I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, May 2, 2010

WAJIRI ZANZIBAR WASEMA VIJANA WENYE TAALUMA ZA KUJIRIWA NI KIDOGO

Chama cha waajiri Zanzibar ZANEMA kimesema kinakabiliwa na mtihani katika kuwachagua vijana wa kuwajiri kutokana na taaluma zao kuwa ndogo.

Mkurugenzi wa ZANEMA Salah Salim Salah amesema ili kuondokana tatizo hilo ameiomba serikali kuchukua juhudi za kuwaendeleza vijana kitaaluma ili waweze kuajirika hasa katika sekta binafsi.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani amesema wakati huu wa ushindani wa mitaji katika uwekezaji, taasisi binafsi zinahitaji wafanyakazi wenye ujuzi na uwezo, hivyo haitakuwa rahisi kuajiriwa vijana wasiokuwa na uwezo.

Amesema suala la kuwaendeleza vijana kitaaluma ili waingie katika soko la ajira linahitaji kufanywa kuwa agenda ya kitaifa.

Aidha mkurugenzi huyo wa ZANEMA ametoa wito kwa serikali kuzifanyia marekebisho sheria za kazi zinazokwenda kinyume na mikataba ya kimataifa ili kutoa fursa kwa watu wenye ulemavu kupata ajira.

Nae katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar ZATUC Khamis Mwinyi Mohammed ameutaka mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF kutoa mafao yote kwa wananchama wake kama yalivyoainishwa katika sheria ya kuanzisha mfuko huo.

Mfuko wa wa ZSSF ambao unaendelea kutoa mafao ya uzeeni kwa wananchama wake wanaostaafu kazi, lakini bado haujanza kutoa mafao ya uzazi na ugonjwa.

No comments:

Post a Comment