I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, May 16, 2010

ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Seif Sharif Hamad wanatarajiwa kufanya uzinduzi wa utowaji wa elimu ya kura ya maoni itakayofanyika Julai 31 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema amewalika viongozi hao kutokana na mchango wao usiosahaulika katika historia ya Zanziar juu ya maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa amesema ingawa tarehe rasmi ya uzinduzi huo haijatolewa, lakini viongozi hao watatoa mchango mkubwa wa kuwaelimisha wananchi ili kushiriki katika kura ya maoni itakayotoa ridhaa ya mfumo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Hata hivyo Mwinyichande amesema katika kura hiyo hakutakuwa na kampeni kwa vile hakuna pande zinazopingana
Kura maoni itafanyika Zanziar Julai 31 kwa mara ya kwanza tokea mapinduzi ya 1964 inatokana na maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa Novemba 5 kati rais Karume na katibu mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad.
16

No comments:

Post a Comment