I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, May 23, 2010

MASAUNI MASHAKANI

Jeshi la polisi nchini limesema linafanya uchunguzi wa nyaraka na vielelezo kuhusu umri wa mwenyekiti wa zamani wa jumuiya ya vijana ya chama cha mapinduzi UV-CCM, Hamad Masauni.
Hatua hiyo ya jeshi la polisi imekuja baada ya Masauni kudaiwa kuhushi umri wake wakati wa kugombea wadhifa huo mwaka 2008.
Naibu kamishna wa jeshi la polisi anekaimu ukurugenzi wa makosa ya jinai Piter Kibuyo amesema taarifa za vielelezo vya uchunguzi vitatolewa baada ya uchunguzi huo kukamilika.
Amesema katiba ya nchi inaeleza hakuna mtu alieko juu ya sheria hivyo iwapo Masauni ataonekana amehushi umri wake sheria itachukua mkondo wake
Masauni alitarajiwa kupokelewa leo kwa mapokezi ya aina yake, lakini umoja wa vijana wa UV-CCM, Zanzibar umesema hausiki na mapokezi hayo.
Uchunguzi uliofanywa na Zenji fm radio umegundua mapokezi hayo yaliandaliwa na baadhi ya vijana wa CCM kutoka jimbo la uchaguzi analoishi Masauni.

No comments:

Post a Comment