I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, June 23, 2010

MKATABA WA MUUNGANO WADAIWA BUNGENI

Kambi ya upinzani bungeni imeomba kupatiwa mkataba wa asili wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ambao unaweza kuyapatia ufumbuzi baadhi ya matatizo yaliomo kwenye muungano huo.

Akizungumza na Zenji Fm radio msemaji wa kambi hiyo katika mambo ya muungano Riziki Omar Juma amesema serikali bado inashikilia mkataba huo na hauwekwi wazi kwa wananchi.

Amesema mkataba huo tayari umeshadaiwa ndani ya bunge na serikali kuahidi kwamba mbunge yoyote anaweza kuuona, lakini hadi sasa bado mkataba huo umekuwa siri.

Riziki amesema lengo la kutaka kuonekana mkataba huo ni kutaka kuufanyia marekebisho kama utaonekana kuwa na kasoro ili kila upande unufaike na maslahi ya muungano…..

Akizungumza na Zenji Fm radio juu ya madai hayo waziri wa muungano Mohammed Seif Khatib amesema mikataba hiyo iko ikulu ya rais mjini Zanzibar na ikulu ya rais wa muungano mjini Dar es Salaam.

Hata hivyo amesema hati hizo zinakuwa na umuhimu pale sheria na katiba hazijaundwa na baada ya vitu hivyo kuwepo mikataba hiyo haina umuhimu sana kama inavyodaiwa…

Hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya kikundi cha watu wanaodai hati halisi ya muungano na kutishia kufungua kesi katika mahakama ya umoja wa mataifa baada madai yao kutupiwa mbali na mahakama kuu ya Zanzibar.

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA MABALOZI

Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi na kuwahamishia vituo vyao vya kazi mabalazi saba kushika nyadhifa mbali mbali za kibalozi nje ya Tanzania.

Mabalozi hao ni pamoja Mohammed Mwinyi Mzale anaekuwa balozi wa Tanzania nchini Sweeden, Alexanda Masinda anaekwenda nchini Canada, Peter Alen Nkalage anakuwa balozi mpya nchini Uingereza.

Dansan Joram anaekuwa balozi wa Tanzania nchini Etheopia, Egum Karim Haji anaekwenda Ufaransa na balozi Ombeni Chubuwe ameteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu katika umoja wa mataifa.

Dr. Omar Mohammed aliekuwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na umoja wa Afrika amerejeshwa nchini atakuwa mkuu wa chuo cha Diplomasia mjini Dar es Salaam.

MKUZA WALETA MAFANIKIO Z’BAR

Mpango wa kukuza uchumi na kuimarisha umasikini Zanzibar umelezewa kupata mafanikio katika sekta ya kilimo na biashara.

Akizunguma na Zenji Fm radio mchumi wa Zanzibar Dr. Mohammed Hafidhi amesema inagawa wananchi wanahitaji maendeleo makubwa zaidi kuliko hayo yaliofikiwa.

Amesema mafanikio hayo yanatokana na kuliweza baraza la biashara la Zanzibar kufanaya kazi zake vizuri kumeziwezesha sekta za kilimo na biashara kupiga hatua kubwa za maendeleo.

Aidha amesema MKUZA pia umesaidia kuendeleza sekta ya ufugaji kwa kuanzisha miradi mbali mbali kama vile PADEP, ASP pamoja na kutoa mafunzo ambayo lengo lake ni kuendeleaza wafugaji.

Hata hivyo Dr. Hafidh amesema bado mpango huo uanakabiliwa na changamoto ikiwemo kudhorota kwa sekta ya viwanda, uvuvi na kuongeza wigo wa mapato ya serikali

WAGOMBEA URAIS CCM WACHUKUA FOMU LEO

anachama Saba wa chama cha Mapinduzi CCM, tayari wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho katika afisi kuu ya CCM Kisiwandui.

Wanachama hao ni waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, makamo wa rais Dr. Ali Mohammed Shein, waziri kiongozi wa zamani Dr. Mohammed Gharib Bilal na naibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna.

Wengine ni naibu waziri wa Afrika mashariki Mohammed Aboud, balozi Ali Abeid Karume na kamishna mstaafu wa utamaduni Hamad Bakar Mshindo.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wagombea hao wametaja kuimarisha sekta za maendeleo zikiwemo elimu, kilimo, miundo mbinu ya usafiri pamoja na kuondoa malumbano ili kuwaunganisha wazanzibari kuwa kitu kimoja.

Wamesema Zanzibar bado inakabiliwa na changamoto za kiuchumi hivyo watajenga mazingira mazuri ikiwani pamoja na kuimarisha sekta za kazi ili kutoa huduma nzuri pamoja na kubuni nafasi za ajira.

Aidha viongozi hao wamesema wataendelea kuimarisha muungano ili kuleta mafanikio zaidi kwa wananchi na kuendelea kuyapatia fumbuzi baadhi ya matatizo yaliosalia kwa lengo la kuleta maslahi kwa pande zote mbili.

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi fomu wagombea hao katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Vuai Ali Vuai amesema kamati kuu ya halamshauri itapitia sifa za wagombea hao na kutoa mapendekezo yake kwa majina matatu kwa halmashauri kuu ya taifa kwa uteuzi wa mwisho…

Afisi kuu ya CCM bado inaendelea kutoa fomu kwa wanachama wengine wanaotaka kuwania urais wa Zanzibar kupitia chama hicho hadi Julai mosi mwaka huu.

Idadi hiyo ya wananchama waliojitokeza kuchukua fomu ya kukiomba chama chao kuwateuwa kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar ni kubwa ikilinganishwa na wanachama waliojitokeza kumrithi rais wa zamani Dr. Salmin Amour Juma mwaka 2000.

Wachambuzi wa masuala ya siasa Zanzibar wanasema uchaguzi wa rais mwaka 2010 utakuwa na upinzani mkali na vyama vikuu viliwi vya siasa vyenye wafuasi wengi CCM na CUF vitahitaji kufanya kazi ya ziada.

SERIKALI YA MSETO Z’BAR YAUNGWA MKONO NA WAISLAM

Jumuiya ya Maimamu Zanzibar JUMAZA imesema inaunga mkono kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kama hatua moja wapo ya kuimarisha amani na utulivu nchini.

Katibu Mtendaji wa JUMAZA sheikh Muhdin Zuber Muhdini amesema hatua hiyo ni kuzishukuru neema za mwenyezi mungu zilizoondosha siasa za chuki zilizoleta mirafarakano na uadui

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa amesema serikali ya umoja wa kitaifa ndio suluhisho la kuleta amani, hivyo amewataka wananchi kushiriki katika kura ya maoni ili kutoa ridhaa ya kuundwa serikali hiyo…

Hata hivyo Sheikh Muhidin amesema jumuiya hiyo haiwezi kuwalazimisha wananchi kutumia uhuru wao wa kuamua, lakini jumuiya za waislamu zinajukumu la kuielekeza jamii umuhimu wa kulinda amani na utulivu.

Aidha jumuiya hiyo pia imewataka wananchi kuendeleza amani na utulivu uliopo hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa kuwachagua viongozi mbali mbali wa nchi.

Tamko hilo la JUMAZA la kuunga mkono kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa limefikiwa katika kikao chake kilichofanyika June 12 mwaka huu na kuzishirikisha jumla ya taasisi 18 za kislamu

Saturday, June 19, 2010

MABADILIKO YA HALI YA HEWA HAYATAIATHIRI Z,BAR

izara ya kilimo mifugo na mazingira imesema tishio la dunia la kuzama kwa visiwa vidogo duniani miaka 50 ijayo kutokana na uharibifu wa mazingira halivihusu visiwa vya Zanzibar.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi naibu waziri wa wizara hiyo Khatib Suleiman Bakar amesema tishio hilo limetolewa kwa visiwa vya Maldives na sio visiwa vya Zanzibar.

Hata hivyo amesema wizara imekuwa ikitoa elimu ya kuhifadhi mazingira juu ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa kutokana nakupanda kwa kina cha bahari katika baadhi ya vijiji vya ukanda wa pwani

Akijibu suala la nyongeza waziri wa wizara hiyo Burhan Saadat Haji amesema serikali inamalizia utafiti wa kupitia visiwa vyote vya Unguja na Pemba ili kuangalia maeneo yalioathirika na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema mara baada ya kumalizika utafiti huo serikali itaangaliza uwezekano wa kudhibiti maeneo yanayovamiwa na maji ya bahari hasa maeno ya kilimo Pemba kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo…

WALIOKOSA KUJIANDIKISHA WASTAHAMILI-HAMZA

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka watu waliokosa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura wastahamili hadi pale tume ya uchaguzi itakapofanya usajili kwa ajili ya chaguzi nyingine. Waziri wa nchi afisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma amesema, hivi sasa tume ya uchaguzi haina muda tena wa kurudia kazi za uandikishaji baada ya kumalizika wamu tatu tofauti za usajili.

Akijibu maswali katika kikao cha baraza la wawakilishi Juma amesema tume imefanikiwa kuandikisha zaidi ya asilimia 80 idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na nchi zilizoendelea

Aidha waziri Juma amesema idadi ya wapiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2010 ni ndogo ikilinganishwa na mwaka 2005 inatokana na hiari mtu mwenyewe kujiandikisha au la kutumia teknolojia inayozuwia watu kujiandikisha zaidi ya mara moja.

Hata hivyo amesema watu waliobainika kujiandikishwa mara mbili, watapata haki ya kupiga kura, lakini watafikishwa mahakamani kutokana na kukiuka taratibu za uandikishaji……

Tume ya uchaguzi Zanzibar imeandikisha wapiga kura laki nne, 8,401 katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu wakati idadi ya watu waliopata vitambulisho vya ukaazi ni zaidi ya laki tano

CCM ZANZIBAR WAJITOKEZA KUWANIA URAIS 2010

Wanachama sita wa chama cha Mapinduzi CCM wamejitokeza kutaka kuwania kiti cha urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Wanachama hao waliojitokeza ni makamo wa rais Dr. Ali Mohammed Shein, waziri kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha na waziri kiongozi wa zamani Dr. Mohammed Gharib Bilal.

Wengine ni naibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna, balozi Ali Abeid Karume na Hamad Bakar Mshindo.

Akiwasilisha majina hayo kwa wandishi wa habari katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Vuai Ali Vuai amesema wanachama hao watachukua fomu siku ya Jumatatu na kusema shughuli hiyo haitakuwa na sherehe.

Amesema fomu za kuwania nafasi hiyo zitaendelea kutolewa kuanzia tarehe 21 mwezi huu hadi Julai mosi kwa wananchama wengine wanaotaka kuwania nafasi hiyo kupitia CCM na kurejesha ndani ya kipindi hicho.

Vuai amesema wanachama hao watalipia fomu hiyo shilingi milioni moja na mwisho wa kurejesha fomu hiyo Juali mosi saa 10.00 jioni ikiwa na wadhamini 250 kutoka mikoa yote ya Zanzibar.

Amesema afisi bado inaendelea kuwakaribisha wanachama wengine watakaokuwa tayari kuchukua fomu za kuwania urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuwania nafasi hiyo akiwemo

Ali Juma Shamhuna

naibu waziri wa Afrika mashariki Mohamed Aboud, waziri wa muungano Mohammed Seif Khatib na waziri wa Elimu Haroun Ali Suleiman bado hawajajitokeza hadharani kutangaza nia zao za kuwania nafasi hiyo.

Waziri kiongozi wa zamani Dr. Gharib hii ni mara yake ya tatu kukiomba chama chake kumteuwe kuwania urais wa Zanzibar ambapo mwaka 2005 aliombwa kujiondoa ili kumwachia rais Karume aendelee na kipindi cha pili cha miaka mitano kinachotarajiwa kumalizika Octoba mwaka huu

MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA IMESEMA MGOMBEA BINAFSI NI SUALA LA KISIASA

Mahakama ya Rufaa nchini imesema haina mamlaka ya kuamua juu ya mgombea binapsi na kwamba mwenye mamlaka wa kuamua hilo ni Bunge na wananchi wenyewe .

Uamuzi huo umetolewa chini ya jopo la majaji saba likiongozwa na Jaji mkuu Agostino Ramadhan katika mahakama ya Rufaa jijini Dar es salaam.

Mahakama hiyo imesema suala hilo ni la kisiasa zaidi na si lakisheria hivyo uamuzi zaidi unahitajika kutolewa na wananchi wenyewe na kueleza kuwa uamuzi huo utakao tolewa ni vyema kuzingatia historia ya Tanzania na matakwa ya wananchi.

MSAMAHA WA KIKWETE HAUHUSU WAFUNGWA WA ZANZIBAR-SMZ

erikali ya mapinduzi Zanzibar imesema msamaha wa wafungwa unaotolewa na rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania hauhusu wafungwa walioko katika vyuo vya mafunzo vya Zanzibar.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa nchi afisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma amesema kila upande wa muunganoi una mamlaka yake , hivyo rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ndio mwenye mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa walioko Zanzibar na rais wa mungano anatoa msamaha kwa wafungwa walioko Tanzania bara.

Amesema licha ya Tanzania kuwa na mahakama moja ya rufaa inayoziunganisha nchi zote mbili, lakini wananchi watakaopatikana na hatia na kupewa adhabu ya kifungo wafungwa watapewa misahama kwa majibu wa mamla wa nchi hizo mbili.

Nae waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha akiongezea majibu ya suala hilo amesema katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na katiba ya Zanzibar kuna mgawanyo maalumu ya mamlaka kulinga na makubaliano ya pande mbili za muungano.

Hivyo hivyo amesema serikali haitapanua wigo ambao unaweza Zanzibar kunyimwa mamlaka yake

Wednesday, June 16, 2010

LIBENEKE LA MTANZANIA AKIWA INDIA


www.allyshams.blogspot.com

TASAF KULETA MATUMAINI TANZANIA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zote kwa pamoja zimepanga mikakati maalum kwa ajili ya kuwapunguzia wananchi wake makali ya umasikini.

Rais Karume aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu miradi ya jamii kwa nchi zinazoendelea unaofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa AICC Mjini Arusha.

Rais Karume ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, alieleza kuwa Serikali zote mbili za Tanzania zinatambua umuhimu wa kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ambao huwashirikisha wadau wengi.

Alieleza kuwa katika kipindi chote ambacho TASAF imekuwa ikifanya kazi jumla ya miradi 11,375 ya jamii imepatiwa misaada kutoka mfuko huo wenye thamani ya Dola za Kimarekani 164,446,823.

Rais Karume alieleza kuwa kati ya miradi yote iliyopata misaada kutoka TASAF 928 ilikuwa ni kwa ajili ya kazi za kijamii yenye thamani ya Dola za Kimarekani 21,422,495.28 iliyowanufaisha jumla ya watu 217,315.

“Tokea kuanzishwa kwa TASAF tayari umeshawanufaisha watu 15,320,58 ambao wameweza kuzitumia huduma zilizotolewa baada ya kukamilika kwa miradi ya kijamii katika maeneo yao”,alieleza Rais Karume.

Aidha, Rais Karume alisema kuwa TASAF imekuwa ikifanya kazi vizuri Zanzibar na tayari imeshatoa kiasi cha Dola za Kimarekani 2.50 milioni kwa ajili ya kusaidia miradi mbali mbali maendeleo katika awamu ya pili iliyoanza mwaka 2005.

Pia, Rais Karume iliisifu TASAF kwa misaada midogo midogo inayotolewa kutoka katika Mfuko huo.

“Mahitaji ya familia yanaongezeka lakini kipato hakiongezeki, kutokana na sababu hii Serikali ya Tanzania imetambua umuhimu wa kuanzisha mfuko wa Mandeleo ya Jamii (TASAF), ambapo matatizo mbali mbali yanayozikabili jamii yamekuwa yakishughulikiwa kwa kiasi kikubwa”,alisisitiza Rais Karume.

Alieleza kuwa Mpango wa Maendeleo wa muda mrefu wa Dira ya 2025 kwa Tanzania Bara na ule wa 2020 kwa Zanzibar unatambua umuhimu wa kuwawezesha watu mbali mbali katika makundi tofauti wakiwemo wale wanaoishi katika mazingira magumu.

Akihutubia katika mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 45 duniani, Rais Karume alisema kuwa mkutano huo unafanyika wakati dunia ikiwa katika jitihada kubwa ya kutatua matatizo yaliyojitokeza kutokana na kutetereka kwa uchumi na mfumo wa fedha wa duniaambao umeathiri shughuli za kibiasahara na kushuka kwa sekta ya uwekezaji duniani.

Rais Karume alieleza kuwa pale uchumi wa dunia unaposhuka matatizo yanayotokea katika mataifa makubwa yenye nguvu za kiuchumi athari zinazotokezea huzikumba na nchi ndogo..

Alieleza kuwa miongoni mwa athari hizo ni pamoja na kuwepo kiwango kidogo cha uwekezaji na kutetereka kwa sekta ya Utalii ambapo nako kumechangia kushuka kwa soko la ajira na mapato ya serikali ambapo pia, imepelekea kuathiri utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya kijamii.

Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. Sophia Simba alieleza kuwa TASAF imekuwa na umuhimu mkubwa katika kuimarisha shughuli za maendeleo ya kijamii hapa Tanzania na kuishukuru Benki ya Dunia kwa uwamuzi wake wa kufanya mkutano wake huo muhimu hapa nchini.

Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bwana John Murray McIntire alieleza kuwa Benki ya Dunia itaendelea kuunga mkono katika kufanikisha Miradi ya TASAF kwa kutambua umhimu wake katika maendeleo ya jamii.

Alieleza kuwa miongoni mwa nchi zilizopata mafanikio katika Mfuko huo wa TASAF ni pamoja na Tanzania ambayo imeweza kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo.

Wakati huo huo Rais Karume alikagua maonyesho yaliyotayarishwa na TASAF na kuona jinsi mfuko huo unavyofanya kazi kutokana na maelezo aliyokuwa akipewa na watayarishaji husika

TAKUKURU KUWA CHUKULIA HATUA WAGOMBEA WANAOTOA ZAWADI

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU Dr. Eduward Husea amesema taasisi hiyo inazifanyia kazi taarifa za wagombea wa nafasi mbali mbali katika uchaguzi mkuu ujao walioanza kutoa vitu kama zawadi.

Akizungumza na wahariri wa habari katika semina juu ya sheria mpya ya uchaguzi mjini Dar es Salaam amesema taarifa za wagombea hao zitakapokamilika wataanza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha amesema suala hilo litachukua muda mrefu kutokana na kuthibitisha tuhuma hizo na kusema sheria hiyo itasaidia kuzuwia na kupambana na rushwa wakati wa uchaguzi ili kuwapata viongozi safi na waadilifu.

Aidha dr. Husea amesema ni kinyume cha sheria kwa baadhi ya watu kutumia madhehebu ya dini kama maeneo ya kufanyia kampeni na watakapobainika sheria itachukua mkondo wake.

VIJANA CHAGUWENI VIONGOZI WATAKAOMALIZA UMASIKINI ZANZIBAR-SHAMHUNA

aibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna amewataka vijana kuwasaidia wazanzibari wenzao katika kumpata kiongozi atakaeweza kupambana na umasikini na kutatua tatizo la ajira linalowakabili hivi sasa.

Akizungumza katika mafunzo ya elimu ya demokrasi huko Eacrotanal mjini hapa amesema Zanzibar bado inakabiliwa na umasikini unaosabisha ukosefu wa ajira na mfumko wa bei za bidhaa, hivyo ni vyema kwa vijana kuwa makini wakati wanapofanya maamuzi yao katika uchaguzi utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Shamhuna ambae pia ni waziri wa habari utamaduni na michezo pia amewataka vijana kujiepusha na siasa zinazolenga kubomowa umoja wa Zanzibar kwa jiepusha na ushawishi wa wanasiasa wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi.

Amesema vijana wengi wamekuwa wakijitumibikiza katika siasa chafu kutokana na kukosa elimu ya demokrasia, hivyo amesema serikali itaendelea kuunga mkono taasisi zinazoendelea kutoa elimu hiyo ikiwemo REDET.

Nae mwakilishi kutoka ubalozi wa Norway amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha elimu ya demokrasia nchini.

Amesema licha ya Zanzibar kuingia katika maridhiano ya kisiasa ambayo yamepongezwa na nchi nyingi duniani, lakini inahitaji kuendeleza maridhiano hayo ili kuwa na demokrasia ya kweli.

Mafunzo hayo ya muhula wa 21 yanayoendeshwa na taasisi ya chuo kikuu cha Dar es Salaam REDET yanawashirikisha vijana 50 kutoka jumuia za kiraia za Unguja na Pemba.

DR. SHEIN AKEMEA WANA CCM WANAOFANYA KAMPENI MAPEMA

Makamo wa rais Dr. Ali Mohammed Shein amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi wa matawi na majimbo kuacha kuendesha shughuli za chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao bila ya kufuata utaratibu unaotakiwa.

Amesema misingi ya demokrasia katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao ni lazima ifuatwe ili kuondoakasoro zinazoweza kutokea katika kufanikisha uchaguzi huo.

Dr. Sheina amesema hayo wakati akizungumza na makatibu wa CCM wa mkoa mjini magharibi baada kumaliza ziara yake ya siku mbili ya kukagua matawi ya chama hicho na kuangalia majina ya wanachama katika madaftari ya chama hicho.

PETROLI KUCHANGANYWA NA MAFUTA YA TAA NI AIBU KWA TANZANIA

Tatizo la uchanganyaji wa mafuta ya taa na petroli limeelezewa suala ni aibu kwa taifa.

Wakichangia hotuba ya bajeti ya serikali ya muungano mjini Dodoma baadhi ya wabunge wamehusisha tatizo hilo na tukio la hivi karibuni mkoani Kilimanjaro la baadhi ya gari za msafara wa rais kuzima baada ya kujazwa mafuta yanayosadikiwa kuchanganywa na mafuta ya taa.

Wabunge hao wamesema chanzo ni nafuu ya kodi katika mafuta ya taa ambaYo haIna maslahi kwa wananchi na kupendekeza unafuu huo uondolewe.

Miongoni mwa waliochangia bajeti hiyo ni mbunge wa Morogoro Dr. Omar Mzeru

KUWEIT KUISAIDIA ZANZIBAR SEKTA YA ELIMU

UWAIT imeahidi kuendelea kuinga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu kutokana na mafanikio makubwa yaliopatika sanjari na mikakati madhubuti iliyojiwekea katika kuimarisha sekta hiyo.

Mjumbe wa Bodi wa Afrika Muslim Agency kutoka Kuwait ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Juu la Chuo Kikuu cha Elimu Zanzibar Dk. Abdulrahman Saleh Muhailan akiwa na ujumbe wake aliyasema hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume.

Katika maelezo yake Dk. Saleh alimueleza Rais Karume kuwa Kuwait inathamini sana juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu na kuahidi kuongeza nafasi za masomo kwa Wazanzibar nchini humo.

Alieleza kuwa hatua hiyo inatokana na Kuwait kuwa na uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati yake na Zanzibar.

Alisema kuwa tayari Afrika Muslim Agency imekuwa ikiendelesha shughuli za elimu kwa muda mrefu na kuweza kuwa na vyuo vingi na skuli katika nchi mbali mbali za bara la Afrika ikiwemo Zanzibar.

Dk. Saleh alimueleza Rais Karume kuwa Chuo Kikuu cha Elimu Zanzibar kinathamini sana ushirikiano uliopo kati yake na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hali ambayo imepelekea kuendelea kupata mafanikio zaidi katika chuo hicho.

Pamoja na Dk. Saleh alimkabidhi Rais Karume hati yenye ‘password’ kwa ajili ya kutumia vitabu vilivyopo katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Gulf kiliopo nchini Kuwait.

Dk. Saleh alimueleza Rais Karume kuwa hatua hiyo itawasaidia wanafunzi wa Zanzibar kupata kusoma vitabu, majarida na taarifa mbali mbali kutoka Maktaba hiyo kwa njia ya Mtandao.

Nae Rais Karume kwa upande wake alitoa shukurani kwa kiongozi huyo pamoja na nchi ya Kuwait kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi mbili hizo.

Rais Karume alisema kuwa Zanzibar ina historia refu na Kuwait hatua ambayo imeweza kuimarika hadi leo hii.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imo katika kuimarisha sekta ya elimu ambayo tayari imeshapata mafanikio makubwa.

Rais Karume alisema kuwa mbali ya sekta ya elimu, tayari sekta mbali mbali za maendeleo hapa nchini zimeweza kupata mafanikio na kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Aidha, Rais Karume alieleza kuwa kutokana na juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta zake za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu imekuwa chachu kwa washirika wa maendeleo kuendelea kuiunga mkono Zanzibar.

Rais Karume alieleza kuwa hivi Karibuni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana saini na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa ajili ya kuziunganisha skuli zote za Unguja na Pemba katika mtandao hivyo hatua ya Taasisi ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Gulf nchini Kuwait ya kusaidia njia ya kupata kusoma vitabu kutoka maktaba yao kutawasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wa Zanzibar.

Sambamba na hayo Rais Karume aliipongeza Afrika Muslim Agency kwa kuendeleza sekta ya elimu na kuweza kuzisaidia kwa nguvu zake zote nchi mbali mbali za Bara la Afrika katika kuimarisha sekta ya elimu.

Pamoja na hayo, Rais Karume aliueleza uongozi huo kuwa Zanzibar inathamini sana mashirikiano hayo yaliopo katika sekta ya elimu na sekta nyengine ambapo imekuwa ikiziunga mkono hapa nchini

Monday, June 7, 2010

TAIFA STARS YA KANDAMIZWA MISUMARI MITANO NA BRAZIL LEO


Haya ndio yaliotokea leo katika uwanja wa Taifa Timu yetu ya taifa imefungwa goli 5 kwa moja mbele ya Mh rais jakaya mrisho kikwete....

SEIF AWAONYA WANAPINGA MARIDHIANO YA KISIASA Z’BAR

Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Seif Sharif Hamad amesema anashangazwa kuona baadhi ya wazanzibari wanakula njama za kuwatenganisha wananchi baada ya kufikiwa maridhiano ya kisiasa.

Akizungumza katika sherehe fupi ya kurejesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia CUF amesema watu hao wanajaribu kuyabeza mafanikio ya maridhiano na kusema lengo lao ni kutaka wazanzibari wahasimiane ili kulinda maslahi yao binafsi.

Hamad amesema mataifa ya nchi wahisani yamepongeza hatua iliyofikiwa na Zanzibar ya kufungua ukurasa mpya wa melewano ambapo nchi hizo zimeahidi kutoa misaada yao na kuwaonya wanaojaribu kuhujumu maridhiano hayo …

Aidha katibu mkuu huyo amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono maridhiano ya kisiasa kwa kushiriki kwa wingi katika kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu kwa kukubali mfumo mpya wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Katibu mkuu wa CUF Hamad anakuwa mwanachama pekee wa CUF kutaka kuteuliwa na chama chake kugombea nafasi ya urai wa Zanzibar.

Mwaka 1995 wanachama wa CUF Mataka Amour Mataka na Suleiman Khamis walijitokeza kuchuana na kiongozi huyo, lakini baadae walijiondoa katika mkutano wa baraza kuu la chama hicho.

CHAMA CHA JAHAZI ASILIA KIMESISITIZA KUANDALIWA KWA KATIBA MPYA YA Z’BAR

Chama cha Jahazi asilia kimesisitiza msimamo wake wa kutaka kuwepo na serikali ya umoja wa kitaifa itakayovishirikisha vyama vyote vya siasa nchini.

Mwenyekiti wa chama hicho Amour Rajab Amour amesema serikali ya aina hiyo itasaidia kuepusha mifarakano ya kisiasa ilinayotokezea mara kwa mara hapa Zanzibar hasa nyakati za uchaguzi wa kitaifa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Amour amesema iko haja ya kuandaliwa katiba mpya ya Zanzibar itakayozingatia matakwa ya mfumo wa vyama vingi na uchaguzi.

Amesema katiba inayotumika hivi sasa ya mwaka 1984 iko katika mfumo wa chama kimoja na kusema matatizo yalitokea katika chaguzi za mwaka 1995, 2000 na 2005 yalisababishwa na katiba hiyo.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi utakaofanyika Octoba mwaka huu Amour amesema chama hicho kina nia ya kumsimamisha mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar, ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia chama hicho.

Chama cha Jahazi asilia kilichosajiliwa Novemba 2004, katika uchaguzi wa mwaka 2005 kilimsimamisha mwenyekiti wake wa zamani Haji Mussa Kitole kuwania kiti cha urais wa Zanzibar na kupata asilimia sufuri nukta nne, nane na kukosa nafasi za uwakilishi, ubunge na udiwani

IRAN IMEAHIDI KUISAIDIA ZANZIBAR

Serikali ya Iran imeahidi kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha sekta za elimu, kilimo na uvuvi.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Dr. Harith Suleiman amesema Zanzibar inayonafasi nzuri ya kuvutia wawekezaji katika sekta hizo, hivyo serikali yake itaongeza nafasi za masomo nchini Iran kwa vijana wa Zanzibar.

Akizungumza na waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha amesema Iran pia itaisaidia Zanzibar kuimarisha kilimo cha umwagiliaji maji na uvuvi wa bahari kuu na hospitali ya kitalii na watu mashughuri.

Nae waziri kiongozi Nahodha amesema upatikanaji wa uemem nchini utasaidia juhudi za serikali za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na wananchi.

WADAU WA SIASA WATAKA UTAFITI WA WANAWAKE KUKOSA NAFASI ZA UONGOZI MAJIMBONI

Siku chache baada ya chama cha wananchi CUF kukosa wagombea wanawake kupitia kura za maoni, wadau wa siasa wametaka kufanyike utafiti ili kubaini chanzo kinachowakwamisha wanawake kukosa nafasi za uongozi majimboni kupitia vyama vya siasa.

Wakizungumza katika mkutano uliojadili ushiriki wa wanawake katika siasa uliofanyika mjini hapa, wamesema matokeo ya utafiti huo yatasaidia kulipatia ufumbuzi tatizo linalosababisha wanawake kutoungwa mkono wakati wa uchaguzi hasa majimboni.

Wadau hao wamesema licha ya wapiga kura wengi ni wanawake, lakini bado wanawake wanaojitokeza kuomba kura za kuwania nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wanakosa kuungwa mkono na wenzao.

Washiriki wengine waliochangia mkutano huo wamesema baadhi ya wanawake wanaopata nafasi za uongozi katika mabaraza ya kutunga sheria wanajisahau kutekeleza majukumu yao kwa wananchi.

Wamesema hali hiyo huenda ikawa chanzo kwa wanawake wanojitokeza kuomba nafasi za uongozi majimboni kupitia vyama vya siasa kukosa kuungwa mkono na wenzao.

Hivi karibuni wagombea wanawake wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia chama cha wananchi CUF wamekataliwa katika kura za maoni ambapo chama hicho kina zaidi ya asilimia 41 wanachama wanawake.

Sunday, June 6, 2010

ZANZIBAR:

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi CCM, Vuai Ali Vuai amesema mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho umechochea kasi ya maendeleo ya wananchi.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2005/2010 serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanikiwa kutekeleza ilani hiyo na kutoa changamoto kwa wananchi kuongeza kasi ya uzalishaji kupitia miradi yao mbali mbali.
Akizunguma katika semina ya makatibu wa wilaya, uenezi na wana CCM wa wilaya za Unguja amesema sekta za maendeleo ya uchumi na kijamii zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuwawezesha wananchi kupambana na umasikini.
Amesema miradi kama vile ya MACEMP, PADEP pamoja na miundo mbinu ya usambazaji wa maji, umeme na utowaji wa mafunzo umewasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi

ZANZIBAR:

Chama cha Jahazi asilia kimesisitiza msimamo wake wa kutaka kuwepo na serikali ya umoja wa kitaifa itakayovishirikisha vyama vyote vya siasa nchini.
Mwenyekiti wa chama hicho Amour Rajab Amour amesema serikali ya aina hiyo itasaidia kuepusha mifarakano ya kisiasa ilinayotokezea mara kwa mara hapa Zanzibar hasa nyakati za uchaguzi wa kitaifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Amour amesema iko haja ya kuandaliwa katiba mpya ya Zanzibar itakayozingatia matakwa ya mfumo wa vyama vingi na uchaguzi.
Amesema katiba inayotumika hivi sasa ya mwaka 1984 iko katika mfumo wa chama kimoja na kusema matatizo yalitokea katika chaguzi za mwaka 1995, 2000 na 2005 yalisababishwa na katiba hiyo.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi utakaofanyika Octoba mwaka huu Amour amesema chama hicho kina nia ya kumsimamisha mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar, ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia chama hicho.
Chama cha Jahazi asilia kilichosajiliwa Novemba 2004, katika uchaguzi wa mwaka 2005 kilimsimamisha mwenyekiti wake wa zamani Haji Mussa Kitole kuwania kiti cha urais wa Zanzibar na kupata asilimia sufuri nukta nne, nane na kukosa nafasi za uwakilishi, ubunge na udiwani

ZANZIBAR:

Serikali ya Iran imeahidi kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha sekta za elimu, kilimo na uvuvi.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Dr. Harith Suleiman amesema Zanzibar inayonafasi nzuri ya kuvutia wawekezaji katika sekta hizo, hivyo serikali yake itaongeza nafasi za masomo nchini Iran kwa vijana wa Zanzibar.
Akizungumza na waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha amesema Iran pia itaisaidia Zanzibar kuimarisha kilimo cha umwagiliaji maji na uvuvi wa bahari kuu na hospitali ya kitalii na watu mashughuri.
Nae waziri kiongozi Nahodha amesema upatikanaji wa uemem nchini utasaidia juhudi za serikali za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na wananchi.

MKOA WA KUSINI UNGUJA:

Mbunge wa jimbo la Uzini Mohammed Seif Khatib amewataka wananchi wa jimbo hilo kutumia raslimali ya ardhi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
Amesema chimbuko la mabadiliko ya binadamu ni kutumia raslimali ya ardhi, kuendeshea shughuli za kilimo, ufugaji na utowaji wa huduma nyingine za kijamii kazi ambazo zinaweza kuwakomboa na umasikini.
Khatib ambae pia ni waziri anaeshughulikia masuala ya muungano ametoa wito huo alipokuwa akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa jumuiya za maendeleo za shehia za Tunduni na Mgenihaji.
Amesema serikali imejitahidi kuweka miundo mbinu ya barabara, maji na umeme ambayo inaweza kumsaidia mwananchi kuleta mabadiliko yake binafsi, familia na taifa kwa ujumla.
Aidha Khatib amesema mafunzo hayo ni chachu kwa wananchi wa vijiji hivyo ili kubuni miradi itakayoleta mbadiliko ya kiuchumi na kijamii katika shehia hizo.
Mafunzo hayo yalioendeshwa kwa awamu tatu tofauti kuanzia April hadi Mei 22 mwaka huu na kufadhiliwa na taasisi ya jumuiya ya kiraia yaliwashirikisha viongozi wa kamati, wajumbe wa kamati tendaji, wahasibu na washika fedha wa jumuiya za maendeleo za vijiji hivyo.

Saturday, June 5, 2010

MSANII MAARUFU WA TANZANIA YUSSUF AHMMED A.K.A BWAN CHUCHU AFRIKI DUNIA


Mamia ya wananchi na wasanii nchini jioni hii wanahudhuria mazishi ya msanii maarufu wa Zanzibar Yusuf Ahmed Alley maarufu bwan’chuchu katika makaburi ya Mwanakwerekwe wilaya ya magharibi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari Marehemu Chuchu amefariki dunia mjini Nairobi, Kenya alikopelekwa kupatiwa matibabu baada ya kuugua kiasi ya mwezi mmoja uliopita.

Mwili wa msanii umerejeshwa mjini hapa ambapo taratibu za mazishi zilifanyika katika mtaa wa Kisima Majongoo na maziko yanafanyika jioni hii katika makaburi ya Mwanakwerekwe wilaya ya magharibi.


Marehemu Chuchu atakumbukwa kwa uhodari wake katika muziki hasa alipounda bendi ya Chuchu Sound iliyotamba kwa vibao vyake na chapuo za mazungumzo kati yake na Omari Mkali yaliyokuwa yakihitimishwa na neno la ‘ee! kwaheri’.

Marehemu chuchu pia alikuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya tamasha la kila mwaka la Sauti za busara na pia alikuwa anamiliki kituo cha redio cha Chuchu Fm kiliopo mjini hapa na studio ya kurekodia muziki.

Marehemu Chuchu aliefariki akiwa na umri wa miaka 51 ameacha mke mmoja ambae kwa sasa yuko nchini Marekani.

Uongozi wa Zenji Fm Radio unatoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu pamoja na

Mungu amlaze mahali pema peponi AAMIN ndugu na jamaa na wafanyakazi wa CHUCHU FM RADIO

SEIF SHARIF HAMAD AWANIA TENA URAIS WA ZANZIBAR

Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Seif Sharif Hamad amechukua fomu ya kuomba kuteliuliwa na chama chake kugombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika tawi la CUF, Mtoni amesema anamatumaini ya kushinda uchaguzi huo kutokana na mazingira mazuri ya kisiasa yaliofikiwa Zanzibar.

Amesema Zanzibar imefungua ukurasa mpya baada ya kufikia maridhiano ya kisiasa ya kusahau tofauti zilizopita na kuweka mbele maslahi ya nchi …………

Hata hivyo katibu mkuu huyo amesema hakuna mwanachama aliezuiliwa kugombea nafasi za urais wa Zanzibar na ile ya muungano ambapo kesho ndio siku ya mwisho ya kurejesha fomu za nafasi hizo.

Maalim Seifa amesema kutokana na kauli ya rais Karume aliyoitoa katika uzinduzi wa umeme kisiwani Pemba kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa tofauti na chaguzi zilizotokea inatoa matumaini kwa chama hicho kushinda katika uchaguzi huo.

Hivyo amewataka viongozi wa vyama vya siasa kushindana kwa hoja wakati wa kampenzi za uchaguzi bila ya kutumia maneno machafu katika majukwaa ili wananchi kutowa ridhaa zao.

Hii ni mara ya nne kwa Malim Seif kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia chama cha CUF tokea kuanza kwa chaguzi za mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1995, lakini bado hajaungwa mkono na wananchi waliowengi.

WALIOSHINDA KURA YA MAONI CUF HUENDA WAKAENGULIWA-SEIF SHARIF

Chama cha wananchi CUF kimewatahadharisha wanachama wake walioshinda katika kura ya maoni kuwania nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wanaweza kuondolewa endapo baraza kuu la chama hicho litaona upo umuhimu wa kufanya hivyo.

Katibu mkuu wa chama hicho Seif Sharif Hamad amesema ingawa baraza kuu litaheshimu maoni ya wanachama lakini, baraza hilo ndio litakalofanya uteuzi wa mwisho.

Hata hivyo amesema kila mwanachama awe mwanamke au mwanamme anayo haki ya kugombea nafasi yoyte katika chama au katika nafasi za uongozi wan chi kupitia

Kauli hiyo ya Hamad imekuja siku chache baaba ya wagombea kadhaa wanawake waliojitokeza kugombea nafasi za ubunge na uwakilishi kukatiliwa katika kura za maoni.

Amesema chama cha CUF kilijitahidi kufanya kampeni za kuwataka wanawake kujitokeza Kwa wingi kugombea nafasi za uongozi , lakini kinachoonekana kwamba wanawake hao hawajiamini.

Amesema wanachama wamefanya uwamuzi juu ya wagombea hao na uwamuzi wao utaheshimiwa, lakini baraza kuu la chama hicho ndilo lenye uwamuzi wa mwisho baada kuchunguzwa kwa makini wagombea hao.

Katika kura ya maoni ya CUF mwaka 2005 mwakilishi wa jimbo la mji Mkongwa Fatma Fereji na mbunge wa jimbo la Chake chake Fatma Magimbi walishinda kura lakini mwaka huu wamekataliwa.

Baraza kuu la CUF linatarajiwa kufanya kikao chake June 25 mwaka huu ili kuchunguza na kupitisha majina yawagombea walioshirika katika kura ya maoni ya chama hicho.

KERO YA WAFANYABIASHARA ZANZIBAR KUTOZWA KODI MARA MBILI YAPATIWA UFUMBUZI-WAZIRI KHATIB

Serikali za Tanzania zimekubaliana kuondoa usumbufu wa wafanyabiashara wa Zanzanzibar kutozwa kodi mara mbili wakati wanaposafirsha bidhaa zao kwenda Tanzania bara.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika kikao cha kamati za kutatua kero muuungano kilichowashirikisha baadhi ya mawaziri wa serikali Mapinduzi Zanzibar na serikali ya muungano wa Tanzania katika hoteli ya Bwawani mapema wiki hii.

Akizungumza na Zenji Fm radio waziri anaeshughulikia masuala ya muungano Mohammed Seif Khatiba amesema chini makubaliano hayo mizigo ya wafanyabiashara itakayokuwa chini ya kiwango cha kulipia kodi afisa wa TRA alieruhusu mzigo huo kupita ndio atakae wajibika.

Amesema kabla ya makubaliano hayo wafanya biashara kutoka Zanzibar walikuwa wakitozwa kodi mara mbili kutokana na mizigo mizigo wanayosafirisha kwenda Tanzania bara kuwa chini ya kiwango cha kulipia kodi………CLIPS…….(SAVED-KHATIB)

Tatizo la wafanyabiashara Zanzibar kutozwa kodi mara mbili ni la muda mrefu na kukwamisha shughuli zao za biashara limefanywa kuwa agenda ya kero za muungano ambalo imepatiwa ufumbuzi.

KARUME AZINDUA UMEME PEMBA

Rasi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amesema huduma ya umeme wa uhakika ulioko kisiwani Pemba utasaidia kufungua milango ya uwekezaji kisiwani humo.

Akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa mradi wa umeme wa uhakika kutoka Tanga hadi Pemba amewahimiza wananchi kuitumia nafasi hiyo kwa kuekeza miradi mbali mbali ya kiuchumi.

Amesema lengo la mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapa fursa wananchi kujendeleza kiuchumi na kusema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuona wananchi hao wanafanikiwa katika sekta ya uwekezaji.

Rais Karume amesema mbali ya umeme huo kusaidia sekta za uchumi, lakini pia utarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile usambazaji wa maji, elimu na huduma nyingine za kijamii….

Aidha rais Karume amewataka wananchi kuyaenzi maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa hivi karibuni katika kujenga umoja wao na kuimarisha amani na utulivu ili uchaguzi mkuu ujao utofautiane na miaka iliyopita.

Amesema wananchi wa Zanzibar wote ni wa moja hivyo ni vyema kujenga mshikamano katika kuiletea maendeleo nchi yao…..

Kwa zaidi ya maiak 40 wananchi wa Pemba wamekuwa wakitegemea huduma ya umeme kwa kutumia majenerata ambayo yakidhi mahitaji.

Mradi huo wa umeme uliogharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 75 umefadhiliwa Norway ambapo serikali ya Mapinguzi imetoa zaidi ya dola milioni 10 na serikali ya muungano imechangia dola milioni tano.

Wednesday, June 2, 2010

MASHA AKIRI ULEGEVU WA ULINZI KATIKA VITUO VYA POLISI NCHINI AMBAKO KWASABABISHA WANANC HI KUCHUKUA SHERIA MIKONONI MWAO

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Laurent Mahsa amekiri kuwepo kwa ulegevu wa ulinzi katika vituo vya Polisi na kulitaka jeshi hilo kuimarisha ulinzi katika vituo vyote vya Polisi nchini .
Amesema hayo jijini Dar es salaam baada ya kuibuka kwa vitendo vya wananchi kujichukulia sheria Mikononi ikiwemo tukuio la hivi karibuni la kuteketezwa kwa kituo cha Polisi cha Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro na Kiela Mkoani Mbeya

WABUNGE NA WAWAKILISHI CUF WAMBWAGA KATIKA KURA ZA MAONI PEMBA

Baadhi ya Wabunge na wawakilishi waliopo madarakani katika majimbo mbali mbali Kisiwani Pemba wameendelea kuangushwa katika kura za maoni katika chama cha wananchi CUF .
Miongoni mwa wabunge ambao wameangusha katika kura hizo ni mbunge wa chakechake Fatma Magib alieyepata kura 417 dhidi ya mpinzani wake Mussa Haji Komba aliyepata kura 974.
Bunge mwengine ni Mbunge wa Jimbo la Chonga Rashid Chai aliepata kura 309 kwa kushindwa na Mohamed Juma Khamis aliyepata kura 414.
Wakati Mbunge wa Ziwani aliepo sasa hakujitokeza katika kinyanganyiro hicho na waliowania nafasi hiyo katika jimbo hilo ni Ahmed Juma Ngwali aliyepata kura 961 na kumshinda Yussuf Sharif aliyepata kura 90.
Kazi hiyo ya upigaji wa kura za maoni ulianza tarehe 21 Mwezi Mey mwaka huu na imemalizika jana katika jimbo la Konde.
Hata hivyo maamuzi ya mwisho ya kupitishwa wagombea wa nafasi hizo yatafanywa na baraza kuu la chama hicho June 15 mwaka huu.

TAASISI 200 IKIWEMO VYUO VIKUU VIWILI HATARINI KUFUTIWA UDHAMINI -SARIBOKO

Wizara ya katiba na sheria nchini imetangaza taasisi 200 ikiwemo vyuo vikuu viwili ambavyo vimo hatarini kufutiwa udhamini kutokana na kuchelewa kuwasilisha taarifa za udhamini.
Kaimu msimamizi mkuu wa udhamini kutoka wakala wa udhamini na ufilisi na usajili RITA Philip Sariboko amezitaja taasisi hizo ni pamoja na Chuo kikuu cha Mtakatifu Agostino cha Jijini Mwanza na Millenium cha Jijini Dar es salaam ambapo na taaisis nyengine 198 zimekiuka sheria ya unganishi wa wadhamini toleo la mwaka 2002 na kushindwa kutoa taarifa za mabadiliko katika taasisi hizo .
Katika taarifa yake Sariboko amezipa siku hizo siku 30 kuanzia Juzi taasisi hizo ziwezimetoa sababu za kutofutiwa udhamini

BAADHI YA KERO ZA MUUNGANO ZAPATIWA UFUMBUZI NA SERIKALI YA MUUNGANO NA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Kamati ya Pamoja ya serikali ya Muungano wwa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar imetia saini hati ya makubaliano kuhusu kero za muungano zilizopatiwa ufumbuzi ikiwemo ile ya utekelezaji ya sheria za haki ya binaadam iliyokuwa haifanyi kazi Zanzibar na kuwekwa katika kero za Muungano .
Hati nyengine za kero za Muungano zilizotiwa saini ni utekelezaji wa sheria ya uvuvi katika eneo la bahari kuu ambayo pia ilikuwa katika kero za Muungano.
Kwa mujibu wa hati ya makubaliano utekelezaji wa masuala hayo umekamilika na si kero tena katika utekelezaji wa shughuli hizo na hivyo inapaswa kuondolewa katika ajenda za kamati hiyo ya pamoja

WALIOVUNJIWA NYUMBA KWARARA ZANZIBAR WALALAMIKIA SERIKALI YA WILAYA KUWAITA WAVAMIZI.

Wananchi waliovunjiwa nyumba zao maeneo ya kwarara wamesikitishwa na kitendo cha kuitwa wavamizi katika maeneo hayo na kutakiwa kuacha kuendela na ujezi wa aina yeyote katika eneo hilo .
Akizungumza na Zenji Fm Radio kwa niaba ya wenziwe waliovunjiwa nyumba zao katika eneo hilo Salum Seif amesema wameitwa katika afisi ya mkuu wa wilaya ya magharib nakuambiwa kuwa niwavamizi hali ambayo imewasikitisha sana.
Wamesema kutokana na kauli hiyo ambayo haijawaridhisha wanamuomba Rais wa Zanzibar kuingilia kati suala hilo ili waweze kupata haki zao…

WAHAMIAJI 21 HARAMU WATIWA MBARONI NA KMKM TUMBATU ZANZIBAR

Jumla ya wahamiaji haramu 21 wamekamatwa baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria na Idara ya uhamiaji Zanzibar kwa kushirikiana na Kikosi cha Kuzuwia Magendo KMKM katika Maeneo ya Tumbatu Unguja.
Akizungumza na zenji fm Radio Afisa Uhusiano wa Idara hiyo Muhsin Abdalla Muhsin amekiri kukamatwa kwa watu hao wakiwa ni raia wa Kenya ,Somali na Ethiopia ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.
Amesema wamepata taarifa ya kukamatwa kwa watu hao siku ya Jumamosi na kikosi cha KMKM kwa msaada wa wananchi kutoa taarifa ya uwepo kwa watu hao .
Hata hivyo watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa zaidi ambapo wanagundua kuwepo kwa wageni ambao wanawatilia mashaka ili hatua za kiusalama ziweze kuchukuliwa.

KESI INAYOMKABILI MWENYEKITI WA DP YAENDELEA KUSIKILIZWA USHAHIDI

Mahakama ya hakimu mkaazi jijini Dar es salaam leo imesikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili mwenyekiti wa chama cha DP mchungaji Kristopha Mtikila anaetuhumiwa kumkashifu rais Jakaya Kikwete mwaka 2007.
Katika ushahidi uliotolewa leo mahakamani hapo mkanda wa video uliokuwa na hutuba ya mtikila Mwezi Novemba mwaka 2007 eneo la mchikichini na kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi yanayomkashifu Rais Kikwete .
Mara baada ya kuangaliwa kwa mkanda huo mahakamani hapo yaligunduliwa maneno ya uchochezi na Chuki zilizotolewa na Mtikila miongoni mwa maneno hayo ni kusema kuwa hawezi kuvumilia nchi kuongozwa na Muhuni.
Katika amaelezo yaliyotolewa na SP Muela ambae ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ambapo mtikila alieleza kwamba yeye ni Mchungaji ,mwenyekiti wa DP na Raia wa Tanganyika maelezo ambayo wakili wa Mtikila alieleza kuwa Mteja wake maelezo hayo anayapinga na wala hakuyasema wala kuyaandika.
Mashahidi kadha awakiwemo waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali miongoni mwa mashahidi 10 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.

