I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, June 1, 2010

SUALA LA MAFUTA NA GESI ASILIA LISIHUSISHWE KISIASA-NORWAY

Serikali ya Norway imesema suala la uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar lisichukuliwe kwa mtazamo wa kisiasa, kwa vile linahitaji kuekewa sera na sheria zitakazotoa maslahi kwa wananchi.

Mtaalamu wa nishati ya mafuta kutoka Norway Al-Kassim Farouk amesema inawezekana Zanzibar kuwa na hazina kubwa ya mafuta na gesi asilia, hivyo ni vyema kuanza kuzifanyia marekebisho sheria na sera zake na kulihusisha suala hilo ndani ya katiba.

Farouk amesema hayo katika semina ya utawala bora wa masuala ya mafuta na gesi asila iliyowahusisha baadhi ya mawaziri na maafisa wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika hoteli Zanzibar Beach Resort.

Amesema uchimbaji wa nishati ya unahitaji mtaji mkubwa na wataalamu wa kutosha kwa wenye makampuni, hivyo ni lazima kuwepo na sera zitazo vutia makampuni ya kigeni kuwekeza katika sekta hiyo.

Hata hivyo ameishauri serikali kuwa makini na uingiaji wa mikataba na makampuni ya mafuta ili kuona wananchi wananufaisha pamoja na kuepusha uharibifu wa mazingira.

Nae waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema semina hiyo ni mwendelezo wa kuwandaa viongozi wa serikali kuwa na maamuzi katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Aidha amesema serikali itaendelea kuwashirikisha wataalamu wa ndani na nje ya nchi ili utafutaji na uchimbaji wa nishati hiyo usije ukaleta athari ya uharibifu wa mazingira kama ule uliotokea Marekani hivi karibuni.

Mafuta na gesi asilia ni miongoni mwa mambo ya muungano, lakini serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia baraza la wawakilishi na baraza la mapinduzi imemaua suala hilo kulishughulikia peke yake.

No comments:

Post a Comment