I made this widget at MyFlashFetish.com.

Friday, September 10, 2010

ZANZIBAR KUTARAJIWA KUKUBWA NA UKAME

Baadhi ya maeneo ya Unguja na Pemba yanatarajiwa kukumbwa na ukame utakaosababisha uhaba wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo na kilimo cha umwagiliaji maji kutokana uhaba wa mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza wiki ya pili mwezi ujao.

Taarifa ya mamlaka ya hali hewa Tanzania iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema hali hiyo inatokana na mvua za vuli kunyesha chini ya kiwango kitakacho athiri unyevunyevu wa kuotesha miti, mazao na malisho ya mifugo.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imewashauri wakulima na wafugaji kutumia maji kwa uangalifu, kuotesha mazao yanayostahamili ukame na kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo katika maeneo yao.

Akizungumza na Zenji Fm Radio juu ya taarifa hiyo inayotishia kuathiri mifugo na kilimo cha umwagiliaji maji hapa Zanzibar mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa Zanzibar Khamis Ali Suleiman amesema

Taarifa hiyo ya hali ya hewa inayoashiria uhaba wa mvua za vuli imetolewa na wataalmu wa hali ya hewa wa nchi za eneo la Pembe ya mashariki mwa Afrika waliokutana mjini Nairobi Kenya kuanzia Agost 23 hadi Septemba tatu mwaka.

No comments:

Post a Comment