ambae anatoa ufafanuzi juu ya kile kilichodaiwa na baadhi ya vyombo hivyo vya habari..Bonyeza HAPA kumsikia Mh Mohd Seif Khatib...Majibu ya kutojenga bara bara

Monday, May 10, 2010

MAKAMO WA RAIS WA TANZANIA DR. ALI MOHAMMED SHEIN AMESEMA


Makamo wa rais wa Tanzania Dr. Ali Mohammed Shein amesema serikali itaendelea na juhudi zake za kuhakikisha haki za wanawake na watoto zinalindwa na kukomesha vitendo vya udhalilishaji dhidi yao.
Dr. Shein ametoa kauli hiyo mjini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 20 ya chama cha wanasheria wanawake katika kipindi hichi ambacjho kimekuwa na vitendo vingi vibaya dhidi ya wanawake.
Makamo wa rais amewataka wadau mbali mbali kutetea haki za wanawake na watoto na huku serikali ikiendelea kukomesha vitendo vyote vya unyasaji dhidi yao

MAMA SALMA KIKWETE


Mwenyekiti wa Mfuko wa taasisi ya wanawake na maendeleo WAMA Mama Salma Kikwete ameitaka jamii kupanga mikakati ya kukabiliana na na matatizo wanayokabili wanafunzi wa kike ikiwemo mimba za umri mdogo.
Amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi alipofanya ziara maalum ya kuangalia maendeleo ya wanafunzi wa kike na kuwahimiza umuhimu wa elimu katika skuli ya sekondari ya Benbella mjini Zanzibar.
Amesema wanafunzi wengi wanakabiliwa na changamoto za ndoa za umri mdogogo, ubakaji na tatizo la umasikini katika familia.
Amesema matatizo hayo yamekuwa yakisababisha kurudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi wa kike katika kujikomboa kielimu…
Mama Salma pia amewataka wanafunzi wa kike kujitokeza zaidi na kukabiliana na ushindani wa kimasomo hasa katika masomo ya sayansi kwani taifa linahitaji wataalamu wazuri.
Nae mwalimu mkuu waskuli ya sekondari BenBela Asia Iddi amesema skuli hiyo ina idadi kubwa ya wanafunzi ikilinganishwa na uchache wa madarasa ya kusomea na walimu.

KUJIANDIKISHA SASA BASI

Tume ya uchaguzi Zanzibar imesema imefunga rasmi kazi za uwandikishaji wa wapiga kura na kuendelea na matayarisho ya uchaguzi.
Taarifa ya tume hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema baada ya kukamilika kwa kazi za uandikishaji, na ubadilishaji wa shahada za kupigia kura tume hiyo inaendelea na kazi za uhakiki wa majina ya wapiga kura waliosajiliwa katika awamu zote mbili.
Taarifa hiyo imesema kazi hizo zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha wapiga kura kwa siku saba ambapo wananchi watapata nafasi ya kuangalia majina yao pamoja na kutoa pingamizi kwa watu wanaowatilia mashaka.
Tume ya uchaguzi Zanzibar imesema baada ya kukamizika na pingamizi zote kushughulikiwa kisheria kutafanyika uchapishaji wa shahada za kupigia kura na kuwataka wananchi kuzihifadhi risiti zao ili kupatiwa shahada hizo.
Uchaguzi mkuu wa Zanzibar utakao wachaguwa madiwani, wawakilishi na rais wa Zanzibar unatarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu.

Sunday, May 9, 2010

HATIMAE PEMBA IMEANZA KUTUMIA UMEME WA TANGA



Huduma ya umeme mpya wa grid ya taifa kutoka Tanga hadi Pemba umewashwa leo kwa majaribio kiswani humo na kwa mafanio mafaniko .
Akizungumza katika zoezi hilo Naibu waziri wa maji ujenzi nishati na ardhi Tafana Kassim Mzee amesema umeme huo kisiwani Pemba umeanza kuwashwa majira ya saa tano Asubuhi.
Bw.Mzee amesema majaribio hayo yatachukua muda wa wiki mbili na umeme huo unatarajiwa kuwashwa rasmi Tarehe 2 June ambapo rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa bara za la mapainduzi Dr.Amani Abeid Karume anatarajiwa kuuzindua rasmi huduma hiyo…
Akizungumza na zenji Fm Radio Miongoni mwa mafundi waliokuwa wakifanikisha kazi hiyo kutoka shirika la umeme Tanzania Tanesco amesema umeme huo ulitarajiwa kuwashwa saa 12 Asubuhi na umechelewa kutokana na kutokea hitilafu katika baadhi ya viungo vya waya wa umeme huo……
Kisiwa cha Pemba kwa muda mrefu hakina huduma ya umeme wa uhakika kutokana na vinu vya kuzalisha umeme kuwa vibovu.
Kuwepo kwa huduma hiyo ya grid ya taifa kutoka Tanga kutachochea maendeleo ya kisiwa hicho hasa katika uwekezaji wa sekta ya utalii na kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa wanachi wake

MAALIM SEIF ATANGAZA NIA YAKE YA KUGOMBEA TENA URAIS


Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Seif Sharif Hamad ametangaza nia yake ya kugombea tena nafasi ya urais wa Zanzibar kwa mara ya nne katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu.
Hatua hiyo ya Hamad kutangaza kugombea nafasi hiyo imekuja siku moja baada ya mwenyekiti wa chama hicho taifa Profisa Ibrahim Harouna Lipumba kutangaza kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho.
Katibu mkuu huyo ameweka bayana nia yake hiyo ya kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar ikiwa imebakia miezi mitano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar
Uchaguzi mkuu wa Zanzibar utakao wachaguwa madiwani, wawakilishi na rais wa Zanzibar unatarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu.

Friday, May 7, 2010

MVUA YA JANA NI BALAAA


Mvua kubwa zilizonyesha nchini jana zimesababaisha maafa makubwa kwa wakaazi wa mjini na vijijini,miongoni mwa sehemu zilizoathirka na mvua hizo ni pamoja na kijiji cha Mchangani ambapo iliripotiwa kuwa baadhi ya nyumba zilijaa maji na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Kufuatia hali hiyo Mwangaza wa Habari ulimtafuta Waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi ambapo ofisi yake ndio inayosimamia kitengo cha maafa nchini ambapo amewataka masheha kuripoti kwa wakuu wa wilaya na kamati zao ili wananchi waweze kusaidiwa Bonyeza HAPA kumsikia Mh warizi

C U F USHINDI NI LAZIMA


Chama cha wananchi CUF kimesema kuwa kinamatumaini ya kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.Akizungumza na Mwangaza wa Habari Mkurugenzi Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Salum Bimani amesema kuwa kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na muafaka uliofikiwa hivi karibuni wana matumaini makubwa ya kupata ushindi.
Kwa upande wa uchaguzi mkuu Bw Bimani amesema kuwa kesho baraza kuu la uongozi la chama hicho litakutana kesho kupanga ratiba ya uchaguzi mkuu pamoja na kuanza mchakato wa kura za maoni ya chama ndani ya chama pamoja kupitia kalenda ya uchukuaji wa fomu kwa wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi.

CHADEMA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHDEMA kimesema kuwa kilitarajia kufanya maandamano makubwa ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Dar es Salaam, leo lakini maandamano hayo yamezuiwa na Polisi kutokana mkutano mkuu unaendelea jijini Dar e es salaam unaowahusisha viongozi wa kuu wan chi mbali mbali.
Akizungumza na Mwangaza wa Habari Mkurugenzi wa mambo ya nje wa chama hicho Mwenyekiti wa Mkoa wa kichama wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es salaam na John Mnyika amesema kuwa lengo la maandamano hayo ni kuunga mkono madai ya TUCTA ambayo wiki iliyopita rais Kikete alipinga madai yao na kusema kuwa mgomo waliokuwa wameuandaa ni batili.
Mnyika alizana kwa kuthibitisha maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na wzee hao.Bonyeza hapa kumsikia . John Mnyika.

