Sunday, May 2, 2010
MKUU WA WILAYA YA WATE AGIZA KUFUKUZWA KAZI WAFANYAKAZI WAWILI WA HOSPITALI YA WETE BAADA YA KUTOA MANENO MACHAFU KWA MAMA MJAMZITO
Mkuu wa wilaya ya Wete Omar Khamis Suleiman ameagiza kusimamishwa kazi wafanyakazi wawili wa hospitali ya Wete baada ya kumtolea lugha chafu mama mjawazito aliekwenda kujifungua katika hospitali hiyo.
Hatua ya kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi hao imekuja baada ya mama mjamzito huyo ambae ni mke wa mkuu wa wilaya hiyo kutolewa lugha chafu na wafanyakazi hao wakati alipokwenda kujifunugua.
Akizungumza na mwandishi wetu kisiwani Pemba Bw. Suleiman amesema wafanyakazi wa hospitali hiyo wanaowapokea wagonjwa wanawatolea lugha chafu wagonjwa wakati wanapotaka kupatiwa matibabu na kuwafanya kuichukia hospitali hiyo.
Amesema lugha kama hizo sio nzuri na kusema yeye mwenyewe amezigundua na kuagiza hatua za kusimamishwa kazi zichukuliwe na uongozi wa wizara ya afya na ustawi wa jamii.
Amefahamisha kuwa serikali yake itaendelea kuchukua hatua kama hizo kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo vya afya vingine hasa maeneo ya vijijini kutokana na vitendo vya aina hiyo kukithiri.
Nae katibu wa hospitali ya Wete Salim Mohammed amesema amezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwa kuwaona baadhi ya wafanyakazi wanakiuka maadili ya kazi na kusema wataendelea kuwaelimisha ili kukomesha vitendo hivyo viovu.
Tukio kama hilo limesharipotiwa kutokea katika hospitali za Pemba ambapo wagonjwa wanadai kunyanyaswa na wafanyakazi wa hospitali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment