Tuesday, May 4, 2010
KESI YA MAUWAJI YA RAIA WA CHINA IMEENDELEA TENA
Mtuhumiwa mmoja wa kesi ya mauwaji ya raia wa china Hwang Hong Xing yaliyotokea Septemba 2006 huko Mazizini amefutiwa dhamana yake baada ya kutohudhuria mahakamani wakati kesi hiyo ikiendelea.
Akitoa uamuzi huo Jaji Abraham Mwampashi wa mahkama kuu Vuga Mjini Zanzibar amemtaja Mtuhumiwa huyo ni Bimkubwa Said Bakar amevunja masharti ya dhamana aliyopewa na mahkama hiyo.
Amesema dhamana hiyo imefutwa baada ya mtuhumiwa huyo kutohudhuria mahakamani kwa siku alizopangiwa na kutotoka nje ya Zanzibar.
Washtakiwa wengine waliopewa dhama na kulipa milioni tano kila mmoja, waraka wa mali isiyohamishika na wadhamini watatu ambao ni Hassan Abdalla mkaazi wa Michenzani na Khamisi Ali Abdalla.
Shahidi anaechunguza silaha kutoka makao makuu ya upelelezi Dar er Salaam Godfredi Luhamba akitoa ushahidi wake mahakamani hapo amesema silaha aliopelekewa kuichunguza aina ya SMG imeshawahii kutumika katika tukio jingine kabla la mauwaji hayo ya raia wa kichina.
Watuhumiwa wengine walirudirudishwa rumande hadi Mey 30 mwaka huu kesi hiyo itakaposikilizwa tena ni Abdulkadir Moh’d Saidi, Miraji Moh’d ,Salum Abdalla na Faki Ali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment