I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, June 16, 2010

VIJANA CHAGUWENI VIONGOZI WATAKAOMALIZA UMASIKINI ZANZIBAR-SHAMHUNA

aibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna amewataka vijana kuwasaidia wazanzibari wenzao katika kumpata kiongozi atakaeweza kupambana na umasikini na kutatua tatizo la ajira linalowakabili hivi sasa.

Akizungumza katika mafunzo ya elimu ya demokrasi huko Eacrotanal mjini hapa amesema Zanzibar bado inakabiliwa na umasikini unaosabisha ukosefu wa ajira na mfumko wa bei za bidhaa, hivyo ni vyema kwa vijana kuwa makini wakati wanapofanya maamuzi yao katika uchaguzi utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Shamhuna ambae pia ni waziri wa habari utamaduni na michezo pia amewataka vijana kujiepusha na siasa zinazolenga kubomowa umoja wa Zanzibar kwa jiepusha na ushawishi wa wanasiasa wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi.

Amesema vijana wengi wamekuwa wakijitumibikiza katika siasa chafu kutokana na kukosa elimu ya demokrasia, hivyo amesema serikali itaendelea kuunga mkono taasisi zinazoendelea kutoa elimu hiyo ikiwemo REDET.

Nae mwakilishi kutoka ubalozi wa Norway amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha elimu ya demokrasia nchini.

Amesema licha ya Zanzibar kuingia katika maridhiano ya kisiasa ambayo yamepongezwa na nchi nyingi duniani, lakini inahitaji kuendeleza maridhiano hayo ili kuwa na demokrasia ya kweli.

Mafunzo hayo ya muhula wa 21 yanayoendeshwa na taasisi ya chuo kikuu cha Dar es Salaam REDET yanawashirikisha vijana 50 kutoka jumuia za kiraia za Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment