I made this widget at MyFlashFetish.com.

Friday, May 21, 2010

MASAUNI KUPOKEWA KWA SHANGWE ZNZ?


Jumuiya ya vijana ya chama cha Mapinduzi UV-CCM imesema haiuhusiki na maandamano yanayotarajiwa kufanyika kesho kwa ajili ya mapokezi ya mwenyekiti wa zamani wa jumuiya hiyo Hamad Masauni.
Kauli hiyo ya jumuiya imekuja kufuatia kuwepo kwa taarifa zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa umoja huo kutaka kuandaa mapokezi ya mwenyekiti huyo wa zamani aliejiuzulu hivi karibuni akidaiwa amejipunguzia umri.
Akizungumza na wandishi wa habari katibu wa vijana wa CCM Zanzibar Shamhuna Mohammed Ibrahim amesema jumuiya hiyo haijaandaa mapokezi ya aina yoyote kwa mwenyekiti huyo wa zamani.
Hivyo amewataka vijana kuacha kutumiliwa na wanasiasa wachache kwa lengo la kuchafua hali ya kisiasa ndani ya umoja wa vijana wa CCM.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari katika jumuiya hiyo kimesema lengo la mapokezi hayo ni kumfariji na kuonesha mshikamano wao kuwa bado wanampenda na kilichotokea ni bahati mbaya.

Waandaaji wa maandamano hayo walidai yatawashirikisha vijana wa mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba kwa kuvaa sare maalum.
Kujiuzuli kwa Masauni kutawafanya vijana wa CCM Zanzibar kutokikalia kiti hicho kwa muda mrefu tokea kuandoka Mohammed Seif Khatib ambaye sasa ni mbunge wa jimbo la Uzini na waziri anaeshughulikia masuala ya muungano.
Hamad Masauni ambae amejiuzulu pamoja na naibu katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Mohammed Moyo wanatazamiwa kutaka kuwania nafasi ya ubunge katika majimbo ya Kikwajuni na Kwahani mjini Zanzibar.
Hatua ya kujiuzulu kwa Masauni imetokana na taarifa zilizotolewa katika vyombo vya habari za kujipunguzia umri wakati wa kuwania wadhifa huo na Moyo amesema amejiuzulu kwa sababu zake binafsi.
Masauni na Moyo walichaguliwa kushika nyadhifa hizo mwishoni mwa mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment