I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, June 1, 2010

ANGOZA KUFANYA TAMASHA LA JUMUIYA ZA KIRAIA ZANZIBAR

ZANZIBAR: Jumuiya ya taasisi za kiraia ANGOZA imeandaa tamasha la siku mbili la maonyesho la asasi za kiraia za Zanzibar litakaloanza leo katika viwanja vya hoteli ya Bwawani. Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa Jumuiya hiyo John Ulanga amesema lengo la tamasha hilo litakalofuatiwa na mijadala ni kuzijengea uwezo taasisi za kiraia. Amesema pamoja na kuandaliwa kwa matamasha jumuiya hiyo pia imekuwa ikitoa ruzuku kwa wananchama wake ili kuona zinatoa huduma nzuri kwa wananchi. Akizungumzia masuala ya uchaguzi na taasisi za kiraia Ulango amesema taasisi hizo pia zitahamasishwa juu ya majukumu yao katika shughuli za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu. Jumuia ya taasisisi za kiraia Tanzania hii ni mara yake ya kwanza kuendesha tamasha kwa wananchama wake hapa Zanzibar kati ya matamasha saba iliyoyafanya katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara. Hata hivyo Jumuiya hiyo imekuwa ikiwashirikisha wanachama wake katika maonyesho ya kila mwaka yanayofanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi yakiwa na lengo la kusogeza huduma zao zaidi kwa wananchi. 18

No comments:

Post a Comment