Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dr. Jakaya Kikwete ameahidi kulipatia ufumbuzi tatizo la uchimbaji wa mafuta ya Zanzibar katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Amesema matatizo mengi yaliodaiwa kuwa kero ya muungano tayari yameshapitiwa ufumbuzi, kupitia kamati ya pamoja ya waziri mkuu na waziri kiongozi na maeneo yaliobakia ikiwemo suala la uchimbaji wa mafuta ya Zanzibar kuondolewa katika muungano litapatiwa jawabu…
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo Zenji Fm radio imetangaza moja kwa moja rais Kikwete pia ameahidi kuimarisha sekta ya uwekezaji ili kulipatia ufumbuzi tatizo la ajira.
Amesema tatizo la ajira kwa vijana bado ni kubwa nchini, lakini amesema endapo atachaguliwa tena kuiongoza Tanzania serikali yake itawavutia wawakezaji kwa kuwawekea mazingira mazuri.
Rais Kikwete amesema mpango huo utakwenda sambamba na kuwawezesha wakezaji wazalendo kwa kuwapatia mikopo ya kuwekeza katika viwanda, huduma na biashara ili kusaidia ukuwaji wa uchumi.
Aidha Dr. Kikwete amesema serikali yake itaanzisha benki ya wakulima na kuongeza fedha katika taasisi za fedha zinazotoa mikopo yenye masharti nafuu ili kuwawezesha wananchi kujiajiri na kuwajiri wengine…….)
Sunday, October 31, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment