Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kuwachukulia hatua za kisheria askari polisi na madaktari wanaopoteza ushahidi wa kesi za makosa ya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto
Akizungumza katika mdahalo wa wazi wa siku ya Umoja wa Ulaya EU afisa wa wanawake na watoto wilaya ya Kaskazini ‘A” Mwajuma Kassim amesema licha ya watuhumiwa wa makosa hayo kukubali makosa yao, lakini baadhi ya watendaji wa taasisi hizo wanapoteza ushahidi kwa kile achodai maslahi yao binafsi.
Amesema hali hiyo imewafanya baadhi ya watuhumiwa kuendelea kufanya vitendo hivyo huku wakidhani wakipelekwa kwenye vyombo vya sharia huachiwa huru kwa kutokuwes na kesi ya kujibu.
Bi mwanajuma amefahamisha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hasa watoto vimeongezeka katika wilya ay Kaskazini ‘A’ hivyo ameiomba serikali kuwa makini na uposhaji wa ushahidi dhidi ya watuhumiwa.
Hata hivyo afisa huyo hakutoa takwimu halisi juu ya matukio ya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya watoto, lakini pio ameonya juu ya kushamiri kwa matukio ya kuwapa mimba wanafunzi.
Mdahalo huo wa siku moja uliofanyika katika chuo kikuu cha Zanzibar SUZA umeandaliwa kwa ushirikiano wa umoja wa Ulaya EU na chama cha wandishi wa habari wanawake TAMWA pia umehudhuriwa na balozi wa EU Tim Clark.
Tuesday, May 11, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment