I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, May 6, 2010

MVUA ZALETA MAAFA ZANZIBAR LEOMvua kubwa zilizonyesha kuanzia jana asubuhi zimeleta maafa ambapo baadhi ya maeneo watu wamelazimika kuzihama nyumba zao kutokana na kujaa maji.
Taarifa kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja zinasema baadhi ya familia wamelazimika kuzihama nyumba zao na kupata hifadhi kwa majirani kutokana na mvua hizo.
Mwandishi wetu katika mkoa wa kaskazini Unguja amesema zaidi ya nyumba nane katika kijiji cha Nungwi zimeingia maji na huko kijiji cha Kitope zaidi ya nyumba 25 zimejaa maji na nyingine kubomoka.
Hata hivyo hakuna taarifa zozote za kifo zilizotolewa kutokana na maafa ya mvua hizo.
Hapa wilaya ya mjini maeneo kadhaa yameripotiwa kujaa maji ni pamoja na Jangombe, Kwahani na Sebleni
Na huko Mchangani wilaya ya Kati mvua hizo zimeripotiwa kuleta uharibifu wa nyumba kubomoka na nyingine kujaa maji.
Akizungumza na Zenji Fm Radio diwani wa wadi ya Mchangani Mohammed Othman amesema nyumba 21 zimejaa maji katika kitongoji cha Machangani Mkiwa Bonyeza HAPA kusikia nini kimetokea

No comments:

Post a Comment