I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, July 11, 2010

SHENI AKATA TIKETI YA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM


Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akiwashukuru wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kwa kumchagua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM.


Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa White house mjini Dodoma jana usiku.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya ushindi wa Dr.Ali Mohamed Shein kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM jana usiku.