I made this widget at MyFlashFetish.com.

Saturday, June 5, 2010

WALIOSHINDA KURA YA MAONI CUF HUENDA WAKAENGULIWA-SEIF SHARIF

Chama cha wananchi CUF kimewatahadharisha wanachama wake walioshinda katika kura ya maoni kuwania nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wanaweza kuondolewa endapo baraza kuu la chama hicho litaona upo umuhimu wa kufanya hivyo.

Katibu mkuu wa chama hicho Seif Sharif Hamad amesema ingawa baraza kuu litaheshimu maoni ya wanachama lakini, baraza hilo ndio litakalofanya uteuzi wa mwisho.

Hata hivyo amesema kila mwanachama awe mwanamke au mwanamme anayo haki ya kugombea nafasi yoyte katika chama au katika nafasi za uongozi wan chi kupitia

Kauli hiyo ya Hamad imekuja siku chache baaba ya wagombea kadhaa wanawake waliojitokeza kugombea nafasi za ubunge na uwakilishi kukatiliwa katika kura za maoni.

Amesema chama cha CUF kilijitahidi kufanya kampeni za kuwataka wanawake kujitokeza Kwa wingi kugombea nafasi za uongozi , lakini kinachoonekana kwamba wanawake hao hawajiamini.

Amesema wanachama wamefanya uwamuzi juu ya wagombea hao na uwamuzi wao utaheshimiwa, lakini baraza kuu la chama hicho ndilo lenye uwamuzi wa mwisho baada kuchunguzwa kwa makini wagombea hao.

Katika kura ya maoni ya CUF mwaka 2005 mwakilishi wa jimbo la mji Mkongwa Fatma Fereji na mbunge wa jimbo la Chake chake Fatma Magimbi walishinda kura lakini mwaka huu wamekataliwa.

Baraza kuu la CUF linatarajiwa kufanya kikao chake June 25 mwaka huu ili kuchunguza na kupitisha majina yawagombea walioshirika katika kura ya maoni ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment