I made this widget at MyFlashFetish.com.

Saturday, June 19, 2010

CCM ZANZIBAR WAJITOKEZA KUWANIA URAIS 2010

Wanachama sita wa chama cha Mapinduzi CCM wamejitokeza kutaka kuwania kiti cha urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Wanachama hao waliojitokeza ni makamo wa rais Dr. Ali Mohammed Shein, waziri kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha na waziri kiongozi wa zamani Dr. Mohammed Gharib Bilal.

Wengine ni naibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna, balozi Ali Abeid Karume na Hamad Bakar Mshindo.

Akiwasilisha majina hayo kwa wandishi wa habari katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Vuai Ali Vuai amesema wanachama hao watachukua fomu siku ya Jumatatu na kusema shughuli hiyo haitakuwa na sherehe.

Amesema fomu za kuwania nafasi hiyo zitaendelea kutolewa kuanzia tarehe 21 mwezi huu hadi Julai mosi kwa wananchama wengine wanaotaka kuwania nafasi hiyo kupitia CCM na kurejesha ndani ya kipindi hicho.

Vuai amesema wanachama hao watalipia fomu hiyo shilingi milioni moja na mwisho wa kurejesha fomu hiyo Juali mosi saa 10.00 jioni ikiwa na wadhamini 250 kutoka mikoa yote ya Zanzibar.

Amesema afisi bado inaendelea kuwakaribisha wanachama wengine watakaokuwa tayari kuchukua fomu za kuwania urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuwania nafasi hiyo akiwemo

Ali Juma Shamhuna

naibu waziri wa Afrika mashariki Mohamed Aboud, waziri wa muungano Mohammed Seif Khatib na waziri wa Elimu Haroun Ali Suleiman bado hawajajitokeza hadharani kutangaza nia zao za kuwania nafasi hiyo.

Waziri kiongozi wa zamani Dr. Gharib hii ni mara yake ya tatu kukiomba chama chake kumteuwe kuwania urais wa Zanzibar ambapo mwaka 2005 aliombwa kujiondoa ili kumwachia rais Karume aendelee na kipindi cha pili cha miaka mitano kinachotarajiwa kumalizika Octoba mwaka huu

No comments:

Post a Comment