Kamati ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi Tanzania TEMCO imesema inashindwa kutekeleza shughuli za uangalizi wa chaguzi zinazofanyika nchini kutokana na uhaba wa fedha.
Mratibu wa TEMCO DR. Benson Banner amesema taasisi hiyo inayofanya kazi muhimu, lakini haipokei fungu lolote la fedha kutoka serikalini na badala yake hutegemea wahisani wenye masharti magumu.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari wa utowaji wa taarifa ya mwenendo wa uchaguzi mwaka 2010 mjini Zanzibar amesema hali hiyo imeifanya TEMCO kuwa na wangalizi wachache ikilinganishwa na ukubwa wa maeneo ya uchaguzi Tanzania.
Dr. Banner amesema taasisi za ndani zina uwezo mkubwa wa kuendesha shughuli za uangalizi wa chaguzi zinazofanyika nchini ikilinganishwa na taasisi za kimataifa, lakini bado haiziwezeshwi kifedha na serikali
Nae makamo mwenyekiti wa tume hiyo Maryam Abdulrahman amesema TEMCO inatarajia kutuma wangalizi wa uchaguzi elfu saba, 210 katika majimbo yote ya Tanzania bara na Zanzibar kuangalia mwenendo wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.
Amesema wangalizi hao wa muda mrefu na mfupi watatumwa majimboni na kwenye vituo vya kupigia kura kuangalia undeshaji wa kampeni, upigaji na kuhesabu kura, utowaji wa matokeo, malalamiko na ukataji wa rufaa ambapo taarifa zake zitatolewa ndani ya siku tano baada ya upigaji wa kura.
TEMCO ni taasisi ya ndani inayoundwa na taasisi mia moja na 52 imekuwa ikiangalia mwenendo wa uchaguzi Tanzania tokea mwaka 1995.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment