I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, October 31, 2010

UCHAGUZI WA ZANZIBAR 2010

Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC imesema inatarajia kutangaza Matokeo mara baada ya kupokea Majumuisho ya Fomu zilizosainiwa na Mawakala kwa Majimbo mbali mbali ya Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC Salum Kassim Ali amesema hadi sasa hawajapokea Fomu yeyote ya Majumuisho licha ya kwamba Matokeo ya awali kubandikwa katika Vituo mbali mbali vya uchaguzi.
Amesema kitu ambacho kimejitokeza ni Mawakala vyama katika Majimbo kutosaini Fomu husika za Uchaguzi. Leo ndio uchaguzi umefanyika nchi nzima licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo zilizosababisha baadhi ya majimbo maa 4 ya unguja na pemba ya ubunge na wadi tisa kwa Zanzibar kutofanyika kutokana na hitilafu za karatasi za kupigia kura

No comments:

Post a Comment