Thursday, May 6, 2010

MVUA ZALETA MAAFA ZANZIBAR LEO



Mvua kubwa zilizonyesha kuanzia jana asubuhi zimeleta maafa ambapo baadhi ya maeneo watu wamelazimika kuzihama nyumba zao kutokana na kujaa maji.
Taarifa kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja zinasema baadhi ya familia wamelazimika kuzihama nyumba zao na kupata hifadhi kwa majirani kutokana na mvua hizo.
Mwandishi wetu katika mkoa wa kaskazini Unguja amesema zaidi ya nyumba nane katika kijiji cha Nungwi zimeingia maji na huko kijiji cha Kitope zaidi ya nyumba 25 zimejaa maji na nyingine kubomoka.
Hata hivyo hakuna taarifa zozote za kifo zilizotolewa kutokana na maafa ya mvua hizo.
Hapa wilaya ya mjini maeneo kadhaa yameripotiwa kujaa maji ni pamoja na Jangombe, Kwahani na Sebleni
Na huko Mchangani wilaya ya Kati mvua hizo zimeripotiwa kuleta uharibifu wa nyumba kubomoka na nyingine kujaa maji.
Akizungumza na Zenji Fm Radio diwani wa wadi ya Mchangani Mohammed Othman amesema nyumba 21 zimejaa maji katika kitongoji cha Machangani Mkiwa Bonyeza HAPA kusikia nini kimetokea

KUNA TAARIFA ZA UMEME KUTOKA TANGA KWENDA PEMBA HUENDA UKAFANYIWA MAJARIBIO HAPO KESHO.


Kuna taarifa za umeme kutoka Tanga kwenda Pemba huenda ukafanyiwa majaribio hapo kesho.
Kwa Mujibu wa taarifa zilizopatikana Kisiwani Pemba, zinadai kuwa Umeme wa kutokaTanga utafanyiwa majaribio hapo kesho, baada ya kuwepo kwa ahadi ya umeme huo kuwa tayari mwishoni mwa mwezi April.
Baada ya kupata taarifa hizo za awali ,Mwangaza wa habari kama kawaida ulimtafuta Meneja wa Shirika la Umeme Pemba Salum Masoud ili kupata taarifa za uhakika juu ya majaribio hayo.Bonyeza hapa kumsikia Meneja wa Shirika la Umeme Pemba.....Salum Masoud

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR

Tume ya Uchaguzi Zanzibar –ZEC yasisitiza hairudii Zoezi la Uandikishaji
Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC, imesema hairudiii zoezi la uandikishaji bali inawashughulikia kwa kuwabadilishia shahada wale waliojiorodhesha kwa wakati ule wa awamu ya kwanza na wakiwa katika mchakato wa kupata Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.
Akizungumza na Mwangaza wa habari,afisa habari wa Tume ya uchaguzi Zanzibar , Maalim Idrisa Haji Jecha amesema ni baada ya kutokea malalamiko kwa baadhi ya vyama vya Siasa hususan kisiwani Pemba. Bonyeza HAPA kusikia

MKUTANO WA UCHUMI WA DUNIA,UTAWEZA KUFANIKIWA KUINUA UCHUMI WA AFRIKA IWAPO UTAANGALIA UWEZO WA MFUMO WA UZALISHAJI


Mkutano wa Uchumi wa Dunia,utaweza kufanikiwa kuinua uchumi wa Afrika iwapo utaangalia uwezo wa mfumo wa Uzalishaji
Ikiwa katika siku yake ya pili ya Mkutano wa Uchumi Duniani (WEF), ambao unawakutanisha washiriki kutoka nchi 85 duniani ,ukijadili namna ya kunyanyua uchumi wa Bara la Afrika hasa baada ya kukumbwa na msukosuko mwaka mmoja uliopita.
Wasomi hapa nchini wana maoni gani juu ya mkutano huo na ni kweli unaweza kufanikiwa katika kunyanyua Uchumi barani Afrika.
Mwangaza wa habari umemtafuta Daktari wa mambo ya uchumi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk.Kasoga ,ambapo yeye amesema Mkutano huo unaweza kufanikiwa iwapo wataangalia uwezo wa mfumo wa kuzalisha uchumi wa Afrika
Hata hivyo, Mkutano huo unakusudia kutoa changamoto na mapendekezo ya njia sahihi ya kupambana na kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria ambao unadaiwa kuwa ni namba moja kwa kusababisha vifo vya kina mama waja wazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano duniani.

HOSPITALI YA CHAKECHAKE WALIA NA UKOSEFU WA DAMU UNAOPELEKEA KUKWAMISHA UPASUAJI


Hospitali ya ChakeChake walia na Ukosefu wa damu unaopelekea kukwamisha Upasuaji
Kufuatia kuwepo kwa taarifa za Wodi ya watoto ya Hospitali ya Chakechake kutokuwa na huduma za matibabu ikiwemo dawa na mashuka ,daktari wa zamu nyakati za usiku pamoja na damu ya akiba ambayo inakwamisha upasuaji mkubwa.

