I made this widget at MyFlashFetish.com.

Saturday, June 5, 2010

KARUME AZINDUA UMEME PEMBA

Rasi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amesema huduma ya umeme wa uhakika ulioko kisiwani Pemba utasaidia kufungua milango ya uwekezaji kisiwani humo.

Akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa mradi wa umeme wa uhakika kutoka Tanga hadi Pemba amewahimiza wananchi kuitumia nafasi hiyo kwa kuekeza miradi mbali mbali ya kiuchumi.

Amesema lengo la mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapa fursa wananchi kujendeleza kiuchumi na kusema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuona wananchi hao wanafanikiwa katika sekta ya uwekezaji.

Rais Karume amesema mbali ya umeme huo kusaidia sekta za uchumi, lakini pia utarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile usambazaji wa maji, elimu na huduma nyingine za kijamii….

Aidha rais Karume amewataka wananchi kuyaenzi maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa hivi karibuni katika kujenga umoja wao na kuimarisha amani na utulivu ili uchaguzi mkuu ujao utofautiane na miaka iliyopita.

Amesema wananchi wa Zanzibar wote ni wa moja hivyo ni vyema kujenga mshikamano katika kuiletea maendeleo nchi yao…..

Kwa zaidi ya maiak 40 wananchi wa Pemba wamekuwa wakitegemea huduma ya umeme kwa kutumia majenerata ambayo yakidhi mahitaji.

Mradi huo wa umeme uliogharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 75 umefadhiliwa Norway ambapo serikali ya Mapinguzi imetoa zaidi ya dola milioni 10 na serikali ya muungano imechangia dola milioni tano.

No comments:

Post a Comment