I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, September 26, 2010

UCHAGUZI WA ZANZIBAR 2010

PROFISA LIPUMBA APATA AJALI TANGA

Msafara wa mgombea urais wa jamhuri ya muungano Tanzania kupitia chama cha wananchi CUF Profisa Ibrahim Harouna Lipumba umepata ajali leo asubuhi mkoani Tanga.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Handeni imehusisha magari mawili ya yaliokuwa katika kampeni, moja ilimbeba meneja wa kampeni na mgombea urais Profisa Lipumba na nyingine jingine limewabeba wandishi wanne wa habari.

Ajali hiyo imetokea baada ya gari hilo la mgombea kuchomoka tairi na kupoteza mwelekeo. Hata hivyo mgombea huyo na meneja wa kampeni Saidi Miraj hawakupata majeraha, lakini walikimbizwa hospitali kwa ajili ya kuangaliwa afya zao.

Gari ya waandishi wa habari wanne ilipinduka mara mbili, lakinihakuna mwandishi hata mmoja aliepata majeraha makubwa

MUASISI WA MAPINDUZI ZANZIBAR SAID ABDALLA NATEPE AMEFARIKI DUNIA

Mmoja wa viongozi 14 wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Meja Jenerali Abdallah Said Natepe amefariki dunia jana mchana katika hospitali yajeshi Lugalo mjini Dar es Salaam.

Marehemu Natepe ni miongoni mwa viongozi wa mapinduzi kumbi na mbili waliofariki dunia ambao walifanikisha kufanikiwa kwa mapinduzi ya Januari 12, 1964 yaliyoindoa serikali ya kisultani visiwa vya Zanzibar,

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, kifo hicho kimetokea jana mchana kwenye hospitali hiyo kuu ya Jeshi la Wananchi.
Taarifa hiyo inamnukuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akieleza kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha mwanamapinduzi huyo na kumtumia salamu za rambirambi katibu mkuu wa CCM akielezea jinsi alivyoguswa na kifo hicho cha Mzee Natepe.

“Kifo kimemchukua mwanamapinduzi, mzalendo na mwanachama wetu mwaminifu katika kipindi ambacho taifa na chama bado kinamhitaji sana. Kifo kimetunyang’anya tunu wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu; ni huzuni kubwa kwetu; ni majonzi makubwa na hatuna neno kubwa linaloweza kuelezea huzuni hii,” Rais Kikwete anakaririwa kwenye taarifa hiyo.

Rais alipokea taarifa za kifo cha Mzee Natepe jana mchana akiwa Njombe mkoani Iringa ambako yuko kwa ajili ya shughuli za kampeni.

Rais Kikwete pia ametuma salaamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Natepe.

“Mzee Natepe amekuwa sehemu ya maisha yangu ya kisiasa, kijamii na amenipa malezi na maelekezo mengi nikiwa kama kijana wake na amekuwa moja ya nguzo yangu kubwa katika shughuli zangu za kisiasa na kikazi katika maeneo yote niliyotumikia nchi yangu,” alisema rais na kuelezea kwa masikitiko huzuni aliyonayo na kuwahakikishia kuwa yuko nao katika kipindi hiki kigumu.

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi na Mzee Natepe na kufanya naye kazi. Tunamuomba Mungu amlaze mzee wetu mahali pema peponi na kumpa pumziko la milele, amina”

MGOMBEA WA CUF MALIM SEIF AHADI KUCHIMBA MAFUTA NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITANO

Chama cha wananchi CUF kimesema endapo kitaingia madarakani kuingoza Zanzibar suala la mafuta na gesi asilia litaondolewa kwenye orodha ya mambo ya muungano ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Mgombea urais kupitia chama hicho Malim Seif Sharif Hamad amesema suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa kwenye orodha ya mambo ya muungano halina lengo la kuvunja muungano bali ni kujali uchumi wa nchi ndogo na kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Ocean View mjini hapa amesema tayari baadhi ya makampuni yameonesha nia ya kutaka kuchimba mafuta yaliopo Zanzibar hivyo serikali yake itatakeleza suala hilo ndani ya kipindi cha miaka mitano.

DR. SHEIN AHIDI KUWARUDISHA MATAJIRI WAZALENDE KWENDA KUEKEZA PEMBA

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dr. Ali Mohammed Shein amesema serikali yake itaendelea kuimarisha miundo mbinu ya kiuchumi kisiwani Pemba ili kuwainua kiuchumi wananchi wa kisiwa hicho endapo atapata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar.

Amesema wawekezaji kutoka nje ya nchi na wale wazalengo wanaokeza nchi za kigeni wameonesha nia ya kuja kuwekeza Zanzibar hasa maeneo ya Pemba kutokana na kuwepo vivutio vya kiuchumi kama vile umeme wa uhakika, maji na miundo mbunu ya usafirishaji.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu kwa chama hicho kisiwani Pemba Dr. Shein amesema endapo wananchi watamchagua serikali yake itaandaa sera maulum za kuendeleza uchumi kisiwani Pemba kupitia ilani ya uchaguzi.

Amefahamisha kuwa usalama, amani na utulivu wa wananchi utaisaidia Zanzibar kuendeleza sekta za uwekezaji kwa kuwashajihisha wawekezaji wazalendo wanaowekeza nchi za nje pamoja na wawekezaji wageni kuja kuwekeza nchini...

Kuhusu utumishi wa umma Dr. Sheina amesema endapo ataingia madarakani serikali yake itaangalia maslahi ya wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi, nyenzo, na kuongeza na mslahi yao.

Amesema wafanyakazi ndio kiini cha mapinduzi ya Zanzibar, hivyo wanahitaji kuendelezwa kwa kupewa taaluma ya kuwatumikia wananchi kwa ufanisi badala ya kubahatisha ili kuliletea tija taifa lao.

Nae mgombea mwenza Dr. Mohammed Gharib amewataka wana CCM kisiwani Pemba kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha chama hicho kinaleta ushindi kwa wagombea wake.

Wednesday, September 15, 2010

CUF YAZINDUA ILANI YAKE YA UCHAGUZI YA MWAKA 2010 ZANZIBAR

Chama cha wananchi CUF kimesema kitaangalia upya mambo yaliongezwa katika orodha ya mambo ya muungano baada ya makubaliano ya awali ya mwaka 1964 yaliounda muungano huo endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza Zanzibar.

Mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Seif Sharif Hamad amesema mambo hayo yatajadiliwa kwa kina na uwazi ili kuhakikisha muungano huo unazifaidisha nchi zote mbili kwa msingi ya usawa.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 ya chama hicho amesema serikali yake pia itawasiliana na serikali ya muungano kutaka kuandika katiba mpya itakayokidhi makubaliano ya muungano ya mwaka 1964 yenye muundo wa serikali tatu

Kuhusu maendeleo ya uchumi Hamad amesema serikali atakayoiunda itajenga uchumi imara kwa kuzingatia mfumo wa soko huria unatoa fursa ya ushiriki wa wananchi wote ili kuona hali zao za kimaisha zinaimarika.

Amesema sekta za kilimo, utalii, biashara, viwanda na uvuvi zitapewa umuhimu katika ujenzi wa uchumi wa kisasa pamoja na kuhakikisha matumizi bora ya raslimali ziliopo ikiwemo uchimbaji wa mafuta.

Hamad amesema serikali yake itaanzisha shirika la ndege kwa njia ya ubia na wewekezaji wa ndani na nje ili kuwa na njia za uhakika za kuinganisha Zanzibar kibiashara na kiuchumi na nchi nyingine duniani.

Amesema atafanya mazungumzo na mashirika ya kimataifa ya usafiri wa anga kuanzisha usafiri wa moja kwa moja kati ya miji mikuu yao na Zanzibar ili kuimarisha shughuli kiuchumi na biashara…

Kuhusu utumishi wa umma Hamad amesema serikali yake itapandisha mishahara ili iweze kukidhi gharama za maisha na kuhakikisha inatolewa kila baada ya wiki mbili na ambapo kima cha chini kitaanzia shilingi laki moja na nusu.

Amesema licha ya serikali kuwa na wafanyakazi wengi wasiokuwa na tija serikalini, serikali yake itakuwa na mpango maalum wa mashauriano ya kutoa maamuzi baadhi ya wafanyakazi ambao hawana tija serikalini waondolewe.

Amesema wafanyakazi hao watejengewa mazingira mazuri ya kuwa na ajira mbadala ili kuweza kuzalisha au kutoa huduma zenye tija zitakazomuwezehsa kupata mapato makubwa kuliko alivyokuwa serikalini.

Friday, September 10, 2010

KATIBU MKUU WA CUF HAMAD AMSIFU RAIS KARUME KWA KUIACHA ZANZIBAR KUWA NA AMANI

Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Seif Sharif Hamad, amesifu juhudi za rais wa Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume, anaeondoka madarakani kwa kuiacha Zanzibar kuwa nchi ya amani.

Amesema busara za rais Karume katika kusimamia maridhiano ya kisiasa, zinahitaji kupongezwa kwa vile zimesababisha kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, mara baada ya uchaguzi mkuu wa Octoba 31 mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kumaliza sherehe za baraza la Edil fitr huko Forodhani, Hamad pia amesifu maendeleo ya kiuchumi yaliofikiwa na serikali ya rais Karume, katika ujenzi wa miundo mbinu ya kiuchumi na kijamii…

Kuhusu uendeshaji wa kampeni za kisiasa kwa ajili ya uchaguzi mkuu, katibu mkuu huyo amewataka viongozi wenzake wa kisiasa kuendesha kampeni za kistaarabu, ili kuenzi umoja na mshikamno wa wazanzibari uliopo.

RAIS KARUME AMEWATAKA VIONGOZI WA SIASA KUENDESHA KAMPENI ZA KISTAARABU

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume, amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu kwa kuheshimiana, umoja, amani na utulivu.

Amesema siasa sio ugomvi bali ni sehemu ya kutekeleza mahitaji ya watu, hivyo ni vyema kwa wananchi na viongozi wa siasa kuimarisha hali ya utulivu, ili kulinda maridhianoya kisiasa yalioleta umoja na mshikamano.

Akilihutubia baraza la Ediel fitr huko Forodhani, rais Karume amesema katika kipindi kilichopita cha utulivu wa kisiasa nchini, kimeleta mafanikio ya uchumi na ustawi wa jamii, kama vile ujenzi wa miradi ya miundo mbinu, elimu, afya, sekta za huduma na utalii

Hata hivyo rais Karume anaemaliza muda wake, baada ya kufanyika uchaguzi mkuu Octoba 31, amesema juhudi zaidi zinahitajika kuendeleza nyanja nyingine za maendeleo kwa faida ya kila mwananchi.

Amesema wananchi hawanabudi kujituma zaidi, ili kuona mipango ya serikali, kama vile mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini MKUZA na malengo ya Milenia inafanikiwa kwa lengo la kuinua pato la taifa.

Baraza hilo la edil fitr, linalofanyika baada ya waislamu kumaliza wamwezi mtukufu wa ramadhan, pia limehudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa na mabalozi wadogo wanaoziwakilisha nchi zao Zanzibar.

ZANZIBAR KUTARAJIWA KUKUBWA NA UKAME

Baadhi ya maeneo ya Unguja na Pemba yanatarajiwa kukumbwa na ukame utakaosababisha uhaba wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo na kilimo cha umwagiliaji maji kutokana uhaba wa mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza wiki ya pili mwezi ujao.

Taarifa ya mamlaka ya hali hewa Tanzania iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema hali hiyo inatokana na mvua za vuli kunyesha chini ya kiwango kitakacho athiri unyevunyevu wa kuotesha miti, mazao na malisho ya mifugo.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imewashauri wakulima na wafugaji kutumia maji kwa uangalifu, kuotesha mazao yanayostahamili ukame na kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo katika maeneo yao.

Akizungumza na Zenji Fm Radio juu ya taarifa hiyo inayotishia kuathiri mifugo na kilimo cha umwagiliaji maji hapa Zanzibar mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa Zanzibar Khamis Ali Suleiman amesema

Taarifa hiyo ya hali ya hewa inayoashiria uhaba wa mvua za vuli imetolewa na wataalmu wa hali ya hewa wa nchi za eneo la Pembe ya mashariki mwa Afrika waliokutana mjini Nairobi Kenya kuanzia Agost 23 hadi Septemba tatu mwaka.

HOTELI NNE ZA KITALII ZANZIBAR ZIMEWAKA MOTO

Hoteli nne za kitalii na nyumba 12 za wananchi katika kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kusini Unguja zimeteketea kwa moto leo mchana.

Katika tukio hilo hakuna mtu aliejeruhiwa, huku baadhi ya mali zilizokuwemo ndani ya hoteli hizo zimeripotiwa kuteketea kwa moto na nyingine zimewahi kutolewa na wasamaria wema.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema awali waliona moto na moshi mkubwa ukitokea katika maeneo yenye hoteli za kitalii na baadae moto huo kusambaa katika hoteli nyengine ambazo zilikuwa zikiwaka kwa kasi kubwa kutokana na upepo uliokuwa ukivuma baharini nyakti hizo.

Wamesema kikosi cha zima moto na ukozi kilichelewa kufika katika eneo la tukio, huku likiwa halina maji na kulazimika kutumia maji ya bahari lakini baadae lilikwama na kusababishwa moto huo kuchelewa kuzimwa. Hata hivyo mkuu wa Zima moto Sajenti Shukuru amesema wamemaliza kuzima moto huo na kukanusha madai kwamba gari lilikuwa halina maji na kukwama ufukweni

Kamanda wa ppoli mkoa wa kuskazini Unguja, Mselem Masoud Mtulya alithibitisha kutokea kwa moto huo na kuzitaja hoteli zilizoungua ni pamoja na Rummi ambayo imeteketea vibaya sana kwa kuwa ndio iliyoanza kuwaka na baadae moto huo kusambaa na kurukia katika hoteli iitwayo Bwagamoyo ambayo imeungua paa lote la hoteli hiyo.

Kamanda Mtulya alisema baadae moto huo ulishika katika hoteli ya Union ambayo nayo imeungua vibaya vyumba vya kulala na eneo lote la baa, ukumbi wa chakula na maduka ya vifaa na nguo za kitalii yaliokuwa ndani ya hoteli hiyo.

Aliitaja hoteli nyengine ni Diving Center ambayo nayo ilitekeleta katika eneo lake la ukumbi uitwao East Afrcan, ukumbi wa jambo brothers, sehemu ya jikoni yote imeungua na baadhi ya vyumba na kumbi zake zikiwa zimetekeleata vibaya sana.

Aidha alisema licha ya moto huo kusambaa kwa kasi lakini wageni wanane waliokuwa wamelala ndani waliwahi kuokolewa huku wengine wakiwa wamekimbia ambao wengi wao nyakati hizo walikuwa nje ya hoteli hizo na baadhi yao walikuwa wakipunga upepo na wengine walikuwa katika sehemu za kulia wakijipatia chakula.

Alisema nyumba za wananchi nazo hazikusalimika kutokana na moto huo ambapo zaidi ya nyumba 12 ambazo zipo karibu ya hoteli hizo zilizoungua zimeshika moto kutokana na moto huo kusambaa kwa kasi kutokana na upepo na kuwa zimeezekwa paa za makuti ambazo hushika moto haraka.

Kamanda Mtulya alisema chanzo cha moto huo hakijajulikana bado lakini jeshi la polisi linajitahidi kutafuta chanzo halisi cha kuzuka moto huo kabla ya kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vinavyohusika.

Hasara iliyoptaikana kutokana na moto huo bado haijajulikana. Hii ni mara ya pili kwa hoteli za kitalii kuungua moto kwa kipindi kisichozidi miezi miwili ambapo tukio la mwanzo hoteli tatu kwa pamoja ziliungua moto katika kijiji cha Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja.

Tatizo la hoteli kuungua moto limekuwa likitokea mara kwa mara visiwani Zanzibar ambapo mwezi uliopita jumla ya hoteli za kitalii na nyumba zaidi ya sita ziliteketea kwa moto katika kijiji cha Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.

Hoteli zilizoungua mwezi uliopita ni pamoja na Visitors Inn, Sau Inn na Bungalow ambapo zote zipo eneo la Jambiani ukanda wa pwani ambapo kumbi na zaidi ya vyumba 12 vya kulala wageni viliteketea kutokana na moto huo.

Monday, September 6, 2010

MWENYEKITI WA TLP AGUSTINE LYATONGA ADAI KUFANYIWA RAFU KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI

Mgombea ubunge jimbo la Vunjo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour TLP, Agustine Mrema, amenusurika kujeruhiwa na kundi la vijana aliodai wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Akizungumza na Zenji Fm radio Mrema amesema mbali ya kunusurika katika tukio hilo, gari lake liliharibiwa vibaya kwa kupigwa mawe na vioo vyote vya mbele vya gari yake vimepasuliwa.

Amesema tukio hilo, limetokea Jumamosi iliyopita katika eneo la njia panda la Himo, Moshi wakati Mrema alipokuwa akipita barabara kuu karibu na eneo ambalo mgombea ubunge wa CCM, Crispin Meela, alikuwa akifanya mkutano wa kampeni za kuomba kura

WAANGALIZI WA UCHAGUZI WAMEANZA KUSAMBAZWA KUANGALIA UCHAGUZI MKUU 2010

Kamati ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi Tanzania TEMCO imesema inashindwa kutekeleza shughuli za uangalizi wa chaguzi zinazofanyika nchini kutokana na uhaba wa fedha.

Mratibu wa TEMCO DR. Benson Banner amesema taasisi hiyo inayofanya kazi muhimu, lakini haipokei fungu lolote la fedha kutoka serikalini na badala yake hutegemea wahisani wenye masharti magumu.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari wa utowaji wa taarifa ya mwenendo wa uchaguzi mwaka 2010 mjini Zanzibar amesema hali hiyo imeifanya TEMCO kuwa na wangalizi wachache ikilinganishwa na ukubwa wa maeneo ya uchaguzi Tanzania.

Dr. Banner amesema taasisi za ndani zina uwezo mkubwa wa kuendesha shughuli za uangalizi wa chaguzi zinazofanyika nchini ikilinganishwa na taasisi za kimataifa, lakini bado haiziwezeshwi kifedha na serikali

Nae makamo mwenyekiti wa tume hiyo Maryam Abdulrahman amesema TEMCO inatarajia kutuma wangalizi wa uchaguzi elfu saba, 210 katika majimbo yote ya Tanzania bara na Zanzibar kuangalia mwenendo wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Amesema wangalizi hao wa muda mrefu na mfupi watatumwa majimboni na kwenye vituo vya kupigia kura kuangalia undeshaji wa kampeni, upigaji na kuhesabu kura, utowaji wa matokeo, malalamiko na ukataji wa rufaa ambapo taarifa zake zitatolewa ndani ya siku tano baada ya upigaji wa kura.

TEMCO ni taasisi ya ndani inayoundwa na taasisi mia moja na 52 imekuwa ikiangalia mwenendo wa uchaguzi Tanzania tokea mwaka 1995.

BIDHAA MBOVU ZIMEZAGAA ZANZIBAR

Bidhaa zilizopitwa na viwango zimeanza kuzagaa katika kipindi hichi cha kumalizia mwezi mtukufu wa ramadhani ambazo huuzwa kwa bei nafuu.

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na uingizaji wa bidhaa mbovu ulioshamiri hapa Zanzibar hasa kipindi hiki cha kukaribia siku kuu ya Edil fitr.

Hatua hiyo imekuja kufuatiwa kuwepo kwa wimbi kubwa la uingizaji wa vyakula vilivyopita na muda wa matumizi ya binadamu ambalo limezuwa malalamiko kutoka kwa wananchi

Uchunguzi uliofanywa na Zenji Fm radio leo na jana umegundua mchele mbovu aina ya Busmat wenye ujazo wa kilo tano ukiuzwa kwa shilingi elfu sita na tano katika maeneo ya Darajani mjini Zanzibar.

Mchele huo unaouzwa na wafanyabiashara za mikononi maarufu wamachinga unaonesha kutengenezwa March 2008 na kumaliza muda wa matumizi March 2011 ni mbovu na unatoa harufu mbaya unapofunguliwa.

Akizungumza na zenji Fm radio juu ya malalamiko hayo mrajisi wa bodi ya chakula, dawa na vipodozi Dr. Burhan Simai amesema bodi hiyo haina sheria ya kuwadhibiti wafanyabiashara wanaojulikana wamachinga.

Hata hivyo amesema bodi hiyo inafanya ukaguzi katika sehemu zote zinazoingizwa bidhaa Unguja na Pemba na kukagua makontena yote ya bidhaa

Hivi karibuni hiyo imekamata tani 245 za mtama na tani 193 za mchele kutoka nje ya nchi zikiwa zimeharibika na havifai kwa matumizi ya binadamu.

Kutokana na hali hio Dk Simai aliwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wanaponunu

ZANZIBAR YAJENGA MATUMAINI KUPATA UANACHAMA WA FIFA

Naibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna amesema juhudi za Zanzibar kupatiwa uwanachama wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA zimeanza kuleta matumaini baada ya kufunguliwa jalada rasmi la kuomba uanachama huo.

Shamhuna ambae pia ni waziri wa habari, utamaduni na michezo amesema rais wa FIFA Seif Blata ameahidi kulishughulikia ombi la Zanzibar la kupatiwa uwanachama wa shirikisho hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar wakati akitokea Uswiss Shamhuna amezitaja baadhi ya hoja zilizowasilishwa kuomba uanachama huo ni kuwepo nchi ndogo nandi ya FIFA ambazo hadhi zake zinazidiwa na Zanzibar, huku zikiwa sio wanachama wa umoja wa mataifa.

Mwaka 2001 Zanzibar ilishindwa kupata uwanachama wa shirikisho hilo na mwaka huu ilianda hoja nzito za kuomba uanachama huo ambazo zinamwelekeo wa kuzaa matunda.

Sunday, September 5, 2010

CHAMA CHA NLD, ZANZIBAR KUMUUNGA MKONO MGOMBEA WA URAIS ZANZIBAR KUPITIA CCM DR. ALI SHEIN

Chama cha siasa cha NLD, kimekuwa chama cha kwanza cha upinzani kutangaza kumuunga mkono mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dr. Ali Mohammed Shein katika uchaguzi mkuu ujao. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, naibu katibu mkuu wa NLD, Zanzibar Rashid Ahmme Joy amesema chama hicho kimeamuwa kumuunga mkono mgombea huyo kutokana na sera zake zenye kulenga siasa za umoja na kuweka mbele maslahi ya Zanzibar. Amesema chama hicho bado kina wasiwasi na wagombea wengine wa vyama vya kwamba hawatoweza kuendeleza siasa za umoja kwa kile alichodai kuwa na ulafi wa madaraka… “Sisi tutamuunga mkono mgombea atakaeleta mabadiliko na wagombea wa vyama vya upinzani watakapokuja hujui watafanya nini, hivyo mgombea wa CCM Dr. Shein ameonesha mwelekeo wa kufuata sera za siasa za umoja wa nchi”. Alisema Joy. Joy ambae kwa muda wa miezi kadhaa hajaonekana hadharani kutokana na kuugua shindikizo la damu amesema hali yake inaendelea vizuri na wiki mbili zijazo anatarajia kushiriki katika harakati za siasa. Hivyo amewaahidi wafuasi na wapenzi wa chama cha NLD ataendelea kuwepo katika ulingo wa kisiasa kwa lengo la kuleta mabadiliko ya mfumo wa siasa wa vyama vingi hasa Zanzibar. Chama cha NLD hakijasimamisha mgombea wa nafasi ya urais Zanzibar kutokana na Joy alietarajiwa kugombea nafasi hiyo kuugua siku chache baada ya tume ya uchaguzi Zanzibar kuanza kazi za utowaji wa fomu kwa wagombea wa nafasi hiyo kupitia vyama vya siasa. Hivi karibuni chama kingine cha upinzani cha APPT-MAENDELEO kimetangaza kumuunga mkono mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananachi CUF Seif Sharif Hamad. END

Friday, September 3, 2010

BENKI YA WATU WA ZANZIBAR KUIMARISHA HUDUMA ZAKE

Benki ya watu wa Zanzibar PBZ, inakusudia kuweka mitandao itayowawezesha wateja wake wa ndani na nje ya nchi kupata huduma za kuweka, kutoa na kupokea fedha popote walipo.

Kaimu mkurugenzi wa PBZ Bw. Ame Haji Makame amesema hayo katika hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo huko hoteli ya Zanzibar Beach Rasort nje kidogo ya Zanzibar na kuhudhuriwa na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume na wateja wengine wa PBZ.

Amesema uwekezaji huo unahusisha uwekaji wa mashine za ATM, mtandao utakaowaruhusu wateja kutoa na kuchukua fedha katika matawi yote ya PBZ na mtandao wa kimataifa wa kutuma na kupokea fedha kwa njia ya haraka kutoka nje ya Tanzania.

Amesema PBZ pia inaendelea na ujenzi wa tawi la benki kwa ajili ya wateja wakubwa katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar ambalo linatarajiwa kumalizika baada ya miezi mitatu na ujenzi wa tawi jingine mjini Dar es Salaam unaotarajiwa kumalizika mwezi Novemba.

Aidha Bw. Haji ameitaja miradi mingine itakayoiwezesha PBZ kumudu soko la ushindani ni ujenzi wa tawi la Chakechake Pemba pamoja na kujiunga na mfumo wa kutuma na kupokea fedha wa Western Union.

Amesema mfumo huo utasaidia serikali katika upokeaji wa fedha kati ya Zanzibar na nchi nyingine duniani na unatarajiwa kumalizika baada ya miezi miwili

RAIS KARUME ATEMBELEA UJENZI WA BARA BARA KISIWANI PEMBA

AIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Amani Abeid Karume ametoa pongezi kwa Idara ya Barabara Pemba pamoja na wananchi wa Mtambile,Kangani, Kengeja na Mwambe kwa kushiriki vyema katika ujenzi wa barabara zinazopita vijijini mwao.

Rais Karume alitoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara za Mtambile-Kangani na barabara ya Mtambile,Kengeja-Mwambe Kisiwani Pemba.

Katika ziara yake hiyo Rais Karume alitoa pongezi kwa wananchi wa maeneo hayo ambao wamekuwa wakishiriki kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa barabara ikiwa ni miongoni mwa barabara zilizomo kwenye Mradi wa Barara za vijijini Kusini Pemba.

Rais Karume aliwataka wananchi wa maeneo hayo kuongeza juhudi zaidi katika shughuli hiyo ya ujenzi wa brabara ambapo wananchi hupata ajira kwa kiasi kikubwa kutegemea na juhudi zao za kazi.

“Shukrani kwa msaada na mchango wenu mkubwa katika ujenzi wa barabara hivyo ongezeni juhudi na nguvu ili mpate kuendelea na ujenzi kwa ufanisi mkubwa”,alisema Rais Karume.

Akitembelea ujenzi wa barabara hizo ambazo kwa asilimia kubnwa ujenzi wake umekuwa ukiwashirikisha wananchi wenyewe, Rais Karume alisifu juhudi za wananchi hao.

Nae Muhandisi Mkaazi wa Idara ya Barabara Pemba, Khamis Masoud alimueleza Rais Karume kuwa kazi zinaenda vizuri na kuna matumaini makubwa ya kumaliza kwa wakati na kwa ufanisi zaidi.

Masoud alisema kuwa barabara hizo ni miongoni mwa barabara 6 zenye urefu wa kilomita 44.7 ambazo zimo katika Mradi huo wa Barabara za vijijini Kusini Pemba.

Alisema kuwa kazi nyingi za mwanzo katika ujeni huo zimeshalkuwa tayari kwa upande wa barabara ya Mtambile-Mwambe yenye urefu wa kilomita 9.4 ambapo tayari kilomita 2 zimeshaaza kutiwa lami.

Aidha, Masoud alisema kuwa kwa upande wa barabara ya Mtambile-Kangani yenye urefu wa kilomita 6.4 nayo kazi zake za ujenzi zinaenda vizuri. Pia, alisema kuwa barabara ya Miingani-Wambaa yenye urefu wa kilomita 9.7 nayo imo kwenye mchakato mbapo baada ya hapo barabara ya Kenya-Chambaani itafuatia.

Katika maelezo yake Mhandisi Mkaazi huyo alieleza kuwa kutokana na wananchi wengi kupata mafunzo juu ya ujenzi wa barara hatua hiyo imeweza kurahisisha ujenzi huo wa barabara ambapo hufanya kazi kwa makundi baada ya kupata utaalamu.

Masoud alisema kuwa utaalamu unaotumika wa Emulsion Treated Base (ETB) katika ujenzi wa barabara hizo kisiwani Pemba ambao hutumia lami baridi ni ujenzi wa mwanzo kwa nchi za Afrika za Mashariki na tayari nchi mbalimbali zimeomba kuja kisiwani Pemba kupata mafunzo zikiwemo Kenya, Msumbiji na nyenginezo

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi huyo ujenzi wa barabara hizo sita zilizomo katika Mradi huo unatarajiwa kukamilika Disemba mwaka 2011.

Barabara hizo zinajengwa na Idara ya Barabara chini ya ufadhili wa Serikali ya Norway hadi kumalizika kwake zitatumia zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 9.

