I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, May 20, 2010

MASAUNI AJIUZULU


Habari tulizozipata katika chumba chetu cha habari zinasema mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa chama cha Mapinduzi UV-CCM bwana Masauni amejiuzulu katika mkutano wa jumuiya hiyo unaofanyika mkoani Iringa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari katika mkutano ameiambia Zenji Fm radio naibu katibu mkuu wa UV-CCM upande wa Zanzibar bw. Mohamme Moyo nae pia amejiuzulu.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa UV-CCM wilaya ya Kinondoni mjini Dar es Salaam Emanuel Malema amesema mabishano kati ya viongozi hao na wajumbe wengine wa mkutano huo yalikuwa makali.
Amesema malumbano hayo yanatokana na wanasiasa wachache kuwatumia vijana wa Jumuiya hiyo kwa maslahi yao binafsi.

Aidha Malema alifahamisha shutuma anazotupiwa Masauni za kuhushi umri wake ni njama za wanasiasa wachache waliomo ndani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Viongozi hao waliojiuzulu Masauni na Moyo wanadaiwa kujipunguzia umri katika vikao vilivyohusika kupitisha majina yao wakati walipogombea nyadhifa hizo.
Hivi karibuni bw. Masauni alitanagaza nia yake ya kutaka kuteuliwa na chama chake cha CCM kuwa mgombea wa ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu

No comments:

Post a Comment