Wananchi wa Tanzania wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa rais, bunge, uwakilishi na udiwani Jumapili ya tarehe 31 Octoba mwaka 2010.
Uchaguzi huo wa nne wa vyama vingi vya siasa kwa upande wa Zanzibar unaonekana kuwa na mchuano mkali kati ya mgombea wa urais wa CCM Dr. Ali Mohammed Shein na mgombea wa CUF Seif Sharif Hamad.
Jumla ya wapiga kura laki nne, elfu saba, 658 kwa upande wa Zanzibar watapiga kura kuwachagua wagombea urais wa jamhuri ya muungano Tanzania, urais wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani katika vituo vya kupigia kura vipatavyo elfu moja, 291 Unguja na Pemba.
Na huko Tanzania bara wapiga kura watawachagua wagomea urais wa jamhuri ya muungano, wabunge na madiwani. Kampeni za uchaguzi huo mkuu zinatarajiwa kumalizika rasmi hapo kesho
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetenga zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kugharamia uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Sunday, October 31, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment