Sunday, May 16, 2010
MREMA ASEMA HAAMINI KUWA KAULI YA RAIS KIKWETE YA HIVI KARIBUNI JUU YA TAKRIMA ILIKUSUDIA KUHALALISHA TAKRIMA
Katika mbio za kuelekea uchaguzi mkuu Tanzania unaotegemewa kufanyika Oktoba mwaka huu, wanachama na wanasiasa wa vyoma tofauti nchini wamekuwa wakitangaza nia za kugombea nafasi tofauti katika vyama vyao.
Miongoni mwa wanachama hao ni pamoja na Bw Mtanegwa Mhinywa na Bw Maxmilian Lyimo wa TLP wametangaza nia ya kugombea kiti cha urais katika serikali ya jamhuri ya muungano wa Tananzia.
Akithibitisha hayo Mwenyekiti wa TLP Taifa B w Augustine Lyatonga Mrema amesema kuwa endapo mmoja kati yao atakuwa na sifa kwa mujibu wa taifa letu na wakapitishwa na mkutano mkuu wa chama chake wataruhusiwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.Bonyeza HAPA kumsikia Bw Augustine Mrema...Athibitisha baadhi ya wanachama kutangaza nia ya kugombea urais
Kwa upande wa tarifa iliyopewa nafasio kubwa mwishoni mwa wiki katika vyombo vya habari kuwa Rais Kikwete juzi mbele ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, muda mfupi kabla ya kufunga mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ambao ulijadili masuala ya uchaguzi na sheria zake amekiri kuwa kuikomesha takrima ni jambo gumu kwa sababu utamaduni wa Mtanzania umejengwa kwa misingi ya kumkirimu mgeni, kauli ambayo imechukuliwa kwa hisia tofauti na baadhi ya wnasiasa na wananchi.
Kufuatia hili Nyota Matukio ilitaka kufahamu kwa upande wake Bw Mrema ana maoni gani juu ya kauli hiyo..bonyeza HAPA kumsikia Bw Augustine Lyatonga Mrema...Maoni yake juu ya kauli ya Rais ya Takrima
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Nyota Matukio haikuishia hapo pia ilimtafuta mwanasiasa na mhadhiri katika chuo kikuu cha Dra es salaam Dr Sengondo Mvungi ambae ni mwalimu wa sheria na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha NCCR Mageuzi ambae amesema kuwa, kauli hiyo ni kupigwa vita vita na watanzania kwa nguvu zote kwa vile kufanya hivyo ni kuvunja katiba ya nchi.
Dr Mvungi amesema kuwa kama Rais Kikwete ameamua kutoa kauli hiyo, ina maana kuwa chama chake cha CCM kiko tayari kuvunja katiba na sheria na hatimaye kutoa takrima..Bonyeza HAPA kumsikia Dr Sengodo Mvungi....Maoni yake juu ya kauli ya Kikwete kuh takrima
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Baada ya kusikia kauli tofauti kutoka kwa wanasiasa mbali mbali Nyota matukio iligeukia upande wa chama tawala ambacho kinashutumiwa kuwa ni chama cha rushwa ambapo tulibahatika kuzungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Capt John Chiligati ambae amesema kuwa kauli ya Rais Kikwete imepotoshwa kwa makusudi na baadhi ya vyombo vya habari na amekanusha kuwa Rais amesema takrima ni kuksa.
Chiligati amefafanua kuwa Rais alikuwa anatoa maelezo kuwa baadhi ya maeneo utekelezaji wa sheria hiyo ni mgumu kutokana na mila na desturi za baadhi ya maeneo nchini na sio kuruhusu takrima kama ilivyoandikwa na baadhi ya magazeti.
Aidha Chiligati amesema kuwa sheria ya takrima iko pale pale na hivi karibuni bunge lilipigilia msumari wa moto sheria hiyo ambapo amedai kuwa hata wakati wa kura za maoni endapo watu watatoa takrima ni rushwa na atakaebainika sheria itachukua nafasi yake..Bonyeza HAPA kumsikia John Chiligati....Kauli ya Kikwete kuh takrima yapotoshwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment