I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, May 2, 2010

HAI HAI KWA WAGOMBEA KITI CHA URAIS ZANZIBAR ZAANZA

Wakati tume ya uchaguzi Zanzibar ikitangaza uchukuwaji wa fomu za kuwania kiti cha urais wa Zanzibar kuanza tarehe 10 hadi 30 Agosti baadhi ya wananchi wamejaa hamu ya kutaka kujua jina la mgombea atakae mrithi rais Karume anaemalizia muda wake.

Wanaotajwa kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM ni waziri kiongozi wa zamani Dr.Mohammed Gharib Bilal aliejitokeza kuwania kiti hicho mwaka 2000 na 2005.

Wengine wanaotajwa kutaka kuwania kiti hicho ni waziri kiongozi wa sasa Shamsi Vuai Nahodha, makamo wa rais Dr. Ali Mohammed Shein, waziri wa elimu Haroun Ali Suleiman na waziri anaeshughulikia masuala ya muungano Mohammed Seif Khatib.

Balozi wa Tanzania nchini Itali Ali Karume kaka yake rais wa sasa wa Zanzibar tayari ameshajitokeza kutaka kuwania kiti hicho na mwengine anaetajwa ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Afrika ya Kusini Profesa Makame Mbarawa Mnyaa.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema rais atakaefaa kuiongoza Zanzibar ni yule atakayewaunganisha wazanzibari, kuondosha tofauti za kisiasa zilizoathiri shughuli za maendeleo za visiwa vya Unguja na Pemba.

Akizungumza katika mkutano wa makada wa CCM wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu Tanzania jana makamo mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar rais Amani Abeid Karume amewataka wananchi kuwakataa viongozi wanaowashawishi kukataa serikali ya umoja wa kitaifa kupitia kura ya maoni.

Tume ya uchaguzi Zanzibar imetangaza uchaguzi mkuu wa rais, wawakilishi na madiwani utafanyika tarehe 31 Octoba na kampeni rasmi za chaguzi hizo zitaanza terehe 10 hadi 30 Septemba na matokeo ya uchaguzi yatangazwa tarehe 31 hadi tarehe pili Novemba 2010.

No comments:

Post a Comment