Hoteli nne za kitalii na nyumba 12 za wananchi katika kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kusini Unguja zimeteketea kwa moto leo mchana.
Katika tukio hilo hakuna mtu aliejeruhiwa, huku baadhi ya mali zilizokuwemo ndani ya hoteli hizo zimeripotiwa kuteketea kwa moto na nyingine zimewahi kutolewa na wasamaria wema.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema awali waliona moto na moshi mkubwa ukitokea katika maeneo yenye hoteli za kitalii na baadae moto huo kusambaa katika hoteli nyengine ambazo zilikuwa zikiwaka kwa kasi kubwa kutokana na upepo uliokuwa ukivuma baharini nyakti hizo.
Wamesema kikosi cha zima moto na ukozi kilichelewa kufika katika eneo la tukio, huku likiwa halina maji na kulazimika kutumia maji ya bahari lakini baadae lilikwama na kusababishwa moto huo kuchelewa kuzimwa. Hata hivyo mkuu wa Zima moto Sajenti Shukuru amesema wamemaliza kuzima moto huo na kukanusha madai kwamba gari lilikuwa halina maji na kukwama ufukweni
Kamanda wa ppoli mkoa wa kuskazini Unguja, Mselem Masoud Mtulya alithibitisha kutokea kwa moto huo na kuzitaja hoteli zilizoungua ni pamoja na Rummi ambayo imeteketea vibaya sana kwa kuwa ndio iliyoanza kuwaka na baadae moto huo kusambaa na kurukia katika hoteli iitwayo Bwagamoyo ambayo imeungua paa lote la hoteli hiyo.
Kamanda Mtulya alisema baadae moto huo ulishika katika hoteli ya Union ambayo nayo imeungua vibaya vyumba vya kulala na eneo lote la baa, ukumbi wa chakula na maduka ya vifaa na nguo za kitalii yaliokuwa ndani ya hoteli hiyo.
Aliitaja hoteli nyengine ni Diving Center ambayo nayo ilitekeleta katika eneo lake la ukumbi uitwao East Afrcan, ukumbi wa jambo brothers, sehemu ya jikoni yote imeungua na baadhi ya vyumba na kumbi zake zikiwa zimetekeleata vibaya sana.
Aidha alisema licha ya moto huo kusambaa kwa kasi lakini wageni wanane waliokuwa wamelala ndani waliwahi kuokolewa huku wengine wakiwa wamekimbia ambao wengi wao nyakati hizo walikuwa nje ya hoteli hizo na baadhi yao walikuwa wakipunga upepo na wengine walikuwa katika sehemu za kulia wakijipatia chakula.
Alisema nyumba za wananchi nazo hazikusalimika kutokana na moto huo ambapo zaidi ya nyumba 12 ambazo zipo karibu ya hoteli hizo zilizoungua zimeshika moto kutokana na moto huo kusambaa kwa kasi kutokana na upepo na kuwa zimeezekwa paa za makuti ambazo hushika moto haraka.
Kamanda Mtulya alisema chanzo cha moto huo hakijajulikana bado lakini jeshi la polisi linajitahidi kutafuta chanzo halisi cha kuzuka moto huo kabla ya kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vinavyohusika.
Hasara iliyoptaikana kutokana na moto huo bado haijajulikana. Hii ni mara ya pili kwa hoteli za kitalii kuungua moto kwa kipindi kisichozidi miezi miwili ambapo tukio la mwanzo hoteli tatu kwa pamoja ziliungua moto katika kijiji cha Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja.
Tatizo la hoteli kuungua moto limekuwa likitokea mara kwa mara visiwani Zanzibar ambapo mwezi uliopita jumla ya hoteli za kitalii na nyumba zaidi ya sita ziliteketea kwa moto katika kijiji cha Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Hoteli zilizoungua mwezi uliopita ni pamoja na Visitors Inn, Sau Inn na Bungalow ambapo zote zipo eneo la Jambiani ukanda wa pwani ambapo kumbi na zaidi ya vyumba 12 vya kulala wageni viliteketea kutokana na moto huo.
Friday, September 10, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment