Jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar Zapha plus imesema inakabiliwa na ongezeko la watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki na ukimwi pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao wazazi wao wanaishi na virusi vya ukimwi.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Jumuiya hiyo Salma Soud Nasibu wakati akizungumza na zenjiFm Radio huko afisini kwake Vuga mjini Zanzibar .
Amesema kutokana na ongezeko hilo Jumuiya hiyo imekuwa haina uwezo wa kuweza kuwapatia mahitaji mbali mbali ambayo wanahitaji watoto hao.
Aidha Mratibu huyo ameeleza kuwa Jumuiya hiyo pia imekuwa ikikosa uwezo wa kuweza kuwasaidia wanachama wao ambao wamepatiwa Rufaa ya Kimatibabu nje ya Zanzibar hivyo kupelekea kukosa msaada msaada kutokana na tatizo hilo.
Hivyo ameziomba Taasisi mbali mbali Jamii na Serikali kuitambua Jumuiya hiyo na kutoa misaada mbali mbali katika kuhakikisha watu wanaishi na virusi vya ukimwi wanaishi katika mazingira bora na salama
Tuesday, May 11, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment