I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, May 2, 2010

KARUME ASEMA SERA YA KUONGEZA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI ITAKUWA TAYARI JUNE MWAKA HUU 2010


Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amesema serikali inaendelea kutayarisha sera ya utumishi wa umma itakayowezesha kupandisha mishahara ya wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi kulingana na hali ya maisha.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani huko hoteli ya Bwawani amesema utayarishaji wa sera hiyo ni miongoni mwa mageuzi ya mfumo wa utumishi wa umma unaofanywa na serikali kwa kushirikiana na shirika la kazi duniani ILO.

Amesema mfumo huo wa utumishi wa umma utakaozingatia maslahi ya watumishi wa taasisi za serikali na sekta binafsi pia utahusisha upandishaji wa pencheni kwa wastaafu utakamilika June mwaka huu.

Dr. Karume amesema serikali inaendelea kutatua matatizo ya wafanyakazi na kusema sehemu kubwa ya matatizo hayo yameshapatiwa ufumbuzi ikiwemo ulipaji wa mishahara kwa wakati na mafao ya wafanyakazi wanaostaafu…

Aidha rais Karume amewataka vijana na wafanyabiashara kuzitumia fursa za soko la pamoja la nchi wananchama wa jumuiya ya Afrika kamshariki E.A.C ili kuendelesha shughuli za biashara na kutafuta ajira.

Amesema wizara ya kazi imeshaweka kitengo cha kuwandaa vijana kuingia katika soko hilo na kuzitaka taasisi nyingine kujenga mazingira yatakayowawezesha wazanzibari kulitumia soko hilo.

Katika maadhimisho hayo Dr. Karume alipokea maandamano ya wafanyakazi na kuwazawadia wafanyakazi bora 76 fedha taslimu na vyeti.

Siku ya wafanyakazi duniani inadhimishwa Mei Mosi ya kila mwaka duniani kote ili kuwakumbuka zaidi ya wafanyakazi mia moja na 20 waliouwawa mwaka 1889 katika jimbo la Chicago nchini Marekani walioandamana kudai haki zao.

No comments:

Post a Comment