I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, September 1, 2010

RAIA WA AFRIKA YA KUSINI AJINYONGA KISIWANI PEMBA

Raia mmoja wa Afrika ya kusini amekutwa amekufa baada ya kujinyonga chumbani kwake katika hoteli ya Manta Riff iliyopo Micheweni Kisiwani Pemba.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kaskazini Pemba Rashid Yahya Bugi amesema raia huyo alitambuliwa kwa jina la James Ignatus White mwenye umri wa miaka 21 ni mfanyakazi wa hotel ya Manta Riff.

Amesema jeshi la polisi mara baada ya kupokea taarifa za tukio hilo lilikwenda katika eneo hilo na kuukuta mwili wa White ukiwa ananinginia katika kamba aliyojitundika.

Hata hivyo amesema chanzo cha kujiua kwa raia huyo wa kigeni bado hakijafahamika kwa vile hajawacha ujumbe wowote…

Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa uongozi wa hoteli ya Manta Riff kwa ajili ya kuusafirisha nchini kwao Afrika ya Kusini.

No comments:

Post a Comment