I made this widget at MyFlashFetish.com.

Saturday, June 5, 2010

SEIF SHARIF HAMAD AWANIA TENA URAIS WA ZANZIBAR

Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Seif Sharif Hamad amechukua fomu ya kuomba kuteliuliwa na chama chake kugombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika tawi la CUF, Mtoni amesema anamatumaini ya kushinda uchaguzi huo kutokana na mazingira mazuri ya kisiasa yaliofikiwa Zanzibar.

Amesema Zanzibar imefungua ukurasa mpya baada ya kufikia maridhiano ya kisiasa ya kusahau tofauti zilizopita na kuweka mbele maslahi ya nchi …………

Hata hivyo katibu mkuu huyo amesema hakuna mwanachama aliezuiliwa kugombea nafasi za urais wa Zanzibar na ile ya muungano ambapo kesho ndio siku ya mwisho ya kurejesha fomu za nafasi hizo.

Maalim Seifa amesema kutokana na kauli ya rais Karume aliyoitoa katika uzinduzi wa umeme kisiwani Pemba kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa tofauti na chaguzi zilizotokea inatoa matumaini kwa chama hicho kushinda katika uchaguzi huo.

Hivyo amewataka viongozi wa vyama vya siasa kushindana kwa hoja wakati wa kampenzi za uchaguzi bila ya kutumia maneno machafu katika majukwaa ili wananchi kutowa ridhaa zao.

Hii ni mara ya nne kwa Malim Seif kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia chama cha CUF tokea kuanza kwa chaguzi za mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1995, lakini bado hajaungwa mkono na wananchi waliowengi.

No comments:

Post a Comment