Chama cha Jahazi asilia kimesisitiza msimamo wake wa kutaka kuwepo na serikali ya umoja wa kitaifa itakayovishirikisha vyama vyote vya siasa nchini.
Mwenyekiti wa chama hicho Amour Rajab Amour amesema serikali ya aina hiyo itasaidia kuepusha mifarakano ya kisiasa ilinayotokezea mara kwa mara hapa Zanzibar hasa nyakati za uchaguzi wa kitaifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Amour amesema iko haja ya kuandaliwa katiba mpya ya Zanzibar itakayozingatia matakwa ya mfumo wa vyama vingi na uchaguzi.
Amesema katiba inayotumika hivi sasa ya mwaka 1984 iko katika mfumo wa chama kimoja na kusema matatizo yalitokea katika chaguzi za mwaka 1995, 2000 na 2005 yalisababishwa na katiba hiyo.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi utakaofanyika Octoba mwaka huu Amour amesema chama hicho kina nia ya kumsimamisha mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar, ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia chama hicho.
Chama cha Jahazi asilia kilichosajiliwa Novemba 2004, katika uchaguzi wa mwaka 2005 kilimsimamisha mwenyekiti wake wa zamani Haji Mussa Kitole kuwania kiti cha urais wa Zanzibar na kupata asilimia sufuri nukta nne, nane na kukosa nafasi za uwakilishi, ubunge na udiwani
Sunday, June 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment