I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, June 7, 2010

WADAU WA SIASA WATAKA UTAFITI WA WANAWAKE KUKOSA NAFASI ZA UONGOZI MAJIMBONI

Siku chache baada ya chama cha wananchi CUF kukosa wagombea wanawake kupitia kura za maoni, wadau wa siasa wametaka kufanyike utafiti ili kubaini chanzo kinachowakwamisha wanawake kukosa nafasi za uongozi majimboni kupitia vyama vya siasa.

Wakizungumza katika mkutano uliojadili ushiriki wa wanawake katika siasa uliofanyika mjini hapa, wamesema matokeo ya utafiti huo yatasaidia kulipatia ufumbuzi tatizo linalosababisha wanawake kutoungwa mkono wakati wa uchaguzi hasa majimboni.

Wadau hao wamesema licha ya wapiga kura wengi ni wanawake, lakini bado wanawake wanaojitokeza kuomba kura za kuwania nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wanakosa kuungwa mkono na wenzao.

Washiriki wengine waliochangia mkutano huo wamesema baadhi ya wanawake wanaopata nafasi za uongozi katika mabaraza ya kutunga sheria wanajisahau kutekeleza majukumu yao kwa wananchi.

Wamesema hali hiyo huenda ikawa chanzo kwa wanawake wanojitokeza kuomba nafasi za uongozi majimboni kupitia vyama vya siasa kukosa kuungwa mkono na wenzao.

Hivi karibuni wagombea wanawake wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia chama cha wananchi CUF wamekataliwa katika kura za maoni ambapo chama hicho kina zaidi ya asilimia 41 wanachama wanawake.

No comments:

Post a Comment