Kambi ya upinzani bungeni imeomba kupatiwa mkataba wa asili wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ambao unaweza kuyapatia ufumbuzi baadhi ya matatizo yaliomo kwenye muungano huo.
Akizungumza na Zenji Fm radio msemaji wa kambi hiyo katika mambo ya muungano Riziki Omar Juma amesema serikali bado inashikilia mkataba huo na hauwekwi wazi kwa wananchi.
Amesema mkataba huo tayari umeshadaiwa ndani ya bunge na serikali kuahidi kwamba mbunge yoyote anaweza kuuona, lakini hadi sasa bado mkataba huo umekuwa siri.
Riziki amesema lengo la kutaka kuonekana mkataba huo ni kutaka kuufanyia marekebisho kama utaonekana kuwa na kasoro ili kila upande unufaike na maslahi ya muungano…..
Akizungumza na Zenji Fm radio juu ya madai hayo waziri wa muungano Mohammed Seif Khatib amesema mikataba hiyo iko ikulu ya rais mjini Zanzibar na ikulu ya rais wa muungano mjini Dar es Salaam.
Hata hivyo amesema hati hizo zinakuwa na umuhimu pale sheria na katiba hazijaundwa na baada ya vitu hivyo kuwepo mikataba hiyo haina umuhimu sana kama inavyodaiwa…
Hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya kikundi cha watu wanaodai hati halisi ya muungano na kutishia kufungua kesi katika mahakama ya umoja wa mataifa baada madai yao kutupiwa mbali na mahakama kuu ya Zanzibar.
Wednesday, June 23, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment