Tuesday, April 13, 2010
ZOEZI LA UANDIKISHAJI NA MIZENGWE YAKE
Awamu ya pili ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura unaoendelea visiwani Zanzibar umekumbwa na malalamiko ya kutokuandikishwa kwa baadhi ya wananchi wenye sifa zote zilizowekwa kisheria pamoja na kukataliwa na masheha wakidai hawawatambui au hawako katika shehia husika.
Mwangaza wa habari wa Zenj fm ilibahatika kuzungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Cuf taifa na Mwakilishi wa Kuteuliwa Juma Duni Haji ambaye ametoa malalamiko kutokana na vitendo walivyofanyiwa baadhi ya wananchi ambao walijitokeza katika uandikishaji huo na kukataliwa.
Naibu katibu mkuu huyo wa CUF anazungumzia jinsi zoezi la uandikishaji lilivyokuwa katika maeneo ya Chumbuni, Kituo cha Mabanda ya ng’ombe ambako uandikishaji wake ulifikia tamati kwa siku ya jumapili iliyopita Bonyeza Hapa kumsikia Bw JUMA DUNI
Kufuatia malalamiko hayo Mwangaza wa habari ulimtafuta afisa habari wa tume ya uchaguzi Zanzibar Maalim Idrissa Haji Jecha mabae amesema kuwa tume ya uchaguzi inafanya juhudi za kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapatiwa haki yake kwa vile tume na maafisa wake hawana mamlaka ya kumkatalia mtu bila sababu za msingi Bonyeza hapa kumsikia Bw IDRISSA HAJI JECHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
haya tena zumari imepigwa wachezaji mpooooo....
ReplyDeletemi nadhani siasa za zanzibar ni danganya toto tu na hawa jamaa zangu wa cuf tayari wameingizwa mkenge kwa kisingizio cha serikali ya umoja wa kitaifa,hata kuwatetea wananchi imekua bac kwani ukiangalia utaona jinsi gani wazanzibar wanavyonyimwa haki yao ya kujiandikisha,lakini wabara hao hao wanaokuja kwa msimu wa utalii tu jinsi wanavyopewa kipaumbele
ReplyDelete