I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, May 10, 2010

KUJIANDIKISHA SASA BASI

Tume ya uchaguzi Zanzibar imesema imefunga rasmi kazi za uwandikishaji wa wapiga kura na kuendelea na matayarisho ya uchaguzi.
Taarifa ya tume hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema baada ya kukamilika kwa kazi za uandikishaji, na ubadilishaji wa shahada za kupigia kura tume hiyo inaendelea na kazi za uhakiki wa majina ya wapiga kura waliosajiliwa katika awamu zote mbili.
Taarifa hiyo imesema kazi hizo zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha wapiga kura kwa siku saba ambapo wananchi watapata nafasi ya kuangalia majina yao pamoja na kutoa pingamizi kwa watu wanaowatilia mashaka.
Tume ya uchaguzi Zanzibar imesema baada ya kukamizika na pingamizi zote kushughulikiwa kisheria kutafanyika uchapishaji wa shahada za kupigia kura na kuwataka wananchi kuzihifadhi risiti zao ili kupatiwa shahada hizo.
Uchaguzi mkuu wa Zanzibar utakao wachaguwa madiwani, wawakilishi na rais wa Zanzibar unatarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment