Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeishukuru serikali ya watu wa China kwa juhudi inazochukua katika kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza umasikini kwa wananchi.
Waziri anaeshughulikia fedha na uchumi Dr. Mwinyihaji Makame ametoa pongezi hizo katika hafla fupi ya utiaji wa saini wa mradi wa kupunguza malaria uliotolewa na serikali ya China.
Amesema mbali na China kutoa misaada mbali mbali ya kiuchumi na kijamii lakini pia imekuwa ikisaidia sekta ya afya ikiwa ni miongoni mwa juhudi za serikali za kuimarisha sekta hiyo ili kupunguza umasikini.
Dr. Makame amesema msaada huo wa China wa kupambana na ugonjwa wa malaria utaisaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vinavyotoka na maradhi hayo yanayowasumbua wananchi.
Nae balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Le Jiang Pehn amesema mradi huo utagharimu zaidi ya dola za Marekani laki moja na elfu 46.
Serikali ya China imetoa misaada kadhaa kwa Zanzibar ikiwemo dawa, matrekta ya kulimia, matengenezo ya uwanja wa Amani pamoja na umarishaji wa vyombo vya habari.
Thursday, May 27, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment