TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR IMEAHIRISHA UCHAGUZI KATIKA WADI NNE ZA MKOA WA MJINI MAGHARIBI
Tume ya uchaguzi Zanzibar imeahirisha uchaguzi wa madiwani katika wadi nne za mkoa wa mjini magharibi kutokana na kukosewa kwa uchapishaji wa karatasi za kupigia kura kwa wagombea hao.
Akizungumza na waandishi wa habari huko hoteli ya Bwawani mkurugenzi wa tume hiyo Salum Kassim Ali amezitaja wadi hizo ni Mchangani jimbo la Mji mkongwe, Kwahani jimbo la Kwahani, Miembeni jimbo la Kikwajuni na wadi ya Nyerere jimbo la Magomeni.
Amesema hali hiyo inatokana na baadhi ya majina ya wagombea kuonekana katika wadi ambazo hawahusiki kupigiwa kura na baadhi ya wapiga kura kulazimika kupiga kura wadi sio zao.
Hata hivyo mkurugenzi huyo amesema uchaguzi wa madiwani katika wadi hizo utafanyika Jumapili ijayo tarehe 28 mwezi ujao na hakutakuwa na kampeni wala uteuzi wa wagombea.
Wakati huo huo Ali amesema vifaa vya kupigia kura zikiwemo karatasi za kupigia kura tayari vimeshasambazwa katika vituo vyote vya kupigia kura vya Unguja na Pemba vipatavyo elfu moja, 291.
Uchaguzi mkuu wa nne wa Zanzibar wa mfumo wa vyama vingi unatarajiwa kufanyika kesho ambapo jumla ya wapiga kura laki nne elfu saba, 658 watapiga kura kuwachagua wagomea urais wa Zanzibar, muungano, wawakilishi, wabunge na madiwani.
Sunday, October 31, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment