Tuesday, June 1, 2010
VITENDO VYA UHARAMIA VINAWEZA KUATHIRI UCHUMI WA Z’BAR-DR. MWINYIHAJI
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwepo kwa vitendo vya uharamia kati ya visiwa vya Unguja na Pemba vinavyoripotiwa katika vyombo vya habari kunaweza kuathiri uchumi wa Zanzibar. Akizungumza na zenji fm radio juu ya athari za vitendo hivyo kwa uchumi wa Zanzibar waziri anaeshughulikia masuala ya fedha na uchumi Dr. Mwinyihaji Makame amesema licha ya kutopata uthibitisho wa vitendo hivyo, lakini Zanzibar ni sawa na nchi nyingine ziliomo katika ukanda wa bahari ya Hindi inaweza kuathirika kiuchumi kutokana na uharamia huo. Amesema iwapo meli za mizigo zinazotaka kuingia katika eneo la Afrika ya mashariki zinatishiwa na maharamia wa kisomali bila shaka hali ya uchumi wa Zanzibar itakuwa mbaya. Hata hivyo Dr. Makame amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kufanya doria za kuwasaka maharamia hao walioripotiwa kuwepo katika kisiwa cha Pemba. …CLIPS…(SAVED-MWINYIHAJI) Kazi ya kuwasaka maharamia hao wa kisomali bado zinaendelea kwa ushirikiano wa jeshi la polisi, vikosi vya SMZ pamoja na jeshi la wananchi Tanzania JWTZ. Akizungumza na Zenji Fm Radio juu ya msako huo kamanda wa kikosi cha kuzuia magendo KMKM kisiwani Pemba amesema kuwa kazi inaendelea vizuri na hadi sasa wananchi wanatoa ushirikiano mzuri……CLIPS….(SAVED-KMKM) Msako huo umekuja siku moja baada ya kuripotiwa watu wanaodaiwa maharamia waliotaka kuiteka nyara meli moja katika bahari ya Hindi upande wa Tanzania kukimbilia kisiwani Pemba. Maharamia hao wamekimbilia Pemba baada ya kushambuliwa na majeshi ya jumuiya ya umoja wa ulaya wanaofanya doria katika pwani ya Afrika ya mashariki wakitaka kuiteka meli kati kati ya bahari ya visiwa vya Unguja na Pemba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment