I made this widget at MyFlashFetish.com.

Friday, September 10, 2010

RAIS KARUME AMEWATAKA VIONGOZI WA SIASA KUENDESHA KAMPENI ZA KISTAARABU

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume, amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu kwa kuheshimiana, umoja, amani na utulivu.

Amesema siasa sio ugomvi bali ni sehemu ya kutekeleza mahitaji ya watu, hivyo ni vyema kwa wananchi na viongozi wa siasa kuimarisha hali ya utulivu, ili kulinda maridhianoya kisiasa yalioleta umoja na mshikamano.

Akilihutubia baraza la Ediel fitr huko Forodhani, rais Karume amesema katika kipindi kilichopita cha utulivu wa kisiasa nchini, kimeleta mafanikio ya uchumi na ustawi wa jamii, kama vile ujenzi wa miradi ya miundo mbinu, elimu, afya, sekta za huduma na utalii

Hata hivyo rais Karume anaemaliza muda wake, baada ya kufanyika uchaguzi mkuu Octoba 31, amesema juhudi zaidi zinahitajika kuendeleza nyanja nyingine za maendeleo kwa faida ya kila mwananchi.

Amesema wananchi hawanabudi kujituma zaidi, ili kuona mipango ya serikali, kama vile mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini MKUZA na malengo ya Milenia inafanikiwa kwa lengo la kuinua pato la taifa.

Baraza hilo la edil fitr, linalofanyika baada ya waislamu kumaliza wamwezi mtukufu wa ramadhan, pia limehudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa na mabalozi wadogo wanaoziwakilisha nchi zao Zanzibar.

No comments:

Post a Comment