I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, June 23, 2010

SERIKALI YA MSETO Z’BAR YAUNGWA MKONO NA WAISLAM

Jumuiya ya Maimamu Zanzibar JUMAZA imesema inaunga mkono kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kama hatua moja wapo ya kuimarisha amani na utulivu nchini.

Katibu Mtendaji wa JUMAZA sheikh Muhdin Zuber Muhdini amesema hatua hiyo ni kuzishukuru neema za mwenyezi mungu zilizoondosha siasa za chuki zilizoleta mirafarakano na uadui

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa amesema serikali ya umoja wa kitaifa ndio suluhisho la kuleta amani, hivyo amewataka wananchi kushiriki katika kura ya maoni ili kutoa ridhaa ya kuundwa serikali hiyo…

Hata hivyo Sheikh Muhidin amesema jumuiya hiyo haiwezi kuwalazimisha wananchi kutumia uhuru wao wa kuamua, lakini jumuiya za waislamu zinajukumu la kuielekeza jamii umuhimu wa kulinda amani na utulivu.

Aidha jumuiya hiyo pia imewataka wananchi kuendeleza amani na utulivu uliopo hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa kuwachagua viongozi mbali mbali wa nchi.

Tamko hilo la JUMAZA la kuunga mkono kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa limefikiwa katika kikao chake kilichofanyika June 12 mwaka huu na kuzishirikisha jumla ya taasisi 18 za kislamu

No comments:

Post a Comment