I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, September 1, 2010

TATIZO LA SOMALIA NI UINGILIAJI KATI WA MATAIFA YA KIGENI-HIZB UT-TAHARIR

Jumuiya ya kislamu ya kimataifa ya Hiz Ut-Tahrir imepinga ungiliaji kati unaofanywa na mataifa ya kigeni katika mzozo unaoendelea nchini Somalia kati ya wanamgambo wa Al-shabab na serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa naibu mwakilishi wa wa vyombo vya habari vya Jumuiya hiyo Afrika Mashariki Massoud Mselem amesema mzozo wa Somalia hauhitaji nguvu za kijeshi bali ni kuangalia kiini cha tatizo lenyewe.

Amesema suluhisho la amani ya Somalia sio kupambana na wanamgambo wa Al-Shabab bali ni kupinga uingiliaji kati wa masuala ya nchi hiyo dhidi ya mataifa ya kigeni…

Akizungumzia mateso na vitendo viovu wanavyofanyiwa waislamu wa Tajikistan Masoud ameitahadharisha dola hiyo na kusema iwapo hasara itatokea itarejea upande wa taifa hilo na kusema chama hicho kitajitolea kulingania utukufu wa mwezi mungu.

Amesema serikali ya Tajikistan inafanya makosa hayo huku ikiungwa mkono na madola ya magharibi na taasisi zinazodai kutetea haki za binadamu zikiwa zimekaa kimya.

Masoud amefahamisha zaidi ya waislamu 300 wa Tajikistan wanaendelea kusulubiwa kwa mateso, uonevu na vifungo vya muda mrefu.

Amesema Hiz ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani mateso na uharamia wanaofanyiwa waislamu wasiokuwa na hatia na utawala wa nchi hiyo unaongozwa na rais Rahmanov.

Jumuiya ya Hiz ut-Tahrir ni chama cha kislamu cha kimataifa chenye malengo ya kurejesha tena uislamu kupitia dola ya Helaf iliyoangushwa mwaka 1924.

No comments:

Post a Comment