I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, June 1, 2010

KARUME AMETOWA WITO WA KUFANYIWA MAREKEBISHO MUUNDO WA SHIRIKA LA IMF

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume ametowa wito wa kuwepo mabadiliko katika taasisi za kifedha za Kimataifa ili kuweza kutoa nafasi sawa katika mataifa yote makubwa na madogo ulimwenguni.

Rais Karume ametoa wito huo katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kiuchumi Duniani (WEF) unaofanyika mjini Doha, Qatar.

Katika mkutano huo Rais Karume alisisitiza kuwa maendeleo ya uhakika hayawezi kupatikana bila ya kuwepo mageuzi ya kifedha ya kimataifa hasa kwa kzingatia kuwa taasisi hizo ziliudwa wakati ambao kulikuwa na nchi chache zenya uwezo wa kiuchumi na kiutawala duniani.

Alieleza kuwa wakati huo taasisi hizo ziliundwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya nchi hizo chache.

“Taasisi hizo ziliudwa ili kukidhi mahitaji hayo lakinisasa wadau ambao ni sisi sote tuko wengi na ni lazima kupatikana usawa wa fursa ili kuweza kushiriki kikamilifu”,alisema DK. Karume.

Aidha, Rais Karume alizungumia umuhimu wa elimu katika kuleta maendeleo ya binaadamu na kusisitiza haja ya kuiimarisha sekta hiyo.“Elimu ndio ufunguo wa maisha katika maendeleo ya binaadamu” alieleza Rais Karume.

Rais Karume alisisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano wa kimataifa katika maendeleo ya elimu.

Katika mkutano huo, Rais Karume alkuwa ni miongoni mwa wazungumzaji wakuu katika ufunguzi wa mkutano huo.

Miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na Amir wa Qatar Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani walikuwa ni mrithi wa Mfalme wa Norway Prince Haakon, Mke wa Mfalme wa Jordan Queen Rania, Waziri wa Maendeleo wa Singapore na wengineo.

Wazungumzaji wote wakuu katika mkutano huo walisisitiza haj ya kuimarisha sekta ya elimu kwani ndio mkombozi katika kuimarisha sekta zote za maendeleo na ukuzaji wa uchumi.

Amir wa Qatar Sheikh Hamad akifungua mkutano huo mkubwa wa kiuchumi duniani alisisitiza ushirikiano wa kimataifa na kubuni mikakati itakayosaidia katika kupambana kwa pamoja na matatizo ya kiuchumi duniani.

Aidha, nae mke wa Mfalme waa Jordan Queen Rania alizungumzia umuhimu wa maendeleo ya vijana hasa katika maendeleo ya elimu.

Queen Rania alieleza kuwa kukosekana kwa elmu kunasababisha ukandamizaji wa vijana na watoto sanjari na kukosa fursa za kujiimarisha kimaendeleo.

Ufunguzi wa mkutano huo uliendeshwa na Profesa Claus Schwab ambaye ndie Mwenyekiti Mtendaji wa WEF.

Mkutano huo ulitanguliwa na mikutao midogo midogo ya majadiliano juu ya mada mbali mbali zikiwemo elimu, afya, maendeleo ya ushirikiano wa kimataifa, uimarishaji wa uchumi na fedha, mazingira, usalama na nyenginezo ambayo iliwashirikisha viongozi mbali mbali kutoka sekta tofauti za serikali na zile za kibinafsi wakiwemo mawaziri,wataalamu na wakuu wa taasisi tofauti ambapo Tanzania pia imewakilishwa na baadhi ya Mawaziri waliomo katika nyanja hizo

No comments:

Post a Comment