Jitihada za Mwangaza wa habari kuweza kupata taarifa za kina kuhusiana na matatizo yanayoikabili hospitali hiyo, tulimtafuta katibu wa Hospitali ya Chake Chake Abushiri Masoud na alipoulizwa juu ya tatizo hilo.Bonyeza Hapa kumsikia
Katibu wa Hospitali ya Chake Chake Abushiri Daudi
Mwangaza wa habari haukuishia hapo ulimtafuta Daktari wa upasuaji wa Hospitali hiyo ya Chakechake Dk.Shaaban Issa Mohamed, kutokana na madai kuwa hospiatli hiyo inakabiliwa na tatizo la uapasuaji kutokana na ukosefu wa akiba ya damu.
Dk.Shaaban amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la ukosefu wa damu katika Hospitali hiyo ,ambapo hulazimu kwenda mpaka Wete ambapo pia hukosa huduma hiyo ya damu.Bonyeza hapa kumsiia
Dk.Shaaban Issa Mohamed
Baada ya kubainika kwa tatizo hilo la ukosefu wa damu huko Pemba,Mwangaza umezungumza na Afisa uhamasishaji Mpango wa Taifa wa Damu salama Zanzibar Omari Said Omar ili kujua kama kitengo chao kinafahamu kuhusiana na tatizo hilo ambalo linaendelea huko Pemba la upungufu wa damu hususan katika hospitali hiyo ya ChakeChake.Bonyeza hapa kumsikia
Omari Said Omar Afisa uhamasishaji Damu

Tuesday, May 4, 2010

ETI KWELI MAKADA WA CCM HAWAUNGI MKONO SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA?


Baada ya maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa kati ya rais Kaume na Maalim Seif Sharif Hamad kumekuwa na tetesi kuwa makada wengi wa CCM hawaungi mkono serikali ya umoja wa kitaifa,jee suala hili niu kweli au sio kweli?
Nyota matukio ilipata nafasi ya kuzungumza na spika mstaafu wa bunge la Afrika mashariki na mjumbe wa kamati kuu ambae pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM Abdulrahman Kinana ambae amesema kuwa CCM inaunga mkono mardhina yenye lengo la kujenga umoja,mshikamano na undugu miongoni mwa wazanzibar.
Katika mahojiano na Nyota matukio Bw Kinana alianza kwa kuzungumzia juu ya mtazamo wa chama chake cha CCM juu suala la muafaka ,anasemaje Bonyeza HAPA kumsikia Abdulrahman Kinana..Akizungumzia .Serikali ya umoja wa kitaifa Zanziba

KWANINI TANZANIA IMECHELEWA KUANZISHA VYUO VIKUU?


Imeelezwa kuwa sababu za Tanzania kuchelewa kuanzisha vyuo vikuu ni ubeberu wa kikoloni ambao ulikuwa hauwapendelei waafrika na maendeleo yao.
Akizungumza na Nyota Matukio Mwenyekita wa MISA TANZANIA ambae pia ni mhadhiri katika shule ya Habari na mawasiliano ya Umma (SJMC) Bw Ayoub Rioba amesema kuwa sababu hizo ndizo zilizopelekea kuchelewa kuanzishwa kwa vyuo vikuu vinavyotoa shahada za uandishi wa habari.
Rioba amesema kuwa kutokana na kuanzishwa kwa vyuo vikuu nchini vinavyotoa shahada kwa waandishi wa habari kumepelekea baadhi ya matatizo kuondoka kwa mujibu wa tafiti ziliofanywa zinazoonesha kuwa uandishi wa habari unazidi kuboreka.
Aidha Bw Rioba ametoa changamoto kwa waandishi wa habari kuweka maslahi ya taifa mbele.Katika mahojiano yake na Zenj fm Rioba alianza kwa kueleza sababu zilizopelekea kuchelewa kuanzishwa vyuo vikuu vya habari nchini vinavyotoa shahada kwa waandishi wa habari.. Bonyeza HAPA kusikiliza

KISIWA CHA PEMBA

Baada ya Sakata la Mwakilishi wa jimbo la Tumbe Mh Ali Mohd Bakar aliyedaiwa kumpiga ngumi muuza samaki hivi karibuni kuingia katika hali nyingine ambayo inaonekana kuwastaajabisha wengi, hatimae mwakilishi huyo ameibuka na kudai kuwa vyombo vya habari havikumfanyia haki kwa kutangaza habari hizo pasi na kuulizwa.
Hata hivyo Nyota matukio ilipomthibitishia kuwa ilimtafuta kwa juhudi zake zote kuweza kujua kwa upande wake suala hili likoje aligeuka na kumtupia lawama mwandishi wetu aliyetoa taarifa hizi kwa mara ya kwanza kupitia Zenj fm Radio.
Aidha mwakilishi huyo pia alidai kuwa hakumshambulia mchuuzi wa samaki Said Kombo kama ilivyodaiwa hapo awali na badala yake ni yeye ndie aliyeshambuliwa na aliweka taarifa katika kituo cha polisi cha Chake chake na Bw alikwenda katika kituo cha polisi cha Wete wakati yeye alikuwa tayari ameshatkiwa. Bonyeza hapa kusikia Tukio Hilo

TUCTA HATIMAE IMESITISHA MGOMO WA WAFANYAKAZI


Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA limisitisha mgomo wa wafanyakazi wa nchi nzima uliokuwa uanze leo baada ya serikali kusema mgomo huo sio halali.
Akizungumza na Zenji Fm radio mwenyekiti wa TUCTA Omar Ayoub amesema wameamuwa kusitisha mgomo huo kwa madai ya kuwepo mazingira ya hatari endapo wafanyakazi watagoma
Aidha mwenyekiti huyo amewataka wafanyakazi wote nchini kuwa na subira huku wakisubiri matokeo ya mkutano utakaofanyika kati ya TUCTA na serikali tarehe nane mwezi huu ambao unaweza kuleta matokeo mazuri Shirikisho hilo lilitaka kuitisha mgomo wa wafanyakazi wa nchi nzima kudai nyongeza za misharaha ya kima cha chini kufikia zaidi ya shilingi laki tatu, kupunguza kodi wanazokatwa wafanyakazi katika mishahara yao na kuitaka serika ihakikishe mifuko ya hifadhi ya jamii inatoa mfao mazuri.

KESI YA MAUWAJI YA RAIA WA CHINA IMEENDELEA TENA


Mtuhumiwa mmoja wa kesi ya mauwaji ya raia wa china Hwang Hong Xing yaliyotokea Septemba 2006 huko Mazizini amefutiwa dhamana yake baada ya kutohudhuria mahakamani wakati kesi hiyo ikiendelea.
Akitoa uamuzi huo Jaji Abraham Mwampashi wa mahkama kuu Vuga Mjini Zanzibar amemtaja Mtuhumiwa huyo ni Bimkubwa Said Bakar amevunja masharti ya dhamana aliyopewa na mahkama hiyo.
Amesema dhamana hiyo imefutwa baada ya mtuhumiwa huyo kutohudhuria mahakamani kwa siku alizopangiwa na kutotoka nje ya Zanzibar.
Washtakiwa wengine waliopewa dhama na kulipa milioni tano kila mmoja, waraka wa mali isiyohamishika na wadhamini watatu ambao ni Hassan Abdalla mkaazi wa Michenzani na Khamisi Ali Abdalla.
Shahidi anaechunguza silaha kutoka makao makuu ya upelelezi Dar er Salaam Godfredi Luhamba akitoa ushahidi wake mahakamani hapo amesema silaha aliopelekewa kuichunguza aina ya SMG imeshawahii kutumika katika tukio jingine kabla la mauwaji hayo ya raia wa kichina.
Watuhumiwa wengine walirudirudishwa rumande hadi Mey 30 mwaka huu kesi hiyo itakaposikilizwa tena ni Abdulkadir Moh’d Saidi, Miraji Moh’d ,Salum Abdalla na Faki Ali.

WANAFUNZI NDIO WANAO ATHIRIKA NA KICHOCHO


Kitengo cha kichocho, minyoo na Matendo kimesema tatizo la kichocho limekuwa likiathiri zaidi wanfunzi kutokana na baadhi ya skuli kutokuwa na huduma ya vyoo.Hayo yameelezwa na Meneja a kitengo hicho Khalfani Abdallah Mohammed wakati akizungumza na zenji Fm radio huko afisni kwake Mianzini Lumumba mjini Zanzibar.Amesema Kutokana na hali hiyo kitengo hicho kwa kushirikiana na wizara ya elimu na kitengo cha mazingira itafanya tathmini juu ya tatizo hilo pamoja na kutoa dawa za ugonjwa huo…Amefahamisha kuwa maradhi ya kichocho yamekuwa yakikabili wiliya zote za Pemba na Mkoa wa kaskazini Unguja,Wilaya ya kati na Wilaya ya Magharib na baadhi ya maeneo ya wilaya ya mjini…Hivyo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawakataza watoto wao kutochezea maji machafu ambayo yanaweza kusababisha maradhi hayo.

VIWANJA VYALETA UTATA

Mzozo wa upimaji wa viwanja katika shehia ya Pwani mchangani umeibuka tena baada ya wananchi wa shehia hiyo kuja juu na kusema hawakushirikishwa na kutoridhika na upimaji huo.
Wakizungumza na mwandishi wetu katika kijiji hicho wamesema hali hiyo inaashiria kuwepo nia ya kutaka kunyanganywa viwanja vyao bila ya wao kushirikishwa.
Wamesema katika upimaji huo kumefanyika ujanja ili kunyimwa haki zao na kuitaka serikali kuu kuingilia kati juu ya mzozo huo
Migogoro ya ardhi imekuwa ikiibuka mara kwa mara hasa katika maeneo ya ukanda wa utalii kutokana na maeneo ya ardhi katika sehemu hizo kuuzwa kwa bei kubwa kwa watu wanaokeza katika maeneo hayo.

Sunday, May 2, 2010

HAI HAI KWA WAGOMBEA KITI CHA URAIS ZANZIBAR ZAANZA

Wakati tume ya uchaguzi Zanzibar ikitangaza uchukuwaji wa fomu za kuwania kiti cha urais wa Zanzibar kuanza tarehe 10 hadi 30 Agosti baadhi ya wananchi wamejaa hamu ya kutaka kujua jina la mgombea atakae mrithi rais Karume anaemalizia muda wake.

Wanaotajwa kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM ni waziri kiongozi wa zamani Dr.Mohammed Gharib Bilal aliejitokeza kuwania kiti hicho mwaka 2000 na 2005.

Wengine wanaotajwa kutaka kuwania kiti hicho ni waziri kiongozi wa sasa Shamsi Vuai Nahodha, makamo wa rais Dr. Ali Mohammed Shein, waziri wa elimu Haroun Ali Suleiman na waziri anaeshughulikia masuala ya muungano Mohammed Seif Khatib.

Balozi wa Tanzania nchini Itali Ali Karume kaka yake rais wa sasa wa Zanzibar tayari ameshajitokeza kutaka kuwania kiti hicho na mwengine anaetajwa ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Afrika ya Kusini Profesa Makame Mbarawa Mnyaa.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema rais atakaefaa kuiongoza Zanzibar ni yule atakayewaunganisha wazanzibari, kuondosha tofauti za kisiasa zilizoathiri shughuli za maendeleo za visiwa vya Unguja na Pemba.

Akizungumza katika mkutano wa makada wa CCM wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu Tanzania jana makamo mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar rais Amani Abeid Karume amewataka wananchi kuwakataa viongozi wanaowashawishi kukataa serikali ya umoja wa kitaifa kupitia kura ya maoni.

Tume ya uchaguzi Zanzibar imetangaza uchaguzi mkuu wa rais, wawakilishi na madiwani utafanyika tarehe 31 Octoba na kampeni rasmi za chaguzi hizo zitaanza terehe 10 hadi 30 Septemba na matokeo ya uchaguzi yatangazwa tarehe 31 hadi tarehe pili Novemba 2010.

BARA LA AFRICA LINAHITAJI TEKNOLOJIA ILI KUPIGA HATUA ZA MAENDELEO-KIKWETE


Rais Jakaya Kikwete amesema bara la Afrika linahitaji teknolojia ya kisasa kutoka nchi zinazoendelea kama vile Japan ili kuondoa tofauti kubwa kati ya nchi za Afrika na nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo.

Rais Kiwete amesema hayo mjini Arusha wakati akifungua mkutano wa siku mbili unaowahusisha wafanyabiashara na mawaziri wa biashara kutoka Afrika

Amesema kama Afrika haitasaidia kiteknolojia kuna hatari kwa nchi nyingi kutofikia malengo ya millenium kufikia mwaka 2015.

Malengo ya mkutano huo ni kufuatilia utekelezaji wa mkutano wa nne wa wakuu wa nchi za Afrika na Japan uliozinduliwa mwaka 1993 nchini Japan.

Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa na makundi ya biashara kutoka nchi mbali mbali za Afrika na wawakilishi kutoka Japan

CHADEMA KUTUMIA BILIONI TANO KAMPENZI ZA UCHAGUZI MKUU 2010


Katibu mkuu wa chama cha maendeleo na Demokrasia CHADEMA Dr. Wilbord Slaa amesema chama hicho kinatarajia kutumia shilingi bilioni tano katika kampeni zake za uchaguzi mkuu utakaofanyika Octomba mwaka huu

Dr. Slaa amesema hayo alipokuwa akitangaza maamuzi ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kwa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.

Amesema kamati hiyo imepokea makadirio ya bajeti kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuelekeza sekritarieti ya chama hicho kuendelea kuipitia kwa kufuatilia vyanzo vya mapato.

WAJIRI ZANZIBAR WASEMA VIJANA WENYE TAALUMA ZA KUJIRIWA NI KIDOGO

Chama cha waajiri Zanzibar ZANEMA kimesema kinakabiliwa na mtihani katika kuwachagua vijana wa kuwajiri kutokana na taaluma zao kuwa ndogo.

Mkurugenzi wa ZANEMA Salah Salim Salah amesema ili kuondokana tatizo hilo ameiomba serikali kuchukua juhudi za kuwaendeleza vijana kitaaluma ili waweze kuajirika hasa katika sekta binafsi.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani amesema wakati huu wa ushindani wa mitaji katika uwekezaji, taasisi binafsi zinahitaji wafanyakazi wenye ujuzi na uwezo, hivyo haitakuwa rahisi kuajiriwa vijana wasiokuwa na uwezo.

Amesema suala la kuwaendeleza vijana kitaaluma ili waingie katika soko la ajira linahitaji kufanywa kuwa agenda ya kitaifa.

Aidha mkurugenzi huyo wa ZANEMA ametoa wito kwa serikali kuzifanyia marekebisho sheria za kazi zinazokwenda kinyume na mikataba ya kimataifa ili kutoa fursa kwa watu wenye ulemavu kupata ajira.

Nae katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar ZATUC Khamis Mwinyi Mohammed ameutaka mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF kutoa mafao yote kwa wananchama wake kama yalivyoainishwa katika sheria ya kuanzisha mfuko huo.

Mfuko wa wa ZSSF ambao unaendelea kutoa mafao ya uzeeni kwa wananchama wake wanaostaafu kazi, lakini bado haujanza kutoa mafao ya uzazi na ugonjwa.

KARUME ASEMA SERA YA KUONGEZA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI ITAKUWA TAYARI JUNE MWAKA HUU 2010


Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amesema serikali inaendelea kutayarisha sera ya utumishi wa umma itakayowezesha kupandisha mishahara ya wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi kulingana na hali ya maisha.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani huko hoteli ya Bwawani amesema utayarishaji wa sera hiyo ni miongoni mwa mageuzi ya mfumo wa utumishi wa umma unaofanywa na serikali kwa kushirikiana na shirika la kazi duniani ILO.

Amesema mfumo huo wa utumishi wa umma utakaozingatia maslahi ya watumishi wa taasisi za serikali na sekta binafsi pia utahusisha upandishaji wa pencheni kwa wastaafu utakamilika June mwaka huu.

Dr. Karume amesema serikali inaendelea kutatua matatizo ya wafanyakazi na kusema sehemu kubwa ya matatizo hayo yameshapatiwa ufumbuzi ikiwemo ulipaji wa mishahara kwa wakati na mafao ya wafanyakazi wanaostaafu…

Aidha rais Karume amewataka vijana na wafanyabiashara kuzitumia fursa za soko la pamoja la nchi wananchama wa jumuiya ya Afrika kamshariki E.A.C ili kuendelesha shughuli za biashara na kutafuta ajira.

Amesema wizara ya kazi imeshaweka kitengo cha kuwandaa vijana kuingia katika soko hilo na kuzitaka taasisi nyingine kujenga mazingira yatakayowawezesha wazanzibari kulitumia soko hilo.

