AHMED, mtoto wa Rais wa Zanzibar , Amani Abeid Karume, ametumbukia kwenye kashfa ya kunyang’anya ardhi baada ya kupora shamba kubwa Kaskazini Unguja, NIPE HABARI, limearifiwa.
Mtoa habari wa eneo hilo , alisema kwamba malalamiko yao serikalini kupitia Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid, akidai ya kuwa “Ahmed Amani Abeid Karume amevamia shamba lao.”
Mlalamikaji huyo alitoa madai hayo kupitia kituo cha Redio cha Zenj FM, akisema: “Sisi ni wamiliki wa shamba la huko, lakini limevamiwa na mtu anayeitwa Ahmed Amani Abeid Karume,” lakini watendaji husika serikalini hawaonyeshi kushtushwa.
Mdai huyo, Bi Fatma Ali kutoka familia ya Mzee Diku ya Nungwi, alisema ameshutushwa na kuvamiwa kwa shamba usiku wa manane na mafundi waliojitambulisha kuwa “Wametumwa na Ahmed Amani Abeid Karume.”
“Sisi tuna nyaraka za muda mrefu kumiliki eneo hilo ambalo hatulitumii,” alisema na kuonyesha nyaraka hizo zenye namba ya usajili 1783 uliotolewa 22 Desemba, 1935.
“Tukienda kwa wahusika tunambiwa kuwa amechukua mtoto wa mkubwa,” alisema Bi. Fatma na kuongeza: “Mtoto huyu amepeleka mafundi usiku wa manane ili kuanza kazi ya kujenga.”
Alisema: “Tayari ameshapeleka suala hilo kwa viongozi wote akiwemo waziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kuwaambia kuwa mtoto wa rais amepora ardhi ya raia wanyonge.”
Akielezea hatua alizozichukua ni pamoja na kuwauliza viongozi wote akiwemo Sheha wa Nungwi pamoja na kupeleka barua hata kwa Waziri Kiongozi, Shamvi Vuai Nahodha, lakini hata hivyo taarifa zinasema kwamba waraka wao haukufika.
Alisema japo aliandika barua kwa waziri ilichukua muda mrefu bila ya kupata majibu na zaidi anaona mafundi wamepelekwa kuanza ujenzi unaoonekana utakuwa wa gharama kubwa.
Sheha wa eneo hilo, aliwambia: “Mtoto wa rais ndiye alikuja na maofisa wa Ikulu pamoja na mkuu wa kutuo cha polisi Nungwi na kutuambia kuwa alipewa shamba hilo kwa barua ya mkurugenzi wa ardhi.”
Hata hivyo, Mzee Diku, alisema: “Hakuna chochote tulicholipwa.”
Fundi Mkuu wa ujenzi huo, Abdallah Mkanda alithibitisha: “Ndio, kweli tumetumwa na mtoto huyo wa rais.”
Alikubali kusitisha ujenzi mpaka “tajiri wao”, Ahmed Aman Abeid Karume, atakapokwenda kumaliza matatizo hayo huku akisema: “Sisi tumepewa kila aiana ya msaada tunaotaka ili waweze kuanza kazi, lakini tulikuja hapa usiku kwa sababu tulichelewa kupeleka vifaa katika eneo hilo .”
Sheha wa shehia hiyo ya Nungwi amefafanua, alikubali kuwa “mashamba hayo ni mali halali kwa watu wa Nungwi kwani yanalengwa kugaiwa kwa wazaliwa wa eneo hilo tu.”
Akifananua kuwa eneo hilo , lilikuwa limetolewa kwa Kaligendo kabla ya kupewa Nungwi Peninsula ambao wote walishindwa kuliendeleza ndipo akapewa Ahmed.
Lakini akasema: “Utaratibu huu sasa mimi nimeukuta na masheha wenzangu wameniambia kuwa watu wameshalipwa, lakini naogopa kulalamika kwa kuwa mtoto wa rais,” alisema sheha huku akionyesha kuishiwa nguvu juu ya suala hilo .
“Mimi najua kuwa kweli shamba hili amepewa Ahmed, lakini mimi nalaumu watu wa wizara ya ardhi kwa kuwagawa eneo hilo bila ya kuwatarifu wale wanaolishughulikia eneo hilo .”
Akaifafanua juu ya kadhi hiyo sheha huyo amesema: “Kwa kweli, kutokana na mkono wa rais kuwako hapa, sina la kusema hata kidogo. Kashapewa mtoto wa rais, mimi sina mkono wangu,” alisema sheha aliyeteuliwa mwaka 2008 katika shehia hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bw. Pemba Juma Khamis, alisema hajapokea malalamiko bali amesikia tu kwa watu, lakini alifafanua kuwa eneo hilo amepewa mtu nyeti kabisa lakini ukweli suala hili tukukutane mimi na wewe nitakwambia juu ya ukweli wa suala hilo .”
Akizungumza kwa pozi na taratibu, Waziri Himid, alisema kwa ukali wa maneno: “Kweli nimelipokea suala hili, lakini anahitaji muda kulishuhulikia suala hili kwa umakini zaidi.”
Juhudi za kumpata moja kwa moja Ahmed, zilishindikana lakini kama yake, Abeid aliyeombwa kumsaka pengine atoe majibu, akasema: “Sijampata kwenye simu hivyo tutafanya jitahada zaidi kumtafuta juu ta suala hilo .”
Safu hili lilimsaka tena Abeid Karume, saa chache kabla ya kuingia mtamboni, kwa mara pili, alijibu: “Bado sijampata.”
Friday, April 9, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Eti sheha mzima anasema kuna mkono wa rais kwaio hawezi kuingilia!!!! hiii aibu jamani!! kwa kuwa mtoto wa rais tena ndo afanye atakavyo!! Zanzibar haitoendelea maisha kwa mchongo uo,tutakufa na umaskini wetu uko
ReplyDeleteInauma sana eti maeneo yetuwanafanya kama nisehemu zao za urithi. nakuapieni kwa mwendo huu kitafika kiama zanzibar hatuendelei, ninchoamini sio kweli kama serikali imeshindwa kumpata huyo bwana mdogo, pili kama nisehemu yake kwanini awe hayuko tayari kjiweka wazi kwenye vyobo vya bahari ili ukweli ueleweke, haki ya m2 ni duniani, akhera huenda hesabu.
ReplyDeleteni mimi Ali Diku ktukoa nungwi \email : ally.diku@yahoo.com
Inauma sana eti maeneo yetuwanafanya kama nisehemu zao za urithi. nakuapieni kwa mwendo huu kitafika kiama zanzibar hatuendelei, ninchoamini sio kweli kama serikali imeshindwa kumpata huyo bwana mdogo, pili kama nisehemu yake kwanini awe hayuko tayari kjiweka wazi kwenye vyobo vya bahari ili ukweli ueleweke, haki ya m2 ni duniani, akhera huenda hesabu.
ReplyDeleteni mimi Ali Diku ktukoa nungwi \email : ally.diku@yahoo.com
Ali Diku, pengine huyo Ahmed Karume alitaka kumpa shamba zawani kwa mke wake aliyemuoa July 2010. Harusi ilikuwa kubwa. Ungempata siku ile ungekwenda State House and kufanya protest nje. Wageni wa harusi wangepata message.
ReplyDelete