Nao wananchi wa vijiji hivyo wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti walisifu juhudi za Rais Karume katika kuimarisha Maendeleo na uchumi wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuimarisha ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Walieleza kuwa juhudi za Rais Karume za kuimarisha miundombinu ya barabara kisiwani Pemba ni mkombozi mkubwa wa uchumi na maendeleo ya nchi na wananchi wake kwani faida kubwa itapatikana baada ya kumaliza ujenzi wa barabara hizo a,mbapo wananchi watarahisishiwa kufanya biashara kwa uhakika, kuimarisha kilimo, uwekezaji, uvuvi na shughuli nyengunezo.

Katika ziara yake hiyo, Rais Karume alifuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mkewe Mama Shadya Karume.

Jioni ya leo Rais Karume anatarajiwa kujumuika na Waislamu na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa ajili ya futari ya pamoja aliyowaandalia huko katika viwanja vya Ikulu ndogo ChakeChake Pemba.

Wednesday, September 1, 2010

RAIA WA AFRIKA YA KUSINI AJINYONGA KISIWANI PEMBA

Raia mmoja wa Afrika ya kusini amekutwa amekufa baada ya kujinyonga chumbani kwake katika hoteli ya Manta Riff iliyopo Micheweni Kisiwani Pemba.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kaskazini Pemba Rashid Yahya Bugi amesema raia huyo alitambuliwa kwa jina la James Ignatus White mwenye umri wa miaka 21 ni mfanyakazi wa hotel ya Manta Riff.

Amesema jeshi la polisi mara baada ya kupokea taarifa za tukio hilo lilikwenda katika eneo hilo na kuukuta mwili wa White ukiwa ananinginia katika kamba aliyojitundika.

Hata hivyo amesema chanzo cha kujiua kwa raia huyo wa kigeni bado hakijafahamika kwa vile hajawacha ujumbe wowote…

Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa uongozi wa hoteli ya Manta Riff kwa ajili ya kuusafirisha nchini kwao Afrika ya Kusini.

MAELFU YA WAUMINI WA KISLAMU WAMZIKA MUFTI MKUU WA ZANZIBAR

Maelfu ya waumini wa dini ya kislamu na wananchi wengine leo wamehudhuria maziko ya mufti mkuu wa Zanzibar sheikh Harith bin Helf aliefariki nchini India Alhamis iliyopita.

Maziko hayo yaliofanyika kijijini kwao Muyuni Wilaya ya Kusini yameongozwa na makamo wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Ali Mohammed Shein.

Viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo ni rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, waziri kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha na mufti mkuu wa Tanzania bara Sheikh Shaaban bin Simba na viongozi wengine wa serikali na kidini.

Marehemu Harith amezaliwa mwaka 1927 katika kijiji cha Muyuni alipata elimu ya msingi mwaka 1937 na elimu ya chuo kikuu cha Alzhar nchini Misri na kuchaguliwa mufti mkuu wa Zanzibar mwaka 1992.

Marehemu alifariki dunia nchini India katika hospitali ya Miyot alikukuwa akitibiwa ugonjwa wa moyo na uti wa mgongo. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi amina.

CHADEMA YATAKA RAIS KIKWETE AWEKEWE PINGAMIZI

Chama cha Demokraisa na maendeleo CHADEMA kimewasilisha malalamiko kwa msajili wa vyama vya siasa kikitaka mgombea wa urais wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM rais Jakaya Kikwete awekewe pingamizi katika kinyanganyiro cha uchaguzi wa urais.

Hoja kuu ya CHADEMA kuweka pingamizi ni kwa serikali kupandisha mishahara ya wafanyakazi waliokusudia kugoma wakati wa mkutano wa uchumi wa dunia, lakini rais Kikwete wakati huo alisema hawezikupandisha mishahara.

Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema hatua ya sasa ya serikali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma inahesabiwa kama yenye kutaka ungwaji mkono na wafanyakazi.

Mnyika amedai suala la nyongeza wa mishahara kwa wafanyakazi halikuongezwa na bunge kama vile ilivyopendekezwa hivyo suala hilo linatumiwa kama kampeni za mgombea huyo na kwenda kinyume na sherria ya gharama za uchaguzi

MGOMBEA URAIS KUPITIA SAU ASHINDWA KUREJESHA FOMU

Ikiwa leo ni siku ya mwisho kurejesha fomu za kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar, mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama Cha Sauti ya Umma (SAU) Haji Mussa Kitole ameshindwa kurejesha fomu za kuwania nafasi hiyo kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kitole awali alikataliwa kupewa fomu ya kuwania nafasi hiyo na ZEC kutokana na kuwa chama hicho kimetoa wagombea urais wawili wenye kutaka kuwania urais wa Zanzibar wakati sheria za ZEC zinaeleza chama kitowe mgombea mmoja wa nafasi hiyo.

Vyama ambavyo vimerejesha fomu leo katika afisi hiyo ni NCCR-MAGEUZI, TADEA, AFP, NRA, Jahazi Asilia huku chama cha SAU kikiwa bado hakijarejesha fomu hiyo.

Akizungumza na Zenji fm radio afisa wa habari wa tume ya uchaguzi Zanzibar Idriss Haji Jecha amesema hadi kufikia saa 9.45 cha cha SAU bado hakijarejesha fomu ambapo muda wa mwisho ulikuwa saa 10.00 jioni.

Amesema katika urejeshaji wa fomu hizo hakukuwa na kasoro zozote na fomu zilizorejeshwa zilikuwa safi.

SAU ndio chama pekee kilichoshindwa kuwasilisha fomu zake kwa tume ya uchaguzi ambapo vyama vyengine vilivyorejesha fomu zake jana ni pamoja Juma Ali Khatib (46) -TADEA, saa 4:13 asubuhi, Said Soud Said (62) AFP,saa 5:00, Haji Ambar Khamis (44) NCCR–Mageuzi, saa 5:30, Kassim Bakari Ali (43) Jahazi Asilia, saa 7.06, na Haji Khamis Haji (60) NRA saa 8:20 mchana.

Wengine waliorejesha fomu zao kwa ZEC wa mwanzo ni ni Mgombea wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ((67) alirejesha Agosti 16 majira ya saa 9:00 mchana wakati mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohammed Shein (62) alijesha fomu yake Agosti 18 majira ya saa 8:30 mchana.

Akizungumza katika kikao hicho baada ya kupokea fomu hizo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khatib Mwinchande alisema kwao wao kujitokeza kwa wagombea wengi ni kupanuka kwa demokrasia nchini.

Mwenyekiti huyo aliwaomba wagombea wote ambao watateuliwa na tume kuingia katika mchakato wa kutaka urais baada ya kuhakikiwa fomu zao kuingia katika kampeni za kistaarabu zisizo na matusi ili kuepusha Zanzibar kuingia katika sura mbaya ya kukosekana amani.

Iwapo wagombea urais kutoka vyama hivyo hawatawekewa pingamizi uchaguzi mkuu kwa nafasi ya urais unatarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu utakuwa na wagombea saba

TATIZO LA SOMALIA NI UINGILIAJI KATI WA MATAIFA YA KIGENI-HIZB UT-TAHARIR

Jumuiya ya kislamu ya kimataifa ya Hiz Ut-Tahrir imepinga ungiliaji kati unaofanywa na mataifa ya kigeni katika mzozo unaoendelea nchini Somalia kati ya wanamgambo wa Al-shabab na serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa naibu mwakilishi wa wa vyombo vya habari vya Jumuiya hiyo Afrika Mashariki Massoud Mselem amesema mzozo wa Somalia hauhitaji nguvu za kijeshi bali ni kuangalia kiini cha tatizo lenyewe.

Amesema suluhisho la amani ya Somalia sio kupambana na wanamgambo wa Al-Shabab bali ni kupinga uingiliaji kati wa masuala ya nchi hiyo dhidi ya mataifa ya kigeni…

Akizungumzia mateso na vitendo viovu wanavyofanyiwa waislamu wa Tajikistan Masoud ameitahadharisha dola hiyo na kusema iwapo hasara itatokea itarejea upande wa taifa hilo na kusema chama hicho kitajitolea kulingania utukufu wa mwezi mungu.

Amesema serikali ya Tajikistan inafanya makosa hayo huku ikiungwa mkono na madola ya magharibi na taasisi zinazodai kutetea haki za binadamu zikiwa zimekaa kimya.

Masoud amefahamisha zaidi ya waislamu 300 wa Tajikistan wanaendelea kusulubiwa kwa mateso, uonevu na vifungo vya muda mrefu.

Amesema Hiz ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani mateso na uharamia wanaofanyiwa waislamu wasiokuwa na hatia na utawala wa nchi hiyo unaongozwa na rais Rahmanov.

Jumuiya ya Hiz ut-Tahrir ni chama cha kislamu cha kimataifa chenye malengo ya kurejesha tena uislamu kupitia dola ya Helaf iliyoangushwa mwaka 1924.

RAIS KARUME AFUNGUA NYUMA YA WATOTO YATIMA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akifungua pazia kama ishara ya Uzinduzi wa Nyumba mpya ya watoto Yatima iliyopo Mazizini nje ya Mji wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amewataka wazazi na walezi kuchukuwa tahadhari ya kutowachia watoto wao kudhubaa mitaani.

Akifungua nyumba mpya ya kulelea watoto huko Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar mesema tabia hiyo itawajenga watoto kuishi maisha ya taabu na yasiokuwa na malengo yao ya baadae.

Dr. Karume amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kuiachia hali hiyo ikitokea kwa vile wazanzibari wote ni familia moja na wanadhamana ya kuwalea watoto wote.

Amesema mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 rais wa kwanza Abeid Karume ameanzisha kituo cha kulelea watoto huko Forodhani ili kuona watoto hao wanalelewa katika mazingira mazuri…

Aidha Dr. Karume amesema serikali imeamuwa kuwahamisha watoto wanaolelewa katika kutuo cha Forodhani kutokana na mazingira yaliopo katika eneo hilo hayafai tena kulelea watoto.

Amesema jengo hilo la Forodhani litaendelea kuwa mali ya serikali na kutumika kwa shughuli za makumbusho ya usafiri wa bahari ya Hindi chini ya usimamizi wa taasisi ya Agakhan Foundation.

Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho katibu wa afisi ya Mufti mkuu Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga amewataka waislamu kuendelea kuwatunza watoto yatima kulingana na mafundisho ya dini yao.

Amesema watu wanaowadhulumu watoto yatima kwa kula mali zao ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya kislamu na watu hao tayari wameshabashiriwa kuingia motoni

Nyumba hiyo mpya ya kulelea watoto yenye ghorofa moja, vyumba vya kuishi watoto 80 kwa wakati mmoja, ukumbi wa mikutano, vyumba vya kompyuta, kusomea, na zahanati ujenzi wake umesimamiwa na taasisi ya ZAYADESA na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 883

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CCM DR. SHEIN AREJESHA FOMU

Mgombea wa urais Zanzibar kupitia CCM Dr. Ali Mohammed Shein amesema ataitumikia Zanzibar kwa ufanisi mkubwa na kuweka mbele maslahi ya wananchi.

Akizungumza na wana CCM huko Kisiwandui muda mfupi baada kurudisha fomu za kuwania nafasi hiyo katika tume ya uchaguzi Zanzibar amesema atashirikiana vizuri na viongozi watakaokubali kufanyakazi kwa maslahi ya Zanzibar.

Aidha Dr. Shein ameonya kuwa hatamvumilia kiongozi yoyote ambae atakwenda kinyume na matakwa ya Wazanzibar endapo ataingia madarakani ……

Dr. Shein amesema katika uchaguzi ujao, CCM imejiandaa kuendesha kampeni za kistaarabu zenye kuwaelekeza wananchi malengo ya chama hicho ili wakipe ridhaa tena ya kuiongoza Zanzibar.

Nae naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Saleh Ramadhan Ferouz amewataka wafuasi wa chama hiho kupuuza matamshi yanayotolewa na baadhi ya watu kwamba kumtilia kura kiongozi wa upinzani ni sawa na kumpigia mgombea wa CCM.

Amesema watu hao wanaopotosha wana CCM kwa kusambaza vipeperushi vyenye ujumbe huo, amewataka wafuasi wa chama hicho kuwa makini juu ya mbinu hizo zinazofanywa na vyama vya upinzani.

Dk . Shein anakuwa mgombea wa pili kurejesha fomu zake kwa tume ya uchaguzi Zanzibar kati ya wagombea wanane waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 31 mwaka huu.

TANZANIA YATAKIWA KUBADILISHA KATIBA

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kupitia chama cha wananchi CUF Profia Ibrahim Harouna Lipumba amesema wakati umefika kwa watanzania kurekebisha katiba ili kuruhusu mgombea binafsi na kupanua wigo wa demokrasia nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni wa chama hicho kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mjini Dar es Salaam Profisa Lipumba amesema kutokuwepo kwa fursa hiyo kunanyima mianya ya demokrasia na kuwacha watu wenye sifa za kuongoza kutokana na kutojiunga na vyama vya siasa.

Aidha Profisa Lipumba amesema endapo atachaguliwa kuwa rais amesema atapunguza umasikini unaowakabili watanzania……

Hii ni mara ya nne kwa profisa Lipumba kuwania urais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kupita CUF tangu mfumo wa vyama vingi kuanza mwaka 1992.

CHADEMA KUMUWEKEA PINGAMIZI RAIS KIKWETE

Kaimu katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA John Mnyika amesema chama hicho kinaendelea na taratibu zake katika afisi ya msajili wa vyama vya siasa na tume ya uchaguzi ya taifa kupinga kile alichodai mgombea wa urais kupitia CCM rais Jakaya Kikwete kukiuka sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010.

` Wakati CHADEMA ikiendelea na harakati hizo naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania Bara Peuce Msekwa amesema mgombea huyo hajavunja kifungu chochote cha sheria na inasubiri suala hilo liwasilishwe katika afisi husika ili itowe utetezi wake.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mgombea urais wa wa CHADEMA Dr. Wilbord Slaa amepanga kuwasilisha pingamizi kwa msajili wa vyama vya sisasa nchini John Tendwa kwa madai mgombea urais wa CCM rais Jakaya Kikwete amevunja kifungu nambari 21 cha sehria ya gharama za uchaguzi.

MUFTI MKUU WA ZANZIBAR AFARIKI DUNIA NCHINI INDIA

Mufti mkuu wa Zanzibar Sheikh Harith bin Khelef Khamis amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini India katika hospital ya Meyot ambapo alikuwa anapata matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Mufti imesema kwamba Mufti amefariki dunia jana asuhuhi katika hospitali ya Meyot Mjini Chanay nchini Idia

Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga amesema Zanzibar imepata msiba mkubwa kwa kuondokewa na kiongozi wake huku akisisitiza wananchi kuwa na subra katika msiba huo.

“Nchi yetu imepatwa na msiba mkubwa sana kwa kuondokewa na kiongozi mkuu wa dini visiwani ambaye alikuwa matibabuni kwenye hospitali ya Meyot Mjini Chenay nchini India” alisema Sheikh Soraga.

Soraga alisema mipango ya kusafirisha mwili wa mrehemu inaendelea kwa mashirikiano makubwa na ubalozi wa Tanzania nchini India huku maandalizi ya kuupokea mwili wa marehemu kwa heshima zote za kitaifa yanaendelea.

Alisema wananchi wataelezwa rasmi juu ya suala hilo lilipofikia baada ya kuwasili kwa maiti na muda wa mazishi hayo yatapangwa baada ya kufika Zanzibar mwili wa marehemu.

“Kwa taarifa hii waumini na wananchi wote kwa ujumla wanaombwa kuwa watulivu na kuungana pamoja katika kuukabili msiba huu mkubwa kitaifa” alisema taarifa hiyo iliyosainiwa na katibu wa Mufti Sheikh Soraga.

Licha ya kuwa taarifa ya serikali haikueleza Mufti alipelekwa nchini India kwa ugonjwa gani lakini taarifa za undani zinasema kwamba alipelekwa baada ya kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na matatizo ya figo.

Akizungumza bila ya kutaka kutajwa jina lake gazetini kwa madai kwamba sio msemaji wa familia alisema wakati wa uhai wake Sheikh Harith alikataa kusafirishwa kupelekwa India kutokana na hali yake lakini baada ya kuonekana hali yake imezidi kuzorota ilimshauri kumpeleka matibabuni India.

Hatika hatua nyengine takriban misikiti yote leo Zanzibar imetoa tangazo la kifo cha Mufti na kuwataka waumini wamuombee dua katika kipindi hiki muhimu cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

“Tuna masikitiko makubwa kwa kuondokewa na kiongozi wetu msomi wetu na muumini mwenzetu Mufti wa Zanzibar Sheikh Harith Bin Khelef huko nchini India alipokwenda kwa matibabu kwa hivyo tumuombeeni sana dua Mwenyeenzi Mungu amsameh madhambi yake” alisema Sheikh Abrahaman Habshi imamu mkuu wa msikiti wa Jibril Mkunazini.

Mufti Khelef mwenye umri wa miaka 80 ni miongoni mwa wasomi na wanazuoni wakubwa ambao wamebahatika kusoma katika chuo kikuu maarufu cha Kiislamu kiliopo Misri Al-Azhar katika miaka ya 1960.

Chuo kikuu cha Al-Azhar ni maarufu sana katika bara la Afrika na duniani ambacho hutoa elimu mbali mbali za dini ya kiislamu pamoja na masomo mengine ya lugha za kiarabu.

Marehemu Khelef aliteuliwa kuwa Mufti mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka 1995 wakati wa uongozi wa rais mstaafu Dk Salmin Amour Juma.

Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kutoka India inafanywa na ofisi ya mufti wa Zanzibar ambayo ipo chini ya Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala bora.