Katika maadhimisho hayo Dr. Karume alipokea maandamano ya wafanyakazi na kuwazawadia wafanyakazi bora 76 fedha taslimu na vyeti.

Siku ya wafanyakazi duniani inadhimishwa Mei Mosi ya kila mwaka duniani kote ili kuwakumbuka zaidi ya wafanyakazi mia moja na 20 waliouwawa mwaka 1889 katika jimbo la Chicago nchini Marekani walioandamana kudai haki zao.

ABIRIA WAZILALAMIKIA MELI ZA ABIRI ZANZIBAR

Vyombo vya usafiri wa majini vya abiria vinavyofanya safari kati ya Dar es salaam na Zanzibar vimelalamikiwa na wananchi wa Zanzibar kutokana na tabia ya kujaza abiria kupita kiasi na kutishia usalama wa abiria.

Akizungumza na Zenj Fm radio juu ya malalamiko hayo mrajisi wa meli Zanzibar Abdalah Mohamed amesema meli zinazofanya safari kati ya Dar es salaam na Zanzibar zimekuwa zikikaguliwa mara kwa mara.

Amesema meli hizo zinapokuja Zanzibar kabla ya kusajiliwa ni lazima ikaguliwe na kufuata taratibu zote za huduma za usafiri wa baharini ili zipewe kibal.

Akizungumzia suala la uzidishaji wa abiria ambalo linaonekana kutokea mara kwa mara amesema meli kikawaida inaweza kuzidisha abiria kutokana na sababu maalum ikiwemo wakati wa sherehe.

Hivi karibuni meli ya Flying Hourse iliripotiwa kuzidisha abiria ikiwa katika bandari ya Malindi ambapo abiria waliokuwa katika meli hiyo walipata hofu na hivyo kulazimika kurudi tena bandari wakati nahodha wa meli ya Sea Bus alipandishwa mahakamani kwa kosa kama hilo.

MKUU WA WILAYA YA WATE AGIZA KUFUKUZWA KAZI WAFANYAKAZI WAWILI WA HOSPITALI YA WETE BAADA YA KUTOA MANENO MACHAFU KWA MAMA MJAMZITO


Mkuu wa wilaya ya Wete Omar Khamis Suleiman ameagiza kusimamishwa kazi wafanyakazi wawili wa hospitali ya Wete baada ya kumtolea lugha chafu mama mjawazito aliekwenda kujifungua katika hospitali hiyo.

Hatua ya kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi hao imekuja baada ya mama mjamzito huyo ambae ni mke wa mkuu wa wilaya hiyo kutolewa lugha chafu na wafanyakazi hao wakati alipokwenda kujifunugua.

Akizungumza na mwandishi wetu kisiwani Pemba Bw. Suleiman amesema wafanyakazi wa hospitali hiyo wanaowapokea wagonjwa wanawatolea lugha chafu wagonjwa wakati wanapotaka kupatiwa matibabu na kuwafanya kuichukia hospitali hiyo.

Amesema lugha kama hizo sio nzuri na kusema yeye mwenyewe amezigundua na kuagiza hatua za kusimamishwa kazi zichukuliwe na uongozi wa wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Amefahamisha kuwa serikali yake itaendelea kuchukua hatua kama hizo kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo vya afya vingine hasa maeneo ya vijijini kutokana na vitendo vya aina hiyo kukithiri.

Nae katibu wa hospitali ya Wete Salim Mohammed amesema amezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwa kuwaona baadhi ya wafanyakazi wanakiuka maadili ya kazi na kusema wataendelea kuwaelimisha ili kukomesha vitendo hivyo viovu.

Tukio kama hilo limesharipotiwa kutokea katika hospitali za Pemba ambapo wagonjwa wanadai kunyanyaswa na wafanyakazi wa hospitali.

WATU 20 WAHOFIWA KUFA MAJI MTWARA


Zaidi ya watu 20 wanahofiwa kufa maji mkoani Mtwara baada ya mashua waliokuwa wakisafiria kuzama baharini.

Mashua hiyo inayokadiriwa kuwa na watu 28 imezama leo mchana karibu na pwani ya mji wa Mtwara.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo amesema hadi sasa mtu mmoja amekufa kati ya wanane waliokolewa na wengine 20 hawajulikani waliko Habari zinasema wakati waokowaji wakiendelea na shughuli za uokozi mmiliki wa mashua hiyo amekimbia pamoja na nahodha wake.