Mufti mkuu wa Zanzibar Sheikh Harith bin Khelef Khamis amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini India katika hospital ya Meyot ambapo alikuwa anapata matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Mufti imesema kwamba Mufti amefariki dunia jana asuhuhi katika hospitali ya Meyot Mjini Chanay nchini Idia
Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga amesema Zanzibar imepata msiba mkubwa kwa kuondokewa na kiongozi wake huku akisisitiza wananchi kuwa na subra katika msiba huo.
“Nchi yetu imepatwa na msiba mkubwa sana kwa kuondokewa na kiongozi mkuu wa dini visiwani ambaye alikuwa matibabuni kwenye hospitali ya Meyot Mjini Chenay nchini India” alisema Sheikh Soraga.
Soraga alisema mipango ya kusafirisha mwili wa mrehemu inaendelea kwa mashirikiano makubwa na ubalozi wa Tanzania nchini India huku maandalizi ya kuupokea mwili wa marehemu kwa heshima zote za kitaifa yanaendelea.
Alisema wananchi wataelezwa rasmi juu ya suala hilo lilipofikia baada ya kuwasili kwa maiti na muda wa mazishi hayo yatapangwa baada ya kufika Zanzibar mwili wa marehemu.
“Kwa taarifa hii waumini na wananchi wote kwa ujumla wanaombwa kuwa watulivu na kuungana pamoja katika kuukabili msiba huu mkubwa kitaifa” alisema taarifa hiyo iliyosainiwa na katibu wa Mufti Sheikh Soraga.
Licha ya kuwa taarifa ya serikali haikueleza Mufti alipelekwa nchini India kwa ugonjwa gani lakini taarifa za undani zinasema kwamba alipelekwa baada ya kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na matatizo ya figo.
Akizungumza bila ya kutaka kutajwa jina lake gazetini kwa madai kwamba sio msemaji wa familia alisema wakati wa uhai wake Sheikh Harith alikataa kusafirishwa kupelekwa India kutokana na hali yake lakini baada ya kuonekana hali yake imezidi kuzorota ilimshauri kumpeleka matibabuni India.
Hatika hatua nyengine takriban misikiti yote leo Zanzibar imetoa tangazo la kifo cha Mufti na kuwataka waumini wamuombee dua katika kipindi hiki muhimu cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
“Tuna masikitiko makubwa kwa kuondokewa na kiongozi wetu msomi wetu na muumini mwenzetu Mufti wa Zanzibar Sheikh Harith Bin Khelef huko nchini India alipokwenda kwa matibabu kwa hivyo tumuombeeni sana dua Mwenyeenzi Mungu amsameh madhambi yake” alisema Sheikh Abrahaman Habshi imamu mkuu wa msikiti wa Jibril Mkunazini.
Mufti Khelef mwenye umri wa miaka 80 ni miongoni mwa wasomi na wanazuoni wakubwa ambao wamebahatika kusoma katika chuo kikuu maarufu cha Kiislamu kiliopo Misri Al-Azhar katika miaka ya 1960.
Chuo kikuu cha Al-Azhar ni maarufu sana katika bara la Afrika na duniani ambacho hutoa elimu mbali mbali za dini ya kiislamu pamoja na masomo mengine ya lugha za kiarabu.
Marehemu Khelef aliteuliwa kuwa Mufti mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka 1995 wakati wa uongozi wa rais mstaafu Dk Salmin Amour Juma.
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kutoka India inafanywa na ofisi ya mufti wa Zanzibar ambayo ipo chini ya Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala bora.
Wednesday, September 1, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment