I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, May 20, 2010

ZANZIBAR NA SOKO LA PAMOJA

Zanzibar imeelezewa huenda ikawa msindikizaji katika soko la pamoja la Afrika ya Mashariki linalotarajiwa kuanza hivi karibuni kutokana na kutegemea bidhaa kutoka nje ya nchi kwa asilimi 97.
Mwakilishi kutoka Jumuiya ya wafanyabiashara, wenyeviwanda na wakulima Msellem Khamis amesema Zanzibar inasafirisha bidhaa zake nje ya nchi kwa asilimia tatu hali ambayo inaweza kuiathari mara baada ya soko hilo kuanza Julai mwaka huu.
Aidha amesema wafanyabiashara wengi wa Zanzibar hawana uwezo wa kujiendeleza kibiashara kutokana na masharti magumu na riba kubwa zinatozwa na benki zinazotoa mikopo ikilinganishwa na nchi jirani.
Amefahamisha kuwa serikali ya Kenya ambayo inawasaidia wafanyabiashara wake kwa kuwapa mikopo yenye masharti na riba nafuu hadi kufikia mwaka 2007 zaidi ya wawekezaji 45 wamewekeza Tanzania.
Hivyo bw. Mselem ameiomba serikali ya mapinduzi Zanzibar kuwasaidia wafanyabishara wa ndani pamoja na kuzijengea uwezo wa kitaalamu sekta binafsi ili waweze kuleta ushindani katika soko hilo.

Nae mfanyabiashara wa Zanzibar Salum Turki amesema ipo haja kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuisiadia Zanzbiar kuimarisha sekta ya viwanda kutokana na hali yake ya kigeoraphia
Aidha baadhi ya wajumbe wengine wa mkutano huo wamelezea soko la pamoja la nchi za Afrika Mashariki linaweza kuisaidia Zanzibar kupanua sekta ya uwekezaji na nafasi za ajira kwa wananchi.
Jumuiya ya Afrika ya mashariki iliyoanzisha mwaka 1999 tayari imeshatekeleza itifaki za ushuru wa forodha, soko la pamoja na baadae inatarajiwa kutumia sarafu ya pamoja na hatimae kuwa shirikisho la kisiasa.

No comments:

Post a Comment