ZANZIBAR:

Mkuu wa mkoa wa mjini Magharib Abdalah Mwinyi Khamisi amewataka maafisa na waratibu wa uandikishaji wa katika Daftari la wapiga kura linalosimamiwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC kusimamia vyema kazi hiyo katika kutoa haki kwa kila mwenyesifa ya kuandikishwa katika daftari.
Akizungumza katika mafunzo ya maafisa wa uandikishaji wa mkoa na ngazi ya majimbo yaliyofanyika katika Skuli ya Mbadala Rahaleo mjini Zanzibar.
Amewataka watendaji hao kutekeleza majukumu yao ya kitaifa kwa kutumia uzowefu watakao upata katika kusimamia vyema na kufanikisha zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi.
Aidha amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuelimisha mawakala wao ili kufuata vyema taratibu za uandikishaji katika daftari la wapiga kura la NEC kwa lengo la kufanyika katika mazingira bora .
Nae Naibu Katibu wa uchaguzi wa tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania NEC Cotrida Komba amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu upande wa Zanzibar Litaanza June 14 hadi 16 mwaka huu.
Aidha amewataka watanzania wote wenye sifa ya kundikishwa katika Daftari hilo ambao hawajaandikishwa na tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kujitokeza kujiandikisha kwa mujibu wa taratibu ziliopo.

TUME YA UCHAGUZI ZNZ

Tume ya uchaguzi Zanzibar inakusudia kuwachukulia hatua za kisheria jumla ya wananchi 266 kwa madai ya kujiandikisha mara mbili katika Daftari la kudumu la wapiga kura.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo Salum Kassim ambapo amesema majina ya watu hao yatapelekwa katika afisi ya mkurigenzi wa Mashtaka Zanzibar ili kufikishwa mahakamani.
Akizungumza katika warsha ya waandishi wa habari juu ya masuala ya uchaguzi amesema uchaguzi wa mwaka 2005 watu wengi walijiandikisha mara mbili na wamepandikizwa na vyama vya siasa.
Hata hivyo hakutaja watu waliopandikizwa mwa 2005 lakini amesema tume mwaka huu imedhibiti wimbi hilo la upandikizaji.
Warsha hiyo kwa waandishi wa habari imeandaliwa na chama cha waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar WAHAMAZA na Tume ya uchaguzi Zanzibar kwa kushirikiana na shirika la maendeleo ulimwenguni UNDP kupitia mfuko wa kusaidia uchaguzi Zanzibar .

Tuesday, June 1, 2010

SMZ KUSHAURIWA KUACHANA NA KODI ZA SIGARA


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kutafuta njia mbadala za kuingiza mapato ili kuondokana na mapato yatokanayo na kodi za makampuni ya siraga kutokana kuhatarishs afya za watumiaji.

Akizungumza na Zenji fm radio juu ya siku ya kukataza uvutaji wa sigara duniani afisa wa elimu wa kitengo cha dawa za kulevya Zanzibar Dr. Kassi Ali Simai amesema hasara inayotokana na sumu ya sigara kwa afya ya mwadamu ni kubwa ikilinganishwa na mapato hayo.

Amefahamisha licha ya serikali kukusanya mapato mengi kutoka makampuni ya sigara, lakini moshi wake una zaidi ya chemical 400 zinazohatarisha afya za watumiaji hivyo ni vyema kufikiria njia nyingine mbadala ya ukusanyaji wa mapato.

Dr. Simai amesema vijana wengi wamekuwa wakiathirika na moshi wa sigara kwa kuugua homa ya ini na saratani

Katika kuadhimisha siku ya uvutaji wa sigara duniani shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, limevilaumu viwanda vya sigara kwa kuwahamasisha wanawake katika nchi masikini kuvuta sigara.

Mtaalamu wa shirika hilo la WHO, Douglas Bettcher amesema, utafiti umeonesha idadi ya wanawake na vijana wanaovuta sigara katika nchi masikini imekuwa ikiongezeka.

KARUME AMETOWA WITO WA KUFANYIWA MAREKEBISHO MUUNDO WA SHIRIKA LA IMF

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume ametowa wito wa kuwepo mabadiliko katika taasisi za kifedha za Kimataifa ili kuweza kutoa nafasi sawa katika mataifa yote makubwa na madogo ulimwenguni.

Rais Karume ametoa wito huo katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kiuchumi Duniani (WEF) unaofanyika mjini Doha, Qatar.

Katika mkutano huo Rais Karume alisisitiza kuwa maendeleo ya uhakika hayawezi kupatikana bila ya kuwepo mageuzi ya kifedha ya kimataifa hasa kwa kzingatia kuwa taasisi hizo ziliudwa wakati ambao kulikuwa na nchi chache zenya uwezo wa kiuchumi na kiutawala duniani.

Alieleza kuwa wakati huo taasisi hizo ziliundwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya nchi hizo chache.

“Taasisi hizo ziliudwa ili kukidhi mahitaji hayo lakinisasa wadau ambao ni sisi sote tuko wengi na ni lazima kupatikana usawa wa fursa ili kuweza kushiriki kikamilifu”,alisema DK. Karume.

Aidha, Rais Karume alizungumia umuhimu wa elimu katika kuleta maendeleo ya binaadamu na kusisitiza haja ya kuiimarisha sekta hiyo.“Elimu ndio ufunguo wa maisha katika maendeleo ya binaadamu” alieleza Rais Karume.

Rais Karume alisisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano wa kimataifa katika maendeleo ya elimu.

Katika mkutano huo, Rais Karume alkuwa ni miongoni mwa wazungumzaji wakuu katika ufunguzi wa mkutano huo.

Miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na Amir wa Qatar Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani walikuwa ni mrithi wa Mfalme wa Norway Prince Haakon, Mke wa Mfalme wa Jordan Queen Rania, Waziri wa Maendeleo wa Singapore na wengineo.

Wazungumzaji wote wakuu katika mkutano huo walisisitiza haj ya kuimarisha sekta ya elimu kwani ndio mkombozi katika kuimarisha sekta zote za maendeleo na ukuzaji wa uchumi.

Amir wa Qatar Sheikh Hamad akifungua mkutano huo mkubwa wa kiuchumi duniani alisisitiza ushirikiano wa kimataifa na kubuni mikakati itakayosaidia katika kupambana kwa pamoja na matatizo ya kiuchumi duniani.

Aidha, nae mke wa Mfalme waa Jordan Queen Rania alizungumzia umuhimu wa maendeleo ya vijana hasa katika maendeleo ya elimu.

Queen Rania alieleza kuwa kukosekana kwa elmu kunasababisha ukandamizaji wa vijana na watoto sanjari na kukosa fursa za kujiimarisha kimaendeleo.

Ufunguzi wa mkutano huo uliendeshwa na Profesa Claus Schwab ambaye ndie Mwenyekiti Mtendaji wa WEF.

Mkutano huo ulitanguliwa na mikutao midogo midogo ya majadiliano juu ya mada mbali mbali zikiwemo elimu, afya, maendeleo ya ushirikiano wa kimataifa, uimarishaji wa uchumi na fedha, mazingira, usalama na nyenginezo ambayo iliwashirikisha viongozi mbali mbali kutoka sekta tofauti za serikali na zile za kibinafsi wakiwemo mawaziri,wataalamu na wakuu wa taasisi tofauti ambapo Tanzania pia imewakilishwa na baadhi ya Mawaziri waliomo katika nyanja hizo

VITENDO VYA UHARAMIA VINAWEZA KUATHIRI UCHUMI WA Z’BAR-DR. MWINYIHAJI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwepo kwa vitendo vya uharamia kati ya visiwa vya Unguja na Pemba vinavyoripotiwa katika vyombo vya habari kunaweza kuathiri uchumi wa Zanzibar. Akizungumza na zenji fm radio juu ya athari za vitendo hivyo kwa uchumi wa Zanzibar waziri anaeshughulikia masuala ya fedha na uchumi Dr. Mwinyihaji Makame amesema licha ya kutopata uthibitisho wa vitendo hivyo, lakini Zanzibar ni sawa na nchi nyingine ziliomo katika ukanda wa bahari ya Hindi inaweza kuathirika kiuchumi kutokana na uharamia huo. Amesema iwapo meli za mizigo zinazotaka kuingia katika eneo la Afrika ya mashariki zinatishiwa na maharamia wa kisomali bila shaka hali ya uchumi wa Zanzibar itakuwa mbaya. Hata hivyo Dr. Makame amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kufanya doria za kuwasaka maharamia hao walioripotiwa kuwepo katika kisiwa cha Pemba. …CLIPS…(SAVED-MWINYIHAJI) Kazi ya kuwasaka maharamia hao wa kisomali bado zinaendelea kwa ushirikiano wa jeshi la polisi, vikosi vya SMZ pamoja na jeshi la wananchi Tanzania JWTZ. Akizungumza na Zenji Fm Radio juu ya msako huo kamanda wa kikosi cha kuzuia magendo KMKM kisiwani Pemba amesema kuwa kazi inaendelea vizuri na hadi sasa wananchi wanatoa ushirikiano mzuri……CLIPS….(SAVED-KMKM) Msako huo umekuja siku moja baada ya kuripotiwa watu wanaodaiwa maharamia waliotaka kuiteka nyara meli moja katika bahari ya Hindi upande wa Tanzania kukimbilia kisiwani Pemba. Maharamia hao wamekimbilia Pemba baada ya kushambuliwa na majeshi ya jumuiya ya umoja wa ulaya wanaofanya doria katika pwani ya Afrika ya mashariki wakitaka kuiteka meli kati kati ya bahari ya visiwa vya Unguja na Pemba

VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA TANZANIA WAWASAKA MAHARAMIA WA KISOMALI WALIOKIMBILIA PEMBA

Vikosi vya ulinzi na usalama vimeripotiwa kuweko katika msako mkali wa kuwatafuta maharamia wa kisomali wanaodaiwa kukimbilia kisiwani Pemba baada ya kushindwa kuiteka meli katika bahari kuu ya Tanzania.

Kamanda wa polisi wa mkoa kusini Pemba Hassan Nassir amesema msako huo unavishirikisha vikosi vya SMZ na wanajeshi wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ.

Amesema taarifa za msako huo zitatolewa hapa baadae

Msako huo umekuja siku moja baada ya kuripotiwa watu wanaodaiwa maharamia waliotaka kuiteka nyara meli moja katika bahari ya Hindi upande wa Tanzania kukimbilia kisiwani Pemba.

Maharamia hao wamekimbilia Pemba baada ya kushambuliwa na majeshi ya jumuiya ya umoja wa ulaya wanaofanya doria katika pwani ya Afrika ya mashariki wakitaka kuiteka meli kati kati ya bahari ya visiwa vya Unguja na Pemba

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU TUNGUU ZAIDI 300 WAMEFUKUZWA KWA KUSHINDWA KULIPA ADA

KOA WA KUSINI UNGUJA: Wanafunzi wa chuo kikuu cha Zanzibar, Tunguu mwaka wa pili, wameulalamikia uongozi wa chuo hicho kuwafukuza baada ya kukosa kusajiliwa kwa kile kilichoelezwa kushindwa kukamilisha malipo ya ada. Akizungumza na Zenji Fm radio mmoja wa wanafunzi hao amedai chuo hicho kimeongeza ada ya masomo kinyume na mkataba wao wa zamani hivyo wameshindwa kulipa ada hiyo na kulazimika kufukuzwa. Amedai kutokana na kufukuzwa chuo kinyume na sheria wanatarajia kufungua kesi mahakamani wiki ijayo kutokana na kufukuzwa kwa zaidi ya wanafunzi Hata hivyo uongozi wa chuo hicho haukuweza kupatikana kuelezea juu ya madai hayo ya wanafunzi kufukuzwa chuoni hapo

ANGOZA KUFANYA TAMASHA LA JUMUIYA ZA KIRAIA ZANZIBAR

ZANZIBAR: Jumuiya ya taasisi za kiraia ANGOZA imeandaa tamasha la siku mbili la maonyesho la asasi za kiraia za Zanzibar litakaloanza leo katika viwanja vya hoteli ya Bwawani. Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa Jumuiya hiyo John Ulanga amesema lengo la tamasha hilo litakalofuatiwa na mijadala ni kuzijengea uwezo taasisi za kiraia. Amesema pamoja na kuandaliwa kwa matamasha jumuiya hiyo pia imekuwa ikitoa ruzuku kwa wananchama wake ili kuona zinatoa huduma nzuri kwa wananchi. Akizungumzia masuala ya uchaguzi na taasisi za kiraia Ulango amesema taasisi hizo pia zitahamasishwa juu ya majukumu yao katika shughuli za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu. Jumuia ya taasisisi za kiraia Tanzania hii ni mara yake ya kwanza kuendesha tamasha kwa wananchama wake hapa Zanzibar kati ya matamasha saba iliyoyafanya katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara. Hata hivyo Jumuiya hiyo imekuwa ikiwashirikisha wanachama wake katika maonyesho ya kila mwaka yanayofanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi yakiwa na lengo la kusogeza huduma zao zaidi kwa wananchi. 18

MAHARAMIA WA KISOMALI WAENDESHA SHUGHULI ZAO KATIKA BAHARI KUU YA ZANZIBAR

PEMBA Watu tisa wanaodaiwa maharamia waliotaka kuishambulia meli ya Namtuna katika eneo la kati kati ya kisiwa cha Unguja na Pemba wamefukuzwa na halikopta ya askari wa umoa wa Ulaya na inadaiwa maharamia hao wamekimbilia Pemba. Askari hao waliokuwa doria katika helikopta hiyo ya umoja wa Ulaya wamesema tukio hilo limekuja siku tatu tangu kutokea kwa tukio jingine katika kisiwa cha Sheli sheli. Kiongozi wa opereseheni wa umoja huo unaofanya doria katika pwani ya Afrika ya Mashariki amesema wamepigiwa simu kuhusiana na kuwepo kwa tukio hilo kati kati ya visiwa vya Pemba na Unguja na hivyo kutuma helikopta hiyo na hatimae kuikoa meli hiyo na maharamia hao kukimbilia Pemba. Amesema maharamia hao wameshindwa kuwafuatilia baada ya kuingia katika eneo la Pemba kutokana na sheria haziwapi mamlaka ya kuingi katika pwani ya Tanzania.

Akizungumzia tukio hilo mwana sheria mkuu wa serikali jaji Fred Tungelema amesema wakati umefika kwa serikali ya Tanzania kuweka mpango wa kuliwezesha jeshi kulinda maeneo yote ikiwemo bahari kuu…..CLIPS……(SAVED-MAHARAMIA) Kamanda wa polisi wa mkoa wa kusini Pemba Hassan Nassir amesema tukio hilo bado halijathibitishwa na kusema maharamia hao kukimbilia kisiwani humo ni uvumi. Hivi karibuni mkurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar Mustafa Abudo Jumbe amesema tatizo la maharamia katika pwani ya Afrika ya Mashariki limesababisha wenye meli kupandisha gharama za usafirishaji wa mizigo. Akizungumza katika mkutano uliojadili ushiriki wa Zanzibar katika soko la pamoja la Afrika Mashariki amesema hali hiyo inaweza kudhorotosha shughuli za bandarini na kuongezeka kwa bei za bidhaa

SUALA LA MAFUTA NA GESI ASILIA LISIHUSISHWE KISIASA-NORWAY

Serikali ya Norway imesema suala la uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar lisichukuliwe kwa mtazamo wa kisiasa, kwa vile linahitaji kuekewa sera na sheria zitakazotoa maslahi kwa wananchi.

Mtaalamu wa nishati ya mafuta kutoka Norway Al-Kassim Farouk amesema inawezekana Zanzibar kuwa na hazina kubwa ya mafuta na gesi asilia, hivyo ni vyema kuanza kuzifanyia marekebisho sheria na sera zake na kulihusisha suala hilo ndani ya katiba.

Farouk amesema hayo katika semina ya utawala bora wa masuala ya mafuta na gesi asila iliyowahusisha baadhi ya mawaziri na maafisa wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika hoteli Zanzibar Beach Resort.

Amesema uchimbaji wa nishati ya unahitaji mtaji mkubwa na wataalamu wa kutosha kwa wenye makampuni, hivyo ni lazima kuwepo na sera zitazo vutia makampuni ya kigeni kuwekeza katika sekta hiyo.

Hata hivyo ameishauri serikali kuwa makini na uingiaji wa mikataba na makampuni ya mafuta ili kuona wananchi wananufaisha pamoja na kuepusha uharibifu wa mazingira.

Nae waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema semina hiyo ni mwendelezo wa kuwandaa viongozi wa serikali kuwa na maamuzi katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Aidha amesema serikali itaendelea kuwashirikisha wataalamu wa ndani na nje ya nchi ili utafutaji na uchimbaji wa nishati hiyo usije ukaleta athari ya uharibifu wa mazingira kama ule uliotokea Marekani hivi karibuni.

Mafuta na gesi asilia ni miongoni mwa mambo ya muungano, lakini serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia baraza la wawakilishi na baraza la mapinduzi imemaua suala hilo kulishughulikia peke yake.