Mbunge wa jimbo la Uzini Mohammed Seif Khatib amewataka wananchi wa jimbo hilo kutumia raslimali ya ardhi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
Amesema chimbuko la mabadiliko ya binadamu ni kutumia raslimali ya ardhi, kuendeshea shughuli za kilimo, ufugaji na utowaji wa huduma nyingine za kijamii kazi ambazo zinaweza kuwakomboa na umasikini.
Khatib ambae pia ni waziri anaeshughulikia masuala ya muungano ametoa wito huo alipokuwa akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa jumuiya za maendeleo za shehia za Tunduni na Mgenihaji.
Amesema serikali imejitahidi kuweka miundo mbinu ya barabara, maji na umeme ambayo inaweza kumsaidia mwananchi kuleta mabadiliko yake binafsi, familia na taifa kwa ujumla.
Aidha Khatib amesema mafunzo hayo ni chachu kwa wananchi wa vijiji hivyo ili kubuni miradi itakayoleta mbadiliko ya kiuchumi na kijamii katika shehia hizo.
Mafunzo hayo yalioendeshwa kwa awamu tatu tofauti kuanzia April hadi Mei 22 mwaka huu na kufadhiliwa na taasisi ya jumuiya ya kiraia yaliwashirikisha viongozi wa kamati, wajumbe wa kamati tendaji, wahasibu na washika fedha wa jumuiya za maendeleo za vijiji hivyo.
Sunday, June 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment