I made this widget at MyFlashFetish.com.

Saturday, June 19, 2010

WALIOKOSA KUJIANDIKISHA WASTAHAMILI-HAMZA

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka watu waliokosa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura wastahamili hadi pale tume ya uchaguzi itakapofanya usajili kwa ajili ya chaguzi nyingine. Waziri wa nchi afisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma amesema, hivi sasa tume ya uchaguzi haina muda tena wa kurudia kazi za uandikishaji baada ya kumalizika wamu tatu tofauti za usajili.

Akijibu maswali katika kikao cha baraza la wawakilishi Juma amesema tume imefanikiwa kuandikisha zaidi ya asilimia 80 idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na nchi zilizoendelea

Aidha waziri Juma amesema idadi ya wapiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2010 ni ndogo ikilinganishwa na mwaka 2005 inatokana na hiari mtu mwenyewe kujiandikisha au la kutumia teknolojia inayozuwia watu kujiandikisha zaidi ya mara moja.

Hata hivyo amesema watu waliobainika kujiandikishwa mara mbili, watapata haki ya kupiga kura, lakini watafikishwa mahakamani kutokana na kukiuka taratibu za uandikishaji……

Tume ya uchaguzi Zanzibar imeandikisha wapiga kura laki nne, 8,401 katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu wakati idadi ya watu waliopata vitambulisho vya ukaazi ni zaidi ya laki tano

No comments:

Post a Comment