Sunday, April 11, 2010
UWANDIKISHAJI PEMBA WAENDELEA VIZUZI
Kazi za uwandikishaji awamu ya pili katika daftari la kudumu la wapiga kura kisiwani Pemba zimeelezewa kwenda vizuri huku kukiwa na idadi kubwa ya watu wanaojiandikisha.
Afisa Uandikishaji Wilaya ya Chake Chake Rashid Suleiman Omar amesema wafanyakazi wa tume ya uchaguzi wamekuwa wakipata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi wa maeneo ya uandikishaji.
Amesema wananchi wote wenye sifa wanaandikishwa na hakuna mtu ambae anasifa na aliekosa haki yake ya kujiandikisha kama mpiga kura na kuwataka wananchi wenye sifa kujitokeza katika uandikishaji huo unaoendelea katika wilaya ya Chakechake.
Katika jimbo la Chakechake jumla ya wananchi elfu nne, 438 wa Shehia tisa za jimbo hilo wamejiandikisha wakiwemo wanawake elfu mbili, 388.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hapo juu mumekusudia unaendela virusi vya ukimwi? au vipi muwe waangalifu kwenye habari zenu , jitahidi mwanzo mgumu mtafika
ReplyDeletea/a tumefurahi kuuna hii habari kuhusu zenj fm zanzibar lakini mbona hatuisikii tunaomba mtufahamishe ili tuweze kusikiliza asante ALI
ReplyDelete