Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akifungua pazia kama ishara ya Uzinduzi wa Nyumba mpya ya watoto Yatima iliyopo Mazizini nje ya Mji wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amewataka wazazi na walezi kuchukuwa tahadhari ya kutowachia watoto wao kudhubaa mitaani.
Akifungua nyumba mpya ya kulelea watoto huko Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar mesema tabia hiyo itawajenga watoto kuishi maisha ya taabu na yasiokuwa na malengo yao ya baadae.
Dr. Karume amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kuiachia hali hiyo ikitokea kwa vile wazanzibari wote ni familia moja na wanadhamana ya kuwalea watoto wote.
Amesema mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 rais wa kwanza Abeid Karume ameanzisha kituo cha kulelea watoto huko Forodhani ili kuona watoto hao wanalelewa katika mazingira mazuri…
Aidha Dr. Karume amesema serikali imeamuwa kuwahamisha watoto wanaolelewa katika kutuo cha Forodhani kutokana na mazingira yaliopo katika eneo hilo hayafai tena kulelea watoto.
Amesema jengo hilo la Forodhani litaendelea kuwa mali ya serikali na kutumika kwa shughuli za makumbusho ya usafiri wa bahari ya Hindi chini ya usimamizi wa taasisi ya Agakhan Foundation.
Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho katibu wa afisi ya Mufti mkuu Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga amewataka waislamu kuendelea kuwatunza watoto yatima kulingana na mafundisho ya dini yao.
Amesema watu wanaowadhulumu watoto yatima kwa kula mali zao ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya kislamu na watu hao tayari wameshabashiriwa kuingia motoni
Nyumba hiyo mpya ya kulelea watoto yenye ghorofa moja, vyumba vya kuishi watoto 80 kwa wakati mmoja, ukumbi wa mikutano, vyumba vya kompyuta, kusomea, na zahanati ujenzi wake umesimamiwa na taasisi ya ZAYADESA na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 883
Wednesday, September